Hata mimi nimeliona tatizo hilo, kwa mazingira ya nchi watu waliokuwa wamelala na kuzoea siasa za propaganda bila kupitisha amshaamsha ya nchi nzima ni ngumu. Bila kupiga debe la nguvu watu bado wanaamini ccm ni chama cha wakulima na wafanyakazi kumbe hizo nembo zimebaki kwenye bendera, sasa hivi ni chama cha wafanya biashara tena nyingi ni zisizo halali kama mikataba isiyo na tija kwa nchi, wanyama kuuzwa kinyemela na mauaji ya tembo, unga ndio imekuwa dili kubwa kwenye chama hicho. Uwezo wa kushawishi kama wa Nyerere watu wajitolee kujenga nchi haupo na kujenga hoja umewaishia bali wamebaki kutumia jeshi kulazimisha mambo. Ama Bavicha Iimekabidhiwa kwa Checkbob anayejivunia elimu ya vitabuni bila kuleta mtaji wa watu. Tunataka watu sio kushinda ofisini kupitia mafaili wakati watu hawajui. Hivi bavicha wameshindwa hata kukusanya dhuluma zilizofanyika nchi nzima kwenye uchaguzi wa s/m na kuueleza umma na dunia kwa ujumla. Au mnangoja mpaka mauji yatokee huko mbeleni ndio mjifanye kulialia. Watu wanatishiwa, kuumizwa na hata kuuwawa wakitekeleza wajibu wao wa kikatiba nyinyi mnakaa kwenye viyoyozi mnaangalia tv, kuchat kwenye facebook na miwhatsapp!!! Au mnangoja wazee wa kina Slaa waitishe maandamano ndio mvae magwandwa?
Nendeni mahakamani kama vijana ili tuone mahakama ikiepuka wajibu wake hapo umma utakuwa tayari kuchukua hatua. Au mimi ndio sijui wajibu wa bavicha? Muda wa kujipaka manukato na kutembea na kalamu na milaptop sio huu. Vijana ndio dira ya nchi na sio akina Slaa. Hao akina Slaa wabaki washauri tu. Au mmelewa ile propaganda ya vijana ni taifa la kesho!!?