HECHE ALIDHANI MAHAKAMA NI KIJIWE CHA KAHAWA?

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
783
Reaction score
694
Mwenendo wa kesi inayomkabili Tundu Lissu umeibua maswali mengi kuhusu namna shahidi wake John Heche, alivyokuwa amejiandaa kabla ya kufika mahakamani. Maswali ya Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, yaligusa mambo muhimu ya Katiba, uchaguzi, hati ya mashitaka na misingi ya sheria. Katika baadhi ya majibu yaliyonukuliwa, Heche alionekana kutokuwa tayari au kutokuwa na majibu ya kina kuhusu maswali hayo.

Kinachoibua mjadala ni juu ya maswali mengi anayoulizwa Heche anajibu HAJUI, HAJUI, HAJUI! Imefika kipindi mpaka Tundu Lissu alimwambia kwamba hapa mahakamani unatakiwa ujibu maswali sio kusema hujui. Jambo hili limeleta aibu kubwa.

Mahakama si sehemu ya mazungumzo ya kawaida. Shahidi anapoitwa kutoa ushahidi, kila jibu linaweza kuchambuliwa, kulinganishwa na nyaraka, video au taarifa nyingine zilizowasilishwa mbele ya Mahakama. Ndiyo maana shahidi asiyejiandaa anaweza kukutana na maswali magumu sana na ya kumfedhehesha kama ilivyotokea kwa John Heche.

Kwa mtazamo wa mjadala wa umma, mtu anaweza kujiuliza, je, Heche alifahamu kikamilifu uzito wa kwenda kutoa ushahidi katika kesi ya aina hii au alikurupuka tu? Kama angejua mapema kwamba mchezo unakuwa namna hii bila shaka angetia mpira kwapani, asingekubali kuwa shahidi, kwani Mahakama si mahali ambako John Heche hutamba na kuwadanganya wenzie.

Mahakamani kinachoangaliwa si kelele za nje ya Mahakama, bali ushahidi, maswali na majibu yaliyorekodiwa pamoja na sheria zinazotumika. Mahakama si kijiwe cha kahawa ambako mtu anaweza kusema jambo leo na kesho asikumbuke.
IMG-20260916-WA0051.jpg
 
Mwenendo wa kesi inayomkabili Tundu Lissu umeibua maswali mengi kuhusu namna shahidi wake John Heche, alivyokuwa amejiandaa kabla ya kufika mahakamani. Maswali ya Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, yaligusa mambo muhimu ya Katiba, uchaguzi, hati ya mashitaka na misingi ya sheria. Katika baadhi ya majibu yaliyonukuliwa, Heche alionekana kutokuwa tayari au kutokuwa na majibu ya kina kuhusu maswali hayo.

Kinachoibua mjadala ni juu ya maswali mengi anayoulizwa Heche anajibu HAJUI, HAJUI, HAJUI! Imefika kipindi mpaka Tundu Lissu alimwambia kwamba hapa mahakamani unatakiwa ujibu maswali sio kusema hujui. Jambo hili limeleta aibu kubwa.

Mahakama si sehemu ya mazungumzo ya kawaida. Shahidi anapoitwa kutoa ushahidi, kila jibu linaweza kuchambuliwa, kulinganishwa na nyaraka, video au taarifa nyingine zilizowasilishwa mbele ya Mahakama. Ndiyo maana shahidi asiyejiandaa anaweza kukutana na maswali magumu sana na ya kumfedhehesha kama ilivyotokea kwa John Heche.

Kwa mtazamo wa mjadala wa umma, mtu anaweza kujiuliza, je, Heche alifahamu kikamilifu uzito wa kwenda kutoa ushahidi katika kesi ya aina hii au alikurupuka tu? Kama angejua mapema kwamba mchezo unakuwa namna hii bila shaka angetia mpira kwapani, asingekubali kuwa shahidi, kwani Mahakama si mahali ambako John Heche hutamba na kuwadanganya wenzie.

Mahakamani kinachoangaliwa si kelele za nje ya Mahakama, bali ushahidi, maswali na majibu yaliyorekodiwa pamoja na sheria zinazotumika. Mahakama si kijiwe cha kahawa ambako mtu anaweza kusema jambo leo na kesho asikumbuke.View attachment 3671868
Ushahidi wa uongo hata mimi nijibu "SIJUI"Kautga aendelee na majungu yake.
 
Back
Top Bottom