Heche: Hatuko tayari kutumiwa kulaghai

Heche: Hatuko tayari kutumiwa kulaghai

Mawele

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
912
Reaction score
3,161
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amesema Chama hicho kinaendelea kushikilia msimamo wake thabiti kuhusu masuala ya haki na uwajibikaji kufuatia matukio yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akisisitiza kuwa haki haihitaji kusukumwa bali hujitokeza yenyewe pale inapochunguzwa kwa kina.

Akizungumza katika mahojiano maalum na AyoTV, Heche ameweka wazi kuwa Chama hicho hakiko tayari kushiriki katika mchakato wowote ambao wanaona hauwezi kutoa majibu ya kweli kwa Watanzania, akieleza kuwa kuna mambo muhimu ambayo bado hayajapatiwa ufafanuzi wa kuridhisha.

Aidha ameongeza kuwa msimamo wa Chama chake unalenga kuhakikisha kuwa hatua zinazochukuliwa zinakuwa na uwazi na zinajibu maswali ya msingi yanayogusa maisha na haki za Watu, huku akisisitiza kuwa bila ukweli wa kina, hakuna suluhisho la kudumu linaloweza kupatikana.

Katika hatua nyingine, Heche ameeleza kuwa tofauti za kisiasa haziwezi kuvunja mahusiano ya kifamilia, akibainisha kuwa hata ndani ya Familia yake kuna Watu wenye mitazamo tofauti ya kisiasa, jambo ambalo halijawahi kuathiri uhusiano wao wa kindugu huku akiendelea kusisitiza umuhimu wa kuheshimu haki na misimamo ya kila upande.
 

Attachments

Wenzake akili zao ukitofautiana nao kiitikadi hustahili kuishi
 
Mbona media zenye uelekeo wa kichawa zinaanza kuwapa airtime chadema?

Sawa kuna kipindi walifungiwa, lakini.
 
Back
Top Bottom