Hebu tuambie, Google history yako ina kipi cha kipekee

Number ni 26

JF-Expert Member
Apr 3, 2019
1,478
2,836
Wakuu kwema,

Niende kwenye mada. Ni usiku mnene nikiwa sina hata lepe la usingizi nikiwa natafakari mambo mawili matatu tunayopitia wana wa Adam.

Sasa kama binadamu na mmiliki wa Dunia kijiji "smartphone" pale tunapotafakari kuhusiana na jambo, kitu au maisha kiujumla, wengi wetu huwa tuna kawaida ya kucheki na "msuluhishi Google" kujua kasemaje kuhusu kile kinachokutatiza kwa wakati huo.

Kwahiyo nikasema hebu leo niangalie kwenye google history ni kitu gani kime take over kwenye maisha yangu. Katika kupitia pitia mambo/vitu nilivyovitafuta most of the time, nikajikuta napata huzuni tu na kusema kwakweli bado nina safari ndefu kwenye hii Dunia.

Hebu tuambie "Google history" yako huko ina sound vipi?

NB: Huwa sina kawaida ya ku clear history sababu najiamini kwa ninavyovitafuta.
 
Mara nyingi ni Jf ndio imejaaa... na nina clear kila muda napojisikia, yaweza kuwa mara 2/3+ kwa siku.

Pia uwa nagoogle kila kinachonitatiza
Hata jicho likicheza, ni shwaaaa niko kwa anko google kuuliza sababu.

Hata niwe busy/ naumwa.. google history haiwezi maliza masaa 24 haijawa cleared..sina nachoficha 👋 nadhani tu ni mazoea.
 
Wakuu kwema,

Niende kwenye mada. Ni usiku mnene nikiwa sina hata lepe la usingizi nikiwa natafakari mambo mawili matatu tunayopitia wana wa Adam.

Sasa kama binadamu na mmiliki wa Dunia kijiji "smartphone" pale tunapotafakari kuhusiana na jambo, kitu au maisha kiujumla, wengi wetu huwa tuna kawaida ya kucheki na "msuluhishi Google" kujua kasemaje kuhusu kile kinachokutatiza kwa wakati huo.

Kwahiyo nikasema hebu leo niangalie kwenye google history ni kitu gani kime take over kwenye maisha yangu. Katika kupitia pitia mambo/vitu nilivyovitafuta most of the time, nikajikuta napata huzuni tu na kusema kwakweli bado nina safari ndefu kwenye hii Dunia.

Hebu tuambie "Google history" yako huko ina sound vipi?

NB: Huwa sina kawaida ya ku clear history sababu najiamini kwa ninavyovitafuta.
Hautojibiwa watu wote wameenda op pia hata wewe umeenda op hujaandika google history yako ina nini mf. Dawa ya kuleta usingizi kwa sababu wewe unakosa usingizi ( insomnia).
 
Google history doesn't guarantee your innocence since there is INCOGNITO TAB which leaves no history of pages you visited.
By the way, my Google history has list of jamii forums, Quora, LiveScore and betting sites.
 
Mimi google ni mshikaji wangu sana na ananisaidia kwenye mambo mengi, lakini siku hzi nimekuwa busy na Chatgpt4, huyu ndo suluhisho kwasasa

Ila Google bado namuheshimu sana.
 
  1. Tamisemi and Necta histories (necta.go.tz/brn) nilikua natafuta vitabu vya uchambuzi mara kwa mara Tamisemi.go.tz nafuatilia post za form fivekwa ukaribu
  2. excel formulas
  3. vlookup formula in excel
  4. homophones, homonyms, homograph and synonyms differents
  5. robo tatu ya notification ni taarifa za mtandao wa Jf
 
Mara nyingi hua na search zile site zetu pendwa sema kwa kua google ni msiri wangu kwenye history hua sizikuti hizo search lakini nikisearch kitu kingine labda aina ya simu nazikuta hizo history
 
Ukiingia kwenye history yangu utakutana na
gsmarena.com
Notebookcheck.net
Nanoreview.net
yts.mx
IMDb.com
Netnaija.com
goojara.to
NKIRI.com
xiaomiui.net
na website mbalimbali zinazoreview simu na movies, website nyingine hata sijazikariri majina
 
Quora inaongoza aisee

Nikitaka ku google jambo basi mbele yake naongeza neno quora ili inipe matokeo kutoka forum hiyo

Quora kuna watu wana nondo JF akasome
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom