Hebu tuweni wakweli hasa wadada.

Husninyo

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
23,723
9,189
Hivi jamani, elimu sio kigezo cha kuangalia unapotaka kuingia kwenye mahusiano ya kudumu (ndoa).
Mdada unaweza kuolewa na mwanaume ambae hajaenda shule kabisa au ameishia shule ya msingi?
 
Ngoja tusubiri wadada mnavyochambua ili nasi midume tujitambue.
naona hii imezingatia gender, nimepita tuuu....
 
hapa sasa uanzungumzia personal likes/dislikes. lakini assumption ni kua kila mtu anapenda mainsha bora so wengi wanpenda watu wenye elim though pia ni fact kua sio kila mwenye elim ana maisha bora.
Kwa mimi naeza oa hata darasa la pili.kigzo cha elim sio kikuu sana kwangu ingawa ningependa kama nitabahatika kumpata mwenye elim.
 
Hivi jamani, elimu sio kigezo cha kuangalia unapotaka kuingia kwenye mahusiano ya kudumu (ndoa).
Mdada unaweza kuolewa na mwanaume ambae hajaenda shule kabisa au ameishia shule ya msingi?
:A S 112: kwa vigezo vyenu hivyo ndo maana WADADA WENGI "WAMEDODA" MITAANI! cha msingi ni kuwa mtu ni muelewa, na ana mapenzi ya dhati!
 
Kuna kufol in lov wanasema hata kama ni mpiga debe hajasoma anaweza akazmikiwa na demu msomi na mwenye shule.
Wanawake wengi hawaangalii shule wanaangalia sana sana ngawira ie men unapomtongoza dem hakuuliz una mastaz, phd, diplona, certficate au degree! Weng utasikia una gari gani, una nyumba wap, unafanya kaz gani/wap au unabiashara gani
kwa mtazamo wangu elimu kwa weng siyo muhmu kama cash
MIMI NI MWANAUME YAMENIKUTA NA DEMU AKISHAANZA KUULIZIA CASH NAMPIGA CHINI FASTA!
 
tatizo ni pale "UNAPO FALL IN LUV" wapaswa " ku ENTER IN LUV" Pia kama ulitanguliza kash lazima ukubali!:rain:
 
Ndoa ni hitaji la moyo wa mtu na pia anategemea impe furaha ya maisha yake hapa duniani. Furaha ndani ya ndoa ni mkusanyiko wa mahitaji ya hisia za ndani za mtu pamoja na maisha ya kawaidi ya hapa duniani. Maisha ya kawaida hapa dunia kwa sasa yanategemea ajira na sehemu kubwa ya ajira zinahitajia elimu hivyo watu wenye maisha ya wastani au ya juu sehemu kubwa ni walio soma. Kutokana na kipengele cha maisha ya kawaida ndani ya ndoa kigezo mojawapo cha kuchagua mwenza kinakuwa ni mtu mwenye uwezo wa kukabiliana na changamoto za maisha ya kawaida ndani ya ndoa, ambapo watu waliosoma wanafasi kubwa zaidi kutokana na kuwa na ajira za uhakika ukilinganisha na wengine. Pia kumbuka sehemu kubwa ya maisha ya ndoa siyo mapenzi bali ni majukumu ya kaiwaida ya maisha ambayo yahitaji kipato ili uweze kukabiliana nayo. Kutoka ma maelezo mafupi niliyo yatoa elimu ni miongoni mwa vigezo ambavyo vipo ndani ya mioyo ya wanadamu kote duniani wakati wa kuchagua mwenza japo wengi ukiwauliza watakudanya siyo wakati ukweli ndio huo.

Note: Kama hukuwekeza kwenye elimu nafasi ya kupata msomi pia ni ndogo, kwa hiyo wekeza elimu kwa mtoto wako wa kike ili aje furahia maisha atakapo kuwa mtu mzima.
 
Inawezekana sana tu Hus!Swala ni maelewano na uwezo wa kufikiri kuendana tu!Kuna watu wamesoma ila kuelewana nao ni ngumu balaa,na uwezo wao wa kufikiri hauendani na elimu waliyo nayo ila unakuta mtu wa std 7 au form 4 yuko juu zaidi!Besides kwasababu mtu hajasoma haina maana hana akili...unaweza kuta hakua na uwezo wa kuendelea tu ila ni kichwa sana!
 
Mwanamke ukiwa na uhusiano na mwanaume ambae hajasoma anakuwa na ma infiriority ya kufa mtu sijui kwa nini, wapo wanapendana na wa hivyo ila wengi wao wanakuwa na wakati mgumu sana kwenye mahusiano, kila unachofanya utasikia unaambiwa unafanya kwa kuwa wewe ni msomi. Ila kuna wachache wanabahatika uhusiano unakuwa mzuri tu.
 
mi siangaliii kidato kwa kweli, napenda mwanaume msafi na anayemthamini mwanamke(that is enough for me), ikitokea anangawira poa, asipokuwa nazo pia poa coz im so independent.sijali kama ana uume mkubwa au mdogo as long as will love each other(true love and faithful).
 
Inawezekana sana tu Hus!Swala ni maelewano na uwezo wa kufikiri kuendana tu!Kuna watu wamesoma ila kuelewana nao ni ngumu balaa,na uwezo wao wa kufikiri hauendani na elimu waliyo nayo ila unakuta mtu wa std 7 au form 4 yuko juu zaidi!Besides kwasababu mtu hajasoma haina maana hana akili...unaweza kuta hakua na uwezo wa kuendelea tu ila ni kichwa sana!

Kwa wadada wetu inawezekana kinadharia zaidi, sio kivitendo
 
mi siangaliii kidato kwa kweli, napenda mwanaume msafi na anayemthamini mwanamke(that is enough for me), ikitokea anangawira poa, asipokuwa nazo pia poa coz im so independent.sijali kama ana uume mkubwa au mdogo as long as will love each other(true love and faithful).

Haaaa!
Mzuanda, hayo ya ukubwa au udogo wa naniliu umeenda mbali, ishu ni elimu tu
 
Hivi jamani, elimu sio kigezo cha kuangalia unapotaka kuingia kwenye mahusiano ya kudumu (ndoa).
Mdada unaweza kuolewa na mwanaume ambae hajaenda shule kabisa au ameishia shule ya msingi?

Kwani ndoa inakuwa na mafanikio ikiwa mwanaume kasoma sana? Mbona ndoa nyingi tu za wasomi zina matatizo chungu nzima na nyingine huishia kuvunjika? Wako wanaume ambao wameishia shule ya msingi na wana mafanikio sana katika maisha kwa sababu ni watu wanaojituma sana katika kufanikisha malengo yao ya kimaisha. Msipoteze bahati zenu za kuolewa kwa kuwakimbia wanaume ambao wameishia shule ya msingi, wengine wana mafanikio makubwa kimaisha na pia wanajua kuwajali wake zao na familia zao.
 
mimi naweza, awe tu na vigezo ambavyo vinafunika hilo la kukosa elimu....awe na bidii na anayependa kujiendeleza na mwenye akili ya kujua alipo na anataka kwenda wapi,anayeshaurika na ambaye kukosa elimu hakujamuondolea kujiamini kama mwanaume.
 
niingie kwenye ndoa na mwanaume aliyeishia la saba au ambaye hajaenda shule kabisa? for me hapana siwezi ila naweza kuwa na mwanaume ambaye nimemzidi elimu ( not la saba ) iwapo tuu huyo mwanaume awe anajiamini
 
Hus my dia tunaangalia upendo wadhati mengineo yanarekebishika mbele kwa mbele ndo maana una elimu ya watu wazima :wink2:
 
Mmmh!! Kwa wadada wa siku hizi, wanaangalia FUTURE kwanza LUV baadae!!
Niliwahi kuwa na limupenzi langu b4 sijapta kazi alkuwa na nyodo hata ukimuhitaji hadi umpigie GOTI!!!
Baada ya kupata kikazi duh hadi kero ikabidi nitimuke!!!!

Hivi jamani, elimu sio kigezo cha kuangalia unapotaka kuingia kwenye mahusiano ya kudumu (ndoa).
Mdada unaweza kuolewa na mwanaume ambae hajaenda shule kabisa au ameishia shule ya msingi?
 
wengi darasa la saba ni matajiri kuliko wa vyuo vikuu
na wengi wao wameoa wanawake wasomi na wazuri.....
 
Back
Top Bottom