Wakuu Je, ni kweli Heche amesema wao Oktoba wwanatiki?
- Tunachokijua
- John Heche ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Taifa. Heche na viongozi wengine wa chama hiko wanaendelea na kampeni yao ya No reforms No election katika mikoa mbalimbali nchini.
Wakati kampeni hiyo ikishika kasi kumeibuka kampeni nyingine iitwayo “Oktoba Tunatiki” ikiwa na dhamira ya kuhamisisha watu kushiriki katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwezi wa 10 2025.
Madai
Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Facebook kumekuwapo na taarifa inayoambatana na grafiki inayoonekana kuwa na nembo ya Nipashe ikiwa na ujumbe unaosomeka “Heche: Sisi CHADEMA Octoba Tutatiki” grafiki hiyo imesambazwa kuanzia
Uhalisia wa taarifa hayo
JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kubaini kuwa si ya kweli na wala haijachapishwa na Nipashe katika mitandao yao ya kijamii Juni 9, 2025.
JamiiCheck imefuatilia mikutano aliyoifanya John Heche Juni 9, 2025 na kubaini kuwa hakutamka maneno hayo kuwa wao watatiki Oktoba kuashiria kushiriki uchaguzi. Katika mikutano yote Heche alihimiza kuwa bila mabadiliko hakutakuwa na uchaguzi.
Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao pia umebainisha kuwa John Heche hakuchapisha maneno yenye kuashiria wao kushiriki uchaguzi ama kutiki Oktoba, aidha taarifa hiyo haijachapishwa wala kutolewa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya chama hicho.
Inayoonekana kuwa grafiki ya Nipashe digital pia ni ya kughushi kwani haijachapishwa na chombo hicho cha habari na pia aina ya mwandiko “font” iliyotumika ni tofauti na inayotumiwa na chombo hicho.