Hebu soma hapa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hebu soma hapa!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eiyer, Dec 29, 2011.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Tangu tumezaliwa tumesikia neno UPENDO,mimi binafsi wazazi wala shule sikuwahi kuambiwa maana ya hili neno!Nilikuja kulitafuta mwenyewe!Nakumbuka kwenye mafundisho ya dini tulikua tunaambiwa tupendane,nyumbani hivyohivyo.Nilipokua nikajua kuna kumpenda mwanamke,hawa walionieleza kuhusu upendo hawakuwahi kunifafanulia,nikajiuliza kuna tofauti kati ya kumpenda mama yangu na jirani yangu pia vipi kuhusu mwanamke?Nilibaki mtupu!Lakini niliamua kutafuta maana na nimepata tafsiri hii;Upendo ni kumkubali mtu bila masharti.Yaani kama ni mwanao sio mpaka afaulu mtihani ndo apendwe,kama ni jirani rio mpaka awe na pesa ndo apendwe,upendo ni kutoa tu bila kujali unaempenda anakurudishia nini,yaani wewe ni kutoa tu,na ukiwa hivi hautaona shida kuishi na mke/mume mkorofi.ANGALIZO,kwenye ndoa ni hatari kuishi na mtu mwenye tabia za hatari kama kupiga,kufuja,kudhalilisha n.k,hapa unatakiwa usitishe haya mahusiano,kufanya hivi haimaanishi unamchukia.Unaweza ukatengana nae lakini mkawa pamoja kwenye mambo mengine.Sasa kama niko sahihi,kuna upendo siku hizi?Na kama siko sahihi,tafsiri yako ni muhimu hapa,tuambie......
   
 2. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Upendo upo sana siku hizi tena bwerere
  wewe tu na roho yako.
  OTIS
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Upo kwa tafsiri ipi?Yako au yangu?
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ahsante mwalimu, kwa darasa hili maridhawa la Upendo............... Sina cha kuongeza, umemaliza mkuu
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Anazungumzia ule upendo wa, "I love you honey"
  Au ulikuwa haujamuelewa?
   
 6. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Thanx Mtambuzi!Inaonekana tafsiri zetu zinafanana,je upo huo upendo now days?
   
 7. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #7
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Upendo... Daima huja na huwa ni wa kweli na hauna mpaka.... Dini wala jamii haisemi kua mpende mtu ambae atakufurahisha tu. Hakuna kitu ambacho ni kugumu kufuata katika maisha kama kua na upendo consistent.... Upendo huwepo haijalishi huyo mtu ni mbaya, ana tabia za ovyo ama ana roho mbaya. Kuweza pass all that na ukampenda bado, ndio Upendo hasa wa kweli na ambao hasa kila mwanadamu anatakiwa kua nayo... However because we are human roho zetu zimeumbwa kwa nyama, upendo mara nyingi hujegwa na matendo ya umpendae..... Waweza mpenda mtu, awe mume, mzazi, mtoto ama mwanadamu yoyote yule, ila in the long run upendo ukashuka na kupungua juu ya huyo mwanadamu bila kutarajia.... wala bila kupenda.
   
 8. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Hahahaaa,Mtambuzi kumbe OTIS anazungumzia ule wa kwenye tamthilia za Kifilipino na Latin Amerikaeee!"I Love u more than myself"wizi mtupu!
   
 9. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mkuu,hebu tazama vyema utaona upendo ulivyo nje nje hata kuununua unaweza.
  OTIS
   
 10. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Dada Asha,u hali gani?,.....Upendo halisi haushuki wala hauishi,unaoisha ni ule upendo wa "kutegemea something in return"it means kwamba kama hujanifanyia hiki au kile sitakupenda,huu ni upendo wa masharti,na pia sio upendo!Tena hali hii kwenye uhusiano ndo kubwa,kiukweli hii ni mihemko ambayo hukujia baada ya mtu kukutendea jambo fulani au mtu kuwa na mtazamo/muonekano fulani[makalio,miguu ya bia,sauti,mrefu,mtanashati n.k]mihemko inayotokana na hali hizi huisha pale unapokinai kilichokuvuta au kinapotoweka!Upendo hauna masharti haya,haujali kama unarudisha matusi,au chuchu saa sita zimelala baada ya kunyonywa na mtoto.Mwenye upendo anaangalia ubinadamu tu.
   
 11. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Kama ni huu wa kununua,upo umejaa mpaka unamwagikia!
   
 12. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  mmh this z so true, uko njema leo eiyer naona toka uko juu unamwaga mapoint 2 duh.
  congratzz.
   
 13. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #13
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,649
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  mkuu habari ya masiku? Vp sikukuu?
   
 14. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #14
  Dec 29, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Upendo ni kujipenda wewe tu hakuna kingine-mimi sijawahi kuona mtu anampenda mtu mwingine zaidi yake.
   
 15. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #15
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Obsesd,WAKORAAAAAAAAAA!
   
 16. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Nzuri mkuu,sikuku ilikua njema ila tulipika pilau akaja kibaka akapita na sufuria lote ikabidi tupike UGALI!Si unajua nyumba zetu za uswazi jiko ni nje ya chumba chako...Lol!
   
 17. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #17
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Kama hujui kujipenda huwezi kumpenda mwingine!
   
 18. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #18
  Dec 29, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Good stuff, Eiyer
   
 19. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #19
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Thankx MJ1,heri ya mwaka mpyaa!
   
 20. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #20
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kama tutaangalia kwenye dondoo hizi mbili, kuna mambo yanachanganya - kumpenda mtu bila masharti na upendo wa kutegemmea something in return". Nahisi tusijidanganye, mwenye tabia chafu hapendeki (kama zilizotajwa hapo juu kwenye ndoa, au kwa rafiki mwongo, virungu, mbea, mchonganishi n.k, au mtoto mwizi, mwivu, mlevi n.k.) Anayependa katika mahusiano yoyote, iwe baina ya wapenzi, rafiki au familia, hutegemea kurejeshewa upendo, ikiwa atachokuwa anavuna ni maudhi na maumivu upendo hupungua na pengine huisha kabisa.
  Sumu ya upendo/mapenzi ni maudhi.
   
Loading...