Hayati Magufuli aliwahi kutishia kuchapisha noti mpya! Aliishia wapi?

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Dec 8, 2015
1,397
3,492
Enzi zile za utawala wa awamu ya 5 mambo yalinoga sana. Kila uchwao tungeweza kupigwa biti zito na jipya, kwa kifupi nchi ilikuwa ya moto kila siku, matamko ya kila namna.

Siku moja katika majukumu yake ya kawaida, hayati Magufuli akautangazia umma kupitia kwenye hotuba yake kuwa asingeshindwa kuchapisha noti mpya kwakuwa alipokea taarifa kuwa kuna majamaa walikuwa wameficha maburungutu kibao ya pesa na kufanya pesa isiwepo katika mzunguko.

Je, ni akina nani walificha pesa? Na kwanini mpango wake wa kuchapisha noti mpya haukutimia mpaka anaingia kaburini?
 
Hii issue hadi Nigeria ipo maana viongozi wengi wanaficha pesa hadi kwenye matundu ya vyoo
 
Back
Top Bottom