Uchaguzi 2020 Hebu tujadili ukweli wa mambo haya kuhusu idadi ya wapiga kura Uchaguzi 2020

Papa1

JF-Expert Member
Apr 21, 2012
2,017
2,208
Mwaka 2015 kulikuwa na wapiga kura milioni 16. Leo tunaabiwa Kuna wapiga kura milioni 29, yaani nyongeza ya wapiga kura milioni 13 ndani ya kipindi cha miaka mitano.

IDADI YA WAPIGA KURA:

Toka tupate uhuru, mpaka wakati wa uchaguzi uliopita idadi yawatu ilikuwa milioni 56, wapiga kura milioni 16 sawa na asilimia 28.6%. ya watu wote wa Tanzania. Ndani ya miaka mitano tu, wapiga kura wameongezeka kutoka milioni 16 hadi milioni 29 huku idadi ya watu ikikaribia milioni 60. Wapiga kura Sasa Ni asilimia 50% ya watanzania wote huku tukijua kuwa watoto chini ya miaka 18 walivyojaa mashuleni, achilia mbali wasiojiandikisha.

Kumbukumbu kuwa watu waliisha at tamaa ya uchaguzi kufuatia figisufigisu zinazoendelea ktk chaguzi za siku hizi haza za serikali za mitaa zilizopita, na pia kitendo Cha CCM kupiga kampeni peke yao katika miaka yote mitano ya awamu ya uongozi was ngumi ya chuma. Hakukuwa na mwitikio mkubwa wa watu kujiandikisha kwa wapiga kura wapya, na wapiga kura wengi wa zamani wamekufa. We angalia takwimu za watoto waliozaliwa kijijini kwako linganisha na waliokufa.

Hofu yangu, wasiwasi wangu, nikweli idadi ya wapiga kura inaweza kuwa imeongezeka kwa asklimia 30% katika kipindi cha miaka mitano tu?

Hizi si takwimu za kujiwekea kura kibindoni za kuja kuongezea kwenye zitakazopatikana katika maboksi ya kura halali?

AJIRA:

Tunaambiwa serikali imetengeneza ajira ya watu milioni 6!!. Kweli kabisa hili linaingia akilini mwa mtu makini? Hawa Ni wanajeshi?, Ni waalimu?, Madaktari?, Machinga?, Polisi?, Wachimba migodi? Wafanyakazi viwandani au Ni watu gani hao. Kila mtu aangalie Ni jirani yake yupi kaajiriwa na yupi kapoteza kazi! Sioni uhalisia wa Jambo hili.

Mimi naona timu za ligi kuu zinapunguzwa, wachezaji na makocha wanapoteza kazi.

Naona korona inafuta watu kazi,

Naona TRA wanafukuza wawekezaji

Naona maduka yanafungwa

Sasa nasikia idadi ya ajira itafika hadi milioni 8. Hao wahitimu wanatoka wapi?
 
Hivi CHAUMA wanaanza lini kampeni?

Si wengine tunataka kula wali tu.
 
Mkuu Uzi wako unafikirisha sana, Hapa ilitakiwa kuhakikiwa kwa hao wapiga kura kwanza, Maana Ni wazi Kuna wapiga kura hewa wametajwa.

Pili huu Upinzani kugawana kura bila kujiunga naona kabisa Upinzani unapoteza muda,
 
Mkuu Uzi wako unafikirisha sana, Hapa ilitakiwa kuhakikiwa kwa hao wapiga kura kwanza, Maana Ni wazi Kuna wapiga kura hewa wametajwa.

Pili huu Upinzani kugawana kura bila kujiunga naona kabisa Upinzani unapoteza muda,
Upinzani kujiunga ni kuua demokrasia.Daftari la wapiga kura limejaa kura hewa.Kwa mfumo ulivyo inahitaji kazi ya muda mrefu kuhakiki taarifa zote hasa kwa kuzingatia kwamba uandikishaji wapiga kura umeongezeka kutokana na issue ya nationa id na cheti cha kuzaliwa.
 
Matunda ya Miaka 43 ya Utawala wa CCM Maradhi, Ujinga na Umaskini wa kutupwa. Walau wakati wa TANU hawajamaa walikuwa wanakondeana... tangu CCM ifanye Azimio la Zanzibar 1992, kasi ya unono na ukibonge inaongezea maradufu!
 
Mkuu Uzi wako unafikirisha sana, Hapa ilitakiwa kuhakikiwa kwa hao wapiga kura kwanza, Maana Ni wazi Kuna wapiga kura hewa wametajwa.

Pili huu Upinzani kugawana kura bila kujiunga naona kabisa Upinzani unapoteza muda,

Hao wapiga kura hewa ndio wataleta mgogoro Cha msingi hizo zihesabike kura zilizo haribika... Maridhiano yafanyike mapema.

Bila hivyo uchaguzi utaharibika.
Mpiga kura hewa atawezaje kumchagua diwani, mbunge na rais... Madiwani na wabunge lazma wataenda mahakamni kudai haki zao.
 
Hizo takwimu umezitoa wapi?
2015 kulikuwa na wapiga kura zaidi ya milioni 20.
 
Kupotosha kwako kutasaidia watu kujua ukweli! Ahsante! Nikuulize kaswali kadogo, unakumbuka Magufuli alitajwa kuwa mshindi kwa kura ngapi? Lowassa je? Na wengine kwa pamoja walipata ngapi? Jumla ya kura zote ngapi?
 
2015 walijiandikisha watu milioni 20 wakapiga kura milioni 15, kuongezeka watu milioni 9 ndani ya miaka mi5 sio ajabu.
 
Back
Top Bottom