fazaa
JF-Expert Member
- May 20, 2009
- 2,984
- 1,026
Kabisa kabisa....Kama hujui kujipenda huwezi kumpenda mwingine!
Kabisa kabisa....Kama hujui kujipenda huwezi kumpenda mwingine!
Tangu tumezaliwa tumesikia neno UPENDO,mimi binafsi wazazi wala shule sikuwahi kuambiwa maana ya hili neno!Nilikuja kulitafuta mwenyewe!Nakumbuka kwenye mafundisho ya dini tulikua tunaambiwa tupendane,nyumbani hivyohivyo.Nilipokua nikajua kuna kumpenda mwanamke,hawa walionieleza kuhusu upendo hawakuwahi kunifafanulia,nikajiuliza kuna tofauti kati ya kumpenda mama yangu na jirani yangu pia vipi kuhusu mwanamke?Nilibaki mtupu!Lakini niliamua kutafuta maana na nimepata tafsiri hii;Upendo ni kumkubali mtu bila masharti.Yaani kama ni mwanao sio mpaka afaulu mtihani ndo apendwe,kama ni jirani rio mpaka awe na pesa ndo apendwe,upendo ni kutoa tu bila kujali unaempenda anakurudishia nini,yaani wewe ni kutoa tu,na ukiwa hivi hautaona shida kuishi na mke/mume mkorofi.ANGALIZO,kwenye ndoa ni hatari kuishi na mtu mwenye tabia za hatari kama kupiga,kufuja,kudhalilisha n.k,hapa unatakiwa usitishe haya mahusiano,kufanya hivi haimaanishi unamchukia.Unaweza ukatengana nae lakini mkawa pamoja kwenye mambo mengine.Sasa kama niko sahihi,kuna upendo siku hizi?Na kama siko sahihi,tafsiri yako ni muhimu hapa,tuambie......
Poa! Nilikusudia yote mawili, iwe katika uhusiano wa kimapenzi na/au uhusiano wa kirafiki na kifamilia. Lakini tuangale kwenye ndoa ambako umekuzungumzia zaidi na hapa ninanukuu maelezo yako ya awali: [kwenye ndoa ni hatari kuishi na mtu mwenye tabia za hatari kama kupiga, kufuja,kudhalilisha]. Hayo mawili ya mwanzo mara nyingi huwafika akina dada na mama zetu na hilo la kati anaweza kuwa yeyote.MAMMAMIA,habari yako?......Unaposema mwenye tabia chafu hapendeki nadhani unamaanisha tabia ya kwenye uhusiano...Naomba utofautishe kati ya kutompenda mtu na KUAMUA kutokuishi na mwenye tabia chafu,kutokuishi na mwenye tabia chafu haina maana unamchukia ila ni hatari kuishi nae kama mwandani wako kwani atakuumiza kihisia na kukujengea mazingira ya kupata Ukimwi,na haya yote yatakusababishia kifo lakini mtu huyu huyu mnaweza mkashiriki kwenye mambo mengine ya maisha.Kama unapenda na kutegemea kurejeshewa upendo hujui kupenda kwa mujibu wa tafsiri yangu,upendo wako tayari una masharti.Kwanza fahamu kuwa unatakiwa umpende kila mwanadamu bila kujali kama na wao wanakupend.Kwenye ndoa/mahusiano ya mapenzi kuna baadhi ya tabia unatakiwa uziangalie kwa usalama wako coz huyu mtakua nae karibu sana na mtashare karibu kila kitu!Kuchukua tahadhari hii haina maana unamchukia,masharti wanayokua nayo wasiojua upendo[kwa tafsiri yangu]ni wale ili uwe rafiki au mpenzi wao ni lazima uwe na sura flani,fedha,mrefu,mweupe n.k,mambo ambayo hayana mashiko!