Mr. Politician
Member
- May 16, 2008
- 74
- 7
Toka mwanzo nilikua naamini tofauti na ulivyokuwa unaamini wewe na nilifikiri labda nikipata taarifa za ndani (serikalini) ningeweza kuja kuelimisha na wewe uamini tofauti na unavyoamini wewe. Lakini....................
Kama kuna mtu anaweza kuja namaelezo kwa nn serikali inatetea hivi kuwa amekufa eti sababu balozi ameona jeneza nitamsikiliza kwa makini ili nirudi katika msimamo wangu kuwa Ballali amefariki kweli
BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imejisafisha na kusema kuwa haijui ni lini aliyekuwa Gavana wa BoT said:Nimwamini nani sasa???????? Aaaaaaaah
Wanashirikiana au wananyanyshwa?
hivi watanzania mlioko states hakuna hata mwenye picha ya mazishi? humu jf hakuna ndugu wa balali angalau atuthibitishie tumwache ndugu yao apumzike kwa amani?
kama balali hakufa, jambo hili ni nzito mno, na kwa kuwa MUNGU YUKO, MAAJABU YATATOKEA NA AKIIBUKA DOLA LA MAFISADI LITAKUWA NDO MLINAFUNGA PAZIA, YAANI MOVE IMEISHA
kama balali amekufa kwa mkono wa binadamu yaani kuficha ukweli ili watu waendelee kutesa na pesa za maskini watanzania, basi damu yake itawalilia mafisadi kokote waliko, watalaaniwa kwa dham,bi ya kaini na abel
Mr. Politician
Hapo ndipo kuna kizaazaaa nguo kuchanika, tangu nimezaliwa inakuwa mara ya kwanza kusikia kihoja kama hiki, nyumbani kwa marehu kuwekewa ulinzi!!!! Daaaa, kwenye msiba ni mahali panapohitaji mkusanyiko wa watu ili kuweza kuhani msiba huo, sasa kwa Dr. Balali mambo si hivyo,
Hivi hasa hasa Hao walinzi walikuwa wanalinda nini? Serikali ilikuwa inajihami na nini juu ya hilo? Hatuwezi kujua lakini!
Wanajamii hebu tulijadilini hili.
Toka amefariki Dkt Daudi Ballali kumekuwa na mijadala mbalimbali kwenye vyombo mbalimbali vya habari, wanasiasa na hapa JF ambapo kuna post nyingi sana. Lakini pia kabla ya hapo pia kulikuwa na mijadala ya mahali alipokuwa anauguziwa hadi kufikia wengine kuanza kusema ameshafariki hata kabla ya familia yake kusema. Lakini katika yote hayo serikali ilikaa kimya kwa muda mrefu kabla ya kuja na taarifa moja kuwa haijui alipo na haimuhitaji ila ikimhitaji itamtafuta na kumpata.
Baada ya kufuatilia mijadala ya muda mrefu na kupima uzito (maana hamna hata mmoja aliyeleta ushahidi) nilijiridhisha mwenyewe ya kuwa Ballali amefariki kifo cha kawaida yaani bila mkono wa mtu.
Ila sasa baada ya kusikia taarifa za viongozi wa serikali yetu ( Waziri Simba, Membe na Mkurugenzi wa mawasiliano ikulu bwana Salva) naanza kuamini tofauti huku maswali yakianza kugonga tena kichwani mwangu.
Huyu bwana amefutwa kazi kwa sababu ya upotevu wa mabilioni ya pesa za walalahoi kama ikigundulika ameiba atakabiliwa na kesi ya kujibu, sasa serikali haiogopi mtu ambaye Mh Rais amekosa imani naye akatudanganya amekufa kwa kuishirkisha familia yake katika hili?
Au basi kama si yeye kutudanganya kwa kushirikiana na familia yake basi serikali na yenyewe inahusika katika kupanga kifo chake maana haiwezekani mtu ambaye ulikua hujui alipo leo ukiambiwa amekufa na kuonyeshwa jeneza unakubali bila hata kuuliza na kuja kuwalazimisha wengine waamini.
Au sasa serikali inataka niamini maneno ya baadhi ya watu kuwa yenyewe inahusika katika kifo chake?
Bado nataka kuendelea kuamini kuwa serikali yangu ni makini na wala haijahusika katika kifo cha Ballali hebu kama kuna mtu anaweza kunisaidia nikaamini tofauti na ninavyoanza kuamini baada ya kumsikiliza Salva.