Hayati Mwl. Mzee kaiwanga wa shule ya msingi (vidudu) Tabata Kimanga 1996 A.D

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
37,907
43,821
Kuna kitu ambacho kimekuwa kinaniumiza kichwa kwa miaka mingi sana kuhusu huyu babu na mbinu alizokuwa akitumia kufundisha watoto wadogo kusoma na kuandika, ambayo nahisi kuna kama 'kauchawi' kalikuwa kanatumika.

Ilikuwa ni mwaka 1996 ambapo kaka yangu niliekuwa nasoma nae chekechea katika nursery moja hivi ya kanisa alipelekwa darasa la kwanza, lakini kwa upande wangu, nahisi kut
okana na kuwa na umri mdogo sana nilitoka kapa kabisa bila kujua kusoma, kiandika wala kuhesabu (completely).

Mzee wangu akaamua kwamba nirudie tena vidudu katika shule ya chekechea ya hapo Tabata Kimanga,ambapo nilikutanishwa uso kwa uso na huyo babu mwl. Mzee Kaiwanga. Nakumbuka vizuri sana, ilikuwa ni siku ya nne tu darasani ambapo nilikuwa nimekalia jiwe langu karibu kabisa na ubao, msaidizi wa kike wa Kaiwanga alikuwa anaandika sentensi flani ubaoni, na ofcourse nilikuwa sielewi kinachoandikwa maana nilikuwa sijajua kusoma wa kiandika, LAKINI ghafla bin vuu, kuna kama upepo ulinipiga usoni, na nilipofumbua macho niliweza kusoma na kuelewa alichokuwa anaandika huyo mama msaidizi. Kwa vile nilikuwa mdogo sana, nilisahau kuhusu huo mshtuko na kuona kama ni kawaida tu. Yaani ni kama mtu asiejua kiChina akijue ghafla!

Kesho yake niliweza hata kuandika na kufanya hisabati za kumjulisha na kutoa, from nowhere!, ilibidi niwe najikosesha maswali mengine ya hesabu ile nyumbani wasishtuke sana, hasa mama alikuwa haamini kabisa kinachotokea.

Leo nimeona niulize kama kuna mtu humu amewahi kusoma kwa huyo babu na kukutana na yaliyonikuta, maana hadi leo sina majibu kabisa!
 
Back
Top Bottom