Hayati hata kabla hajazikwa?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,108
115,845
Kwa uelewa wangu Hayati ni baada ya kuzikwa...au nakosea?
Kabla hajazikwa anakuwa Marehem Hadi siku akizikwa..ndo jina Hayati linaanza
Au yote sawa?
 
Wanasema Hayati linatumika wakati wa kukumbuka enzi yake
Ina maana sio Sawa kutumia kabla hajazikwa

Kwa mujibu wa Omni Sigala ndivyo anavyoeleza mkuu. Anasema marehem inahusika zaidi na kumuombea dua/ rehema aliyefariki. Ni aghalam kutumia neno hayati kanisani, msikitini au makaburini. Kwa maana hiyo hayati itatumika pale inapokumbukwa mambo ya aliyefariki enzi za uhai wake. Hajaongelea kuhusu wadhifa, umashuhuri wala umaarufu wa aliyefariki.
 
Nijuavyo hayati ni jina analopewa mtu yoyote aliyefariki, haijadadavuliwa kama awe amezikwa au hajazikwa, kikubwa awe AMEFARIKI,


Marehemu na Hayati ni maana moja.
 
Nijuavyo hayati ni jina analopewa mtu yoyote aliyefariki, haijadadavuliwa kama awe amezikwa au hajazikwa, kikubwa awe AMEFARIKI,


Marehemu na Hayati ni maana moja.

Kuna tofauti ingia hiyo link juu
 
Back
Top Bottom