Hayati Dkt. Magufuli hakuisaidia Chato

Wilaya ya Chato iliyopo mkoani Geita ni Tanzania. Kwahivyo, itakuwa furaha ya kila mzalendo wa Tanzania kuona maendeleo ya Chato kama itakavyokuwa kwa maendeleo ya sehemu nyingine ya Tanzania.

Lakini maendeleo ni nini?

Aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli alijitanabaisha kama mtu anayependa maendeleo, lakini kuna uwezekano mkubwa hakujua tafsiri ya maendeleo. Pamoja na mambo mengine, Magufuli alitamani maendeleo ya nyumbani kwao Chato, na hivyo alifanya mengi huko nyumbani kwao, lakini pengine hakupasaidia inavyotakikana.

Magufuli alijenga uwanja wa ndege wa kutua ndege kubwa wilayani Chato, wakati kuna majiji (mfano Tanga), manispaa na miji mikubwa kuliko Chato ambako hakuna viwanja vya ndege vya maana au vilivyopo havina hadhi ya maeneo hayo. Kwanini Chato?

Hoteli ya Nyota Tano ilikwisha anza kujengwa Chato. Uwanja wa mpira wa miguu wa kisasa ulikuwa kwenye mpango wa kujengwa Chato. Alilazimisha CRDB wapeleke huduma wilayani Chato ingawa hakuna tija ya kibiashara. Na Jengo walilopangisha CRDB huko Chato ni jengo lake huyo Magufuli.

Je! Magufuli aliipenda Chato? Jibu ni Ndiyo. Na sio kosa kupenda kwenu, sio kosa kupenda maendeleo ya kwenu. Shida inakuja kwenye tafsiri ya maendeleo.

Magufuli angetambua maana ya maendeleo; Angeanza kuboresha elimu wilayani Chato kabla ya kujenga Hotel ya Nyota Tano. Moja kati ya wilaya zenye mazingira magumu kwa wanafunzi na walimu ni Wilaya ya Chato. Hoteli ya Nyota tano ya nini wakati wanafunzi wanamaliza darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika? Nani ataijenga Chato wakati idadi kubwa ya vijana hawapati elimu yenye tija katika dunia ya leo (Na hili ni kwa maeneo mengi ya Tanzania).

Kanda ya Ziwa kuna Ng'ombe wengi sana, lakini hawana afya. Pesa ya kujenga uwanja wa ndege ingetosha kutoa elimu kwa wafugaji juu ya namna ya kufuga kwa faida pamoja na kujenga viwanda vidogodogo vya kusindika Nyama na Maziwa ambavyo vingetoa ajira ya kudumu kwa vijana wa Chato. Wafanyabiashara wangemiminika Chato kutoka maeneo ya jirani kwa ajili ya biashara ya Nyama, na mazao ya maziwa. Kwanini mwenyeji wa Geita anunue maziwa ya Tanga Fresh, au Asas kutoka Iringa wakati kuna Ng'ombe wengi ndani ya kanda ya ziwa kuliko Iringa na Tanga kwa pamoja?

Kuna ardhi kubwa wilayani Chato. Magufuli angeweza kupeleka wataalamu wa kilimo kutoa mafunzo kwa vijana juu ya kilimo chenye tija ya kiuchumi na kibiashara. Wakulima wangelima kibiashara zaidi na kuvutia masoko kutoka mikoa jirani na nchi jirani. Watu wangemiminika Chato na kuchangamsha shughuli za maendeleo.

Kuna Ziwa Viktoria. Angeweza kuwekeza kwenye kilimo cha samaki (kuzalisha samaki ndani ya vitalu vya Ziwani) ambacho kingewanufaisha watanzania wanaoishi Chato. Ajira zingepatikana, wafanyabiashara kutoka mikoa jirani na hata nchi jirani za Rwanda, Burundi na DRC wangefika Chato kufungasha mizigo.

Angeweza kujenga Chuo Kikuu au hata matawi mawili matatu ya vyuo vikuu. Mji wa Iringa ni miongoni mwa miji iliyochangamshwa na uwepo vyuo vikuu. Chato ingechangamka pia.

Hayo yote yangewezekana kirahisi kutokana na nguvu aliyokuwa nayo kama Rais. Lakini nguvu ili iwe na tija sharti iambatane na akili.
Halafu yangefuata hayo ya kujenga uwanja wa ndege na mahoteli kwa kuwa sasa watu wenye uwezo wa kuvitumia (labda) wangekuwapo.

Lakini hawapo. Na sasa shirika la Ndege limesitisha safari za ndege Chato kwa sababu aliyekuwa anautumia uwanja wa ndege wa Chato hayupo. Nyasi zina tabia ya kuota hata juu ya zege. Baada ya muda kidogo ile hoteli ya nyota tano ambayo haijamalizika itabaki gofu. Uwanja wa mpira wa kisasa hautajengwa. Benki ya CRDB itaondoka kwa sababu wakazi wa Chato wanaoweka pesa benki ni walimu na watumishi wengine wa serikali - ambao wanatumia NMB. Majengo mazuri ya mahakama na vituo vya polisi hayawezi kuchochea maendeleo.

Kuna suala la Hospitali kubwa ya kanda iliyojengwa Chato. Huduma za afya ni suala zuri lakini jengo pekee halitoshi. Huduma zitakapoanza zitapaswa kufanana na jengo lenyewe. Hata hivyo haikuwa lazima kujenga hospitali kubwa Chato kabla ya kuboresha huduma za zahanati (Primary Health Care) vijijini. Hakuna maana ya kujenga hospitali kubwa eneo moja wakati zahanati katika vijiji mia au zaidi hazina ubora. Huduma za zahanati nyingi zikiwa bora, faida yake ni kubwa zaidi kuliko huduma ya hospitali kubwa moja. Kwahiyo, pamoja na hatua nzuri ya kujenga hospitali ile, naamini haikupaswa kuwa jambo la kwanza.

Magufuli hakuisaidia Chato kwasababu aliamini zaidi katika vitu (hardware) badala ya watu (Software). Angeanza kuwajenga watu kwa elimu na maarifa halafu akawajengea nyenzo za kuboresha elimu na maarifa yao; shule, vyuo, viwanda kwa ajili ya ajira, na mbinu zingine za kuvutia uwekezaji.

Lakini wapi! Aliwaza matokeo badala ya mchakato. Alichojenga Chato kitabaki kuwa makazi ya popo na mijusi kwa sababu hakuna wa kukitumia.

View attachment 1753858

Nawasilisha!

Dr Cyrilo
Big up Daktari Mada imeshiba! Tatizo kubwa la Mwendachato lilikua kutokujua mimi, ulimbukeni na ushamba wa kiwango cha kupindukia! Aliingia madarakani bila kuwa na "roadmap" kwamba anataka kufanya nini, matokeo yake akawa anaruka ruka na kufanya vitu kwa kukurupuka! Sasa kaiacha Chato kama Gbadolite kwa Mobutu, Mapango ya popo na chatu! Chato sifuri, imezimika kama mshumaa!
 
Andiko hili fupi ni bora na lina ujumbe na funzo kubwa mno kuliko thesis nyingi za PhD candidates.

Asante sana
 
Unajiita doctor ila unaandika vitu kama mtoto mdogo alievaa pampas ambae hajui la kufanya!Unasema Magufuli kupenda kwao siyo kosa,unaelewa kuwa Magufuli alikuwa ni Rais wa nchi na wala siyo mwananchi wa kawaida?

Unaelewa kuwa Rais wa nchi anatakiwa kupeleka miundombinu mahali kutokana na economic viability pamoja na economic strategic ya eneo husika na wala siyo kupeleka miundombinu eneo fulani kisa ni nyumbani kwao?

Unaelewa kuwa Rais kupeleka miundombinu eneo fulani kwa sababu tu ni nyumbani kwake hata kama hilo eneo siyo strategic economic area itachochea ukabila na ukanda?Kama kila rais atakomaa kupeleka miundombinu kwake,maeneo mengine ya Tanzania yatapewa maendeleo na nani?

Kama Rais atapeleka maendeleo eneo fulani kisa tu ni nyumbani kwake kama unavyodai,je yale maeneo ya kiuchumi ambayo huchangia pato la Taifa yatakuzwa na nani?Wewe ni doctor wa wapi unajenga hoja kama mtoto mdogo wa chekechea?
Najaribu kutafakari logic ya hiki ulichokiandika, siioni kwa kweli. Inawezekana una jambo zuri ulitaka kuliwasilisha, ila limeishia kichwani kwako. Naamini katika wasomaji wote wa andiko lako, asilimia kubwa sana hawajakuelewa
 
Kwa hiyo kutokuelewa wewe unasukumia kuwa na watu wengine hawajaelewa pia?
 
Wilaya ya Chato iliyopo mkoani Geita ni Tanzania. Kwahivyo, itakuwa furaha ya kila mzalendo wa Tanzania kuona maendeleo ya Chato kama itakavyokuwa kwa maendeleo ya sehemu nyingine ya Tanzania.

Lakini maendeleo ni nini?

Aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli alijitanabaisha kama mtu anayependa maendeleo, lakini kuna uwezekano mkubwa hakujua tafsiri ya maendeleo. Pamoja na mambo mengine, Magufuli alitamani maendeleo ya nyumbani kwao Chato, na hivyo alifanya mengi huko nyumbani kwao, lakini pengine hakupasaidia inavyotakikana.

Magufuli alijenga uwanja wa ndege wa kutua ndege kubwa wilayani Chato, wakati kuna majiji (mfano Tanga), manispaa na miji mikubwa kuliko Chato ambako hakuna viwanja vya ndege vya maana au vilivyopo havina hadhi ya maeneo hayo. Kwanini Chato?

Hoteli ya Nyota Tano ilikwisha anza kujengwa Chato. Uwanja wa mpira wa miguu wa kisasa ulikuwa kwenye mpango wa kujengwa Chato. Alilazimisha CRDB wapeleke huduma wilayani Chato ingawa hakuna tija ya kibiashara. Na Jengo walilopangisha CRDB huko Chato ni jengo lake huyo Magufuli.

Je! Magufuli aliipenda Chato? Jibu ni Ndiyo. Na sio kosa kupenda kwenu, sio kosa kupenda maendeleo ya kwenu. Shida inakuja kwenye tafsiri ya maendeleo.

Magufuli angetambua maana ya maendeleo; Angeanza kuboresha elimu wilayani Chato kabla ya kujenga Hotel ya Nyota Tano. Moja kati ya wilaya zenye mazingira magumu kwa wanafunzi na walimu ni Wilaya ya Chato. Hoteli ya Nyota tano ya nini wakati wanafunzi wanamaliza darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika? Nani ataijenga Chato wakati idadi kubwa ya vijana hawapati elimu yenye tija katika dunia ya leo (Na hili ni kwa maeneo mengi ya Tanzania).

Kanda ya Ziwa kuna Ng'ombe wengi sana, lakini hawana afya. Pesa ya kujenga uwanja wa ndege ingetosha kutoa elimu kwa wafugaji juu ya namna ya kufuga kwa faida pamoja na kujenga viwanda vidogodogo vya kusindika Nyama na Maziwa ambavyo vingetoa ajira ya kudumu kwa vijana wa Chato. Wafanyabiashara wangemiminika Chato kutoka maeneo ya jirani kwa ajili ya biashara ya Nyama, na mazao ya maziwa. Kwanini mwenyeji wa Geita anunue maziwa ya Tanga Fresh, au Asas kutoka Iringa wakati kuna Ng'ombe wengi ndani ya kanda ya ziwa kuliko Iringa na Tanga kwa pamoja?

Kuna ardhi kubwa wilayani Chato. Magufuli angeweza kupeleka wataalamu wa kilimo kutoa mafunzo kwa vijana juu ya kilimo chenye tija ya kiuchumi na kibiashara. Wakulima wangelima kibiashara zaidi na kuvutia masoko kutoka mikoa jirani na nchi jirani. Watu wangemiminika Chato na kuchangamsha shughuli za maendeleo.

Kuna Ziwa Viktoria. Angeweza kuwekeza kwenye kilimo cha samaki (kuzalisha samaki ndani ya vitalu vya Ziwani) ambacho kingewanufaisha watanzania wanaoishi Chato. Ajira zingepatikana, wafanyabiashara kutoka mikoa jirani na hata nchi jirani za Rwanda, Burundi na DRC wangefika Chato kufungasha mizigo.

Angeweza kujenga Chuo Kikuu au hata matawi mawili matatu ya vyuo vikuu. Mji wa Iringa ni miongoni mwa miji iliyochangamshwa na uwepo vyuo vikuu. Chato ingechangamka pia.

Hayo yote yangewezekana kirahisi kutokana na nguvu aliyokuwa nayo kama Rais. Lakini nguvu ili iwe na tija sharti iambatane na akili.
Halafu yangefuata hayo ya kujenga uwanja wa ndege na mahoteli kwa kuwa sasa watu wenye uwezo wa kuvitumia (labda) wangekuwapo.

Lakini hawapo. Na sasa shirika la Ndege limesitisha safari za ndege Chato kwa sababu aliyekuwa anautumia uwanja wa ndege wa Chato hayupo. Nyasi zina tabia ya kuota hata juu ya zege. Baada ya muda kidogo ile hoteli ya nyota tano ambayo haijamalizika itabaki gofu. Uwanja wa mpira wa kisasa hautajengwa. Benki ya CRDB itaondoka kwa sababu wakazi wa Chato wanaoweka pesa benki ni walimu na watumishi wengine wa serikali - ambao wanatumia NMB. Majengo mazuri ya mahakama na vituo vya polisi hayawezi kuchochea maendeleo.

Kuna suala la Hospitali kubwa ya kanda iliyojengwa Chato. Huduma za afya ni suala zuri lakini jengo pekee halitoshi. Huduma zitakapoanza zitapaswa kufanana na jengo lenyewe. Hata hivyo haikuwa lazima kujenga hospitali kubwa Chato kabla ya kuboresha huduma za zahanati (Primary Health Care) vijijini. Hakuna maana ya kujenga hospitali kubwa eneo moja wakati zahanati katika vijiji mia au zaidi hazina ubora. Huduma za zahanati nyingi zikiwa bora, faida yake ni kubwa zaidi kuliko huduma ya hospitali kubwa moja. Kwahiyo, pamoja na hatua nzuri ya kujenga hospitali ile, naamini haikupaswa kuwa jambo la kwanza.

Magufuli hakuisaidia Chato kwasababu aliamini zaidi katika vitu (hardware) badala ya watu (Software). Angeanza kuwajenga watu kwa elimu na maarifa halafu akawajengea nyenzo za kuboresha elimu na maarifa yao; shule, vyuo, viwanda kwa ajili ya ajira, na mbinu zingine za kuvutia uwekezaji.

Lakini wapi! Aliwaza matokeo badala ya mchakato. Alichojenga Chato kitabaki kuwa makazi ya popo na mijusi kwa sababu hakuna wa kukitumia.

View attachment 1753858

Nawasilisha!

Dr Cyrilo
Hivi huyo Mfugale alikuwa nani kwa Magufuli manake kila kitu kimepewa jina la mfugale na Magufuli, si afadhali angeita hilo jengo Mama Jannet!
 
Huyu ni sukuma gang bila shaka.

SAFI KABISA ndugu kwa uchambuzi uliyokamilika. AMEN
 
Na msimlaumu mwenda zake JPM, laumuni bunge la JMT. Bunge ndilo linalopitisha makadirio na matumizi ya serikali, na kupanga na kupitisha kifungu kwa kifungu matumizi ya wizara, idara, wakala, serikali za mitaa n.k. Matumizi yoyote nje ya taratibu za bunge ni kosa, na bunge linatakiwa kuchukua hatua kwa wahusika
 
Back
Top Bottom