Hayati Dkt. Magufuli aliletwa duniani mahsusi na Mungu ili kuleta masomo fulani tujifunze

kapangejr

Member
Jul 3, 2012
89
125
Katika kipindi cha JPM kuangalia hotuba ya raia ilikuwa raha sana...ni kama mechi ya simba na yanga.. Taifa linasimama kwa muda kumsikiliza...kwa machache mapungufu, mengi mazuri yalikuwa upande wa wengi..RIP magufuli
 
tutamkumbukamagu

JF-Expert Member
Jul 3, 2021
229
250
JPM alikuwa fundi sanaa hasa katika uongozi wake. Kwanza aliweza kuweka mambo wazi nyanja zotee.

1. Kimaendeleo hasa linapo kuja swalia za ripoti mbali mbali mfano.Madini kwakweli kupitia Mzee JPM nliweza kujua karibia kila kitu kilicho kuwa kinaendelea katika madini.
Lihali sasa naona giza tu hata taarifa za habari kutoka Channel na redio mbali mbali kukosa mvuto.

2. Aliweza kututia moyo sanaa hasa kwenye swala la kunitegemea na kutuamisha kuwa sisi ni matajiri basi hata kama ni uwongo basi sisi tulijihisi tunaweza na kila mtu alipata mhamko wa kuchapa kazi.JPM best of the Best.

3. Aliweza kukipa hadhi kiti cha uraisi na kueshimika kwa Jinsi alivyo jiweka na mdomaana mnaweza sema alijifanya Mungu mtu lakini kwakweli uraisi ulitua mahala sahihi.

4. Wale matajiri na wakwepa kodi mzee JPM alilala nao mbele mpaka wakakiona cha moto hadi wengine wamepotea kwenye ramani mpaka sasa wameshindwa kusimama tena.
5.Bila majungu nidham serikalini ilirudi kwa sehem kubwa tena sanaa.Si mahospitali nasehem zingine za kijamii.

6. Hakusafiri kwenda popote nje ya Bara la Africa na kulinda maslahi ya nchi yake kwa kuleta maendeleo kitu ambacho mabeberu walikonda sanaa.

Any way zipo zababu nyingi tuu nzuri na pia tunapaswa kujua Binadamu hatukosi kasoro katika maisha yetu ya kila siku.

ILA JPM MPAKA SASA KILA SEHEM HUKAI DAK KADHAA BILA KUTAMKWA JINA LAKE.

HAKIKA TUNA KAZI SANAA YA KUMSAHAU HASA KIZAZI HIKI CHA KWETU.
asanteeeeeeeeeeee
 
tutamkumbukamagu

JF-Expert Member
Jul 3, 2021
229
250
Ongeza na hili!
1. Aliwafanya wahitimu wa vyuo kama mazezeta wanarandaranda mijini bila ajira na kuwadanganya ajira zipo kumbe anaaajiri waliokwisha ajiliwa eti ni ajira mpya. Refer kwa zile alira elfu 13 zq ualimu ambazo kiuhalisia waliajiliwa walikuwa elfu moja halafu magazeti yote yakasema epfu 13 kwa lazima.

2. Mauaji kila kona mpaka maiti zinaokotwa kwenye viroba coco beach

3. Uchumi kuendeshwa kiujanja ujanaja mpaka akafikia hatua ya kidanganya ulimwengu kuwa uchumi unakua kwa asilimia 7 wakati ni asilimia 4 mpaka repory ya imf ikafichwa.

4. Udictator ukatamalaki sana mpaka siasa za upinzani zikazimwa kibabe eti hawastahili kuishi bali kuuuawa refer kwa tundu lisu
zikipigwa kura, umeshindwa!!!!
 
Nyaru-sare

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
3,847
2,000
Yesu alikufa kifo cha fedheha lakini hakuwa na dhambi. Kwahiyo kifo siyo kigezo cha kwamba mtu hayuko na Mungu.
Mkuu Dunia ya leo! una danganywa na kale, kakijana ka yesu kenu kazungu? katapeli! (white chapel,) ''white jesus will never come ma dear! ''. mtasubiri sana! mwana wa Mungu hafi kijinga wewe, unashindwa kujijibu swali rahisi hivo.

Ok! alikufa ajili ya nini?? dhambi zenu siyo!! , km alikufa kiudhalili ajili ya dhambi zenu! kwa nini na wewe ufe?, tena premature death! ndo huyo mungu wenu mzungu aliwaambia? hata siku ukijua mshahara wa dhambi ni nini?,,,,,, utatulia tuli!

Kama haitoshi dogo ni hivi Manabii wamepiga kelele miaka dahari kuwa ''ukiishi kwa upanga .........majibu unayo!! lkn ukitenda haki utakufa umeshiba umri tele!

hivi kabisaa mwana wa Mungu apate kichapo cha mbwa mwizi vile? acha utani bana wee!! sasa km hujui kile kipigo kilikuwa cha yuda Msaliti....... kujinyonga ilikuwa zuga tu! ila kibinadamu utaona hivyo!

kwani si Yesu alijua kuwa juda atamsaliti? unadhani kwa nini hakumsaidia mwanafunzi wake mpendwa na mtunza fedha? ili aepuke hiyo fedheha?
 
Bad Man Tivu

JF-Expert Member
Jan 16, 2019
272
500

Mwenyezi Mungu ninakuamini,ninakuabudu na ninakutukuza na nawaombea msamaha wale wote wasiokuamini,wasiokuabudu na wasiokutukuza..AMEN
 
Nyaru-sare

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
3,847
2,000
Umeandika kishabiki mno sisi masikini wa kitanzania hayo yote hayatuhusu

Kinachotuhusu ni yale maji yaliyoimbwa miaka buku hususani vijijini leo hii na Mimi kijijini kwangu nayafungulia tu kama mjini

Nguzo zilipita kijijini kwetu miaka 20 iliyopita lakini hatukuwahi kuwa na umeme

Hospital tulifunga safari zaidi ya km 200 kufuata huduma sasa naamka asubuhi cha kwanza kukiona ni hospital ya wilaya iko kijijini kwangu

Barabara inayopita kijijini kwangu ilikuwa na mabwawa ya kuvulia samaki leo ni mkeka mpaka amerika

Ni nini hasa nihitaji toka kwa kiongozi zaidi ya maswala ya msingi kama haya

Hawa wasomi ndo chanzo cha maafa kwa taifa hili wakifeli kwenye plans zao wanakimbilia saisa uchwala

Watanzania tumechoka tunahitaji kuyaona mapinduzi ya vitendo na sio polojo za kisiasa

Polojo za kisiasa hazimsaidii mwananchi wa kawaida
Siyo kishabiki Mkuu!! hongera kwa kuletewa maji!! ila sisi kijini kwetu tulikataa kuletewa maji na sirikali mpaka kesho, bali tulifanya kwa hela yetu wenyewe na nguvu zetu wnyewe, tukitumia mikokoteni ya ng;ombe kujenga barabara . mpaka leo ikipata mashimo tuna ziba wenyewe kwa kweli iko vizuri!

Umeme tulitumia kufua kwa Dynamor za baiskeli lkn baadae tuka nunua kubwa vijana wetu walileta tulio wasomesha kwa hela za kijiji, yaani mpaka leo mlikuwa hamjui kutumia umeme? mna akili au mmesha kufa?
 
togetherTight

Member
May 21, 2017
94
125
Ongezea na

1. Miradi ya tija kwenye jamii, zamani ilikuwa ni ndoto kuona lami uswahilini lkn wkt wa JPM tumeona.

2. Umeme, zamani tuliamini umeme hauwezi kuwa wa uhakika nchini kwetu kwani ni maskini nchi hii so tukawa tunaona umeme kukatika katika ni haki yake lkn baada ya JPM kuchukua madaraka umeme kukatika ikawa historia.

3. Miradi mikubwa ya historia, zamani viongozi wetu walishindwa kufanya miradi mikubwa wakisema kuwa nchi yetu ni maskini haiwezi kufanya miradi inayofanyika nchi zilizoendelea lkn wkt wa JPM tuliona ikifanyika mfano electrical SGR, ujenzi wa moja kati ya mabwawa makubwa kabisa ya umeme Africa na duniani JNHPP, flyovers na interchanges, Airports, Ports, ununuzi wa ndege kubwa, ujenzi wa meli kubwa kubwa, masoko n.k kiasi cha kwamba leo hii imeshakuwa fashion kwamba ili ukubalike na jamii lazima ufanye kama alivyokuwa anafanya JPM.

4. Thamani ya mwananchi, zamani mwananchi hasa wa hali duni alikuwa hathaminiki kabisa lkn baada ya JPM vyombo vya dola, wabunge na watumishi serikalini wakaijua thamani halisi ya mtanzania bila kujali ni tajiri au maskini.

5. Heshima ya Tanzania na Watanzania, zamani nchi yetu ilidharaulika sn hasa na nchi jirani, lkn miaka michache baada ya JPM nchi ikapanda thamani na kuwa mfano hapa Afrika kwa utekelezaji wa uchumi jumuishi (inclusive economy)

6. Shamba la bibi, zamani kabla ya JPM nchi yetu ilikuwa shamba la bibi lkn baada ya JPM kila mtu anajua kilichotokea.

7. Msimamo, JPM alikuwa kielelezo cha msimamo wa waafrika mbele ya wazungu kwamba tuna haki ya kupanga mambo yetu pasipo kuingiliwa na mtu yeyote.

Kuna mengi ya kumuelezea Magufuli ambapo kama nitaamua kuyaweka humu itakuwa ni kitabu, hivyo basi itoshe tu kusema kwamba JPM alikuwa moja kati ya viongozi bora zaidi kuwahi kutokea katika nchi hii japo kama mwanadamu hakukosa kasoro lkn kiukweli kabisa kasoro zake haziwezi kuficha mema mengi aliyoifanyia nchi hii.
Duh! umeupiga mwiiiingii..👌
 
kichomiz

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
17,859
2,000
Mungu Kuna watu anawatumia hapaduniani Kama shule kwa umma wake ili uongoke au ujifunze Jambo fulani magufuli ni mmoja wao.

Somo la kwanza
Ndugu pataneni mnapogombana maana mkishindwa mnampa nafasi adui kuneemeka na ugomvi wenu.Mtifuano wa kina lowasa ndani ya ccm ndio uliompa JPM kula kwamba wote tukose.

Somo la pili
Usimtegemee binadamu mwenzako Bali mungu tu. Kuna watu walimtegemea JPM kuliko mungu wakasahau JPM ni mwanadamu tu Sasa katwaliwa kawaacha wanahanyahanya. Rejea polepole makonda bashiru msiba na sabaya nk.

Somo la tatu
Hakuna aijuae kesho yake Bali Mungu tu. Ccm walifikia mahali wakataka JPM atawale milele aongezewe muda atakeasitake. Mungu kumbe ndie aliejua ukomo wa siku zake. Rejea Sanga na mbunge wa kongwa aliekuwa mtangazaji wa radio.

Somo la nne
Watu wasikulalamikie Sana kwa matendo yako vilio vyao vinasikika kwa muumba wao. Utawala wa JPM uliliza wengi kila Kona ya nchi na kila kundi liliguswa vilio vinasikika mbinguni.

Somo la tano
Usijiamini kupita kiasi. JPM alikuwa na over confidence kitu ambacho kilimfanya ajisahau hivyo akajikuta anaharibu mambo mengi pengine kwa kutokujua.

Somo la sita
Umuhimu wa katiba mpya. Sidhani Kama CCM wenyewe wangependa atokee mtu Aina ya magufuli Tena katika chama Chao. Hilo ni funzo na utawala wa magufuli umewafanya watu waone umuhimu wa katiba mpya na demokrasia.

Somo la Saba
Tii Sheria na uifwate hata Kama itakubidi kuwajibika kwa kukataa maagizo mabovu ya wakubwa wako. Sabaya alipokuwa DC alifanya maufiri mengi na mpaka akaiambia mahakama kwamba alikuwa anatii maagizo toka juu Sasa Leo amebaki peke yake na maufiri yake aliyemtegemea kumlinda hayupo.

Ongezea masomo mengine uliyojifunza kwa hayati Magufuli.
SoMo la nane
Usielekeze nguvu zako zote kwenye ulinzi wa nje,
Wakati ulinzi wa ndani haueleweki
 
Ame

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
4,227
2,000
Rejea sababu zilizopelekea kudai na kupigania Uhuru wa Tanganyika zilikuwa ni zipi?

Maendeleo ya vitu hata Mkoloni angeweza kuleta zaidi ya tulipo!
Mbona hao wakoloni hawakuyafanya basi hayo maendeleo?
 
Weakman

Senior Member
Jul 23, 2021
162
250
Mungu Kuna watu anawatumia hapaduniani Kama shule kwa umma wake ili uongoke au ujifunze Jambo fulani magufuli ni mmoja wao.

Somo la kwanza
Ndugu pataneni mnapogombana maana mkishindwa mnampa nafasi adui kuneemeka na ugomvi wenu.Mtifuano wa kina lowasa ndani ya ccm ndio uliompa JPM kula kwamba wote tukose.

Somo la pili
Usimtegemee binadamu mwenzako Bali mungu tu. Kuna watu walimtegemea JPM kuliko mungu wakasahau JPM ni mwanadamu tu Sasa katwaliwa kawaacha wanahanyahanya. Rejea polepole makonda bashiru msiba na sabaya nk.

Somo la tatu
Hakuna aijuae kesho yake Bali Mungu tu. Ccm walifikia mahali wakataka JPM atawale milele aongezewe muda atakeasitake. Mungu kumbe ndie aliejua ukomo wa siku zake. Rejea Sanga na mbunge wa kongwa aliekuwa mtangazaji wa radio.

Somo la nne
Watu wasikulalamikie Sana kwa matendo yako vilio vyao vinasikika kwa muumba wao. Utawala wa JPM uliliza wengi kila Kona ya nchi na kila kundi liliguswa vilio vinasikika mbinguni.

Somo la tano
Usijiamini kupita kiasi. JPM alikuwa na over confidence kitu ambacho kilimfanya ajisahau hivyo akajikuta anaharibu mambo mengi pengine kwa kutokujua.

Somo la sita
Umuhimu wa katiba mpya. Sidhani Kama CCM wenyewe wangependa atokee mtu Aina ya magufuli Tena katika chama Chao. Hilo ni funzo na utawala wa magufuli umewafanya watu waone umuhimu wa katiba mpya na demokrasia.

Somo la Saba
Tii Sheria na uifwate hata Kama itakubidi kuwajibika kwa kukataa maagizo mabovu ya wakubwa wako. Sabaya alipokuwa DC alifanya maufiri mengi na mpaka akaiambia mahakama kwamba alikuwa anatii maagizo toka juu Sasa Leo amebaki peke yake na maufiri yake aliyemtegemea kumlinda hayupo.

Ongezea masomo mengine uliyojifunza kwa hayati Magufuli.
Yote uliyoandika yametokea na kufanywa na viongozi mbalimbali duniani, ni MUNGU wako pekee mwenye upumbavu wa kumtumia JPM kufundisha uyasemayo, wakati si mapya hapa duniani we

Sisi tunayeamini ktk MUNGU mwema tunajua MUNGU amemtumia JPM kufundisha uzalendo wa kweli na uongozi wa kutetea wanyonge
Siku zote MUNGU yupo upande wa wanyonge
 
Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
4,702
2,000
JPM alikuwa fundi sanaa hasa katika uongozi wake. Kwanza aliweza kuweka mambo wazi nyanja zotee.

1. Kimaendeleo hasa linapo kuja swalia za ripoti mbali mbali mfano.Madini kwakweli kupitia Mzee JPM nliweza kujua karibia kila kitu kilicho kuwa kinaendelea katika madini.
Lihali sasa naona giza tu hata taarifa za habari kutoka Channel na redio mbali mbali kukosa mvuto.

2. Aliweza kututia moyo sanaa hasa kwenye swala la kunitegemea na kutuamisha kuwa sisi ni matajiri basi hata kama ni uwongo basi sisi tulijihisi tunaweza na kila mtu alipata mhamko wa kuchapa kazi.JPM best of the Best.

3. Aliweza kukipa hadhi kiti cha uraisi na kueshimika kwa Jinsi alivyo jiweka na mdomaana mnaweza sema alijifanya Mungu mtu lakini kwakweli uraisi ulitua mahala sahihi.

4. Wale matajiri na wakwepa kodi mzee JPM alilala nao mbele mpaka wakakiona cha moto hadi wengine wamepotea kwenye ramani mpaka sasa wameshindwa kusimama tena.
5.Bila majungu nidham serikalini ilirudi kwa sehem kubwa tena sanaa.Si mahospitali nasehem zingine za kijamii.

6. Hakusafiri kwenda popote nje ya Bara la Africa na kulinda maslahi ya nchi yake kwa kuleta maendeleo kitu ambacho mabeberu walikonda sanaa.

Any way zipo zababu nyingi tuu nzuri na pia tunapaswa kujua Binadamu hatukosi kasoro katika maisha yetu ya kila siku.

ILA JPM MPAKA SASA KILA SEHEM HUKAI DAK KADHAA BILA KUTAMKWA JINA LAKE.

HAKIKA TUNA KAZI SANAA YA KUMSAHAU HASA KIZAZI HIKI CHA KWETU.
Sifa za kijinga! Ukiona unazo au unazitoa fahamu tu kuwa wewe ni mjinga!
 
Jp Omuga

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
4,702
2,000
Ongezea na

1. Miradi ya tija kwenye jamii, zamani ilikuwa ni ndoto kuona lami uswahilini lkn wkt wa JPM tumeona.

2. Umeme, zamani tuliamini umeme hauwezi kuwa wa uhakika nchini kwetu kwani ni maskini nchi hii so tukawa tunaona umeme kukatika katika ni haki yake lkn baada ya JPM kuchukua madaraka umeme kukatika ikawa historia.

3. Miradi mikubwa ya historia, zamani viongozi wetu walishindwa kufanya miradi mikubwa wakisema kuwa nchi yetu ni maskini haiwezi kufanya miradi inayofanyika nchi zilizoendelea lkn wkt wa JPM tuliona ikifanyika mfano electrical SGR, ujenzi wa moja kati ya mabwawa makubwa kabisa ya umeme Africa na duniani JNHPP, flyovers na interchanges, Airports, Ports, ununuzi wa ndege kubwa, ujenzi wa meli kubwa kubwa, masoko n.k kiasi cha kwamba leo hii imeshakuwa fashion kwamba ili ukubalike na jamii lazima ufanye kama alivyokuwa anafanya JPM.

4. Thamani ya mwananchi, zamani mwananchi hasa wa hali duni alikuwa hathaminiki kabisa lkn baada ya JPM vyombo vya dola, wabunge na watumishi serikalini wakaijua thamani halisi ya mtanzania bila kujali ni tajiri au maskini.

5. Heshima ya Tanzania na Watanzania, zamani nchi yetu ilidharaulika sn hasa na nchi jirani, lkn miaka michache baada ya JPM nchi ikapanda thamani na kuwa mfano hapa Afrika kwa utekelezaji wa uchumi jumuishi (inclusive economy)

6. Shamba la bibi, zamani kabla ya JPM nchi yetu ilikuwa shamba la bibi lkn baada ya JPM kila mtu anajua kilichotokea.

7. Msimamo, JPM alikuwa kielelezo cha msimamo wa waafrika mbele ya wazungu kwamba tuna haki ya kupanga mambo yetu pasipo kuingiliwa na mtu yeyote.

8. Kujitambua, JPM amefanya watanzania wazijue haki zao kwamba hii nchi ni yetu sote na sio ya kikundi fulani fulani cha watu, na kwamba watanzania wanapaswa kutumikiwa na viongozi wanaowachagua.

9. Pesa ni za wananchi, JPM amefanya Watz wajue miradi inayofanyika ni pesa zao wananchi na kwamba inapaswa kufanyika na kuisha ndani ya muda muafaka, lkn pia miradi inayofanyika inapaswa kuwa bora na kuakisi thamani ya pesa (value for money).

10. Uchapakazi, JPM amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuambukiza uchapakazi wake kwa Watz, leo hii Watz wanafanya kazi bila kuchagua, iwe ni kuajiriwa au kujiajiri, tunaona Watz wengi sasa wamekuwa wakifanya biashara ndogondogo na kubwa si wanawake wala wanaume wala c vijana, kila mtu yuko bize kutafuta maisha yake kwa njia halali mpk imekuwa kero huko mijini hakupitiki, hii yote ni kwasababu raia waliipokea vyema kauli mbiu ya HAPA KAZI TU.

Kuna mengi ya kumuelezea Magufuli ambapo kama nitaamua kuyaweka humu itakuwa ni kitabu, hivyo basi itoshe tu kusema kwamba JPM alikuwa moja kati ya viongozi bora zaidi kuwahi kutokea katika nchi hii japo kama mwanadamu hakukosa kasoro lkn kiukweli kabisa kasoro zake haziwezi kuficha mema mengi aliyoifanyia nchi hii.
Hizo siyo sifa... Huo ni ujinga wa baadhi ya wananchi kujidhania kuwa wao ni wanyonge... Na yupo mmoja pekee ambaye atawapambania! Sifa za kijinga hizi kutoka kwa wajinga kwenda kwa wajinga!
Tunahitaji mind liberations!
Tunahitaji stronger organizations.
Hatuhitaji stronger people!
People come and go!
Strong institutions will stay to be improved!
#Shame!
 
Plsm

Senior Member
Aug 19, 2021
178
500
Ongeza na hili!
1. Aliwafanya wahitimu wa vyuo kama mazezeta wanarandaranda mijini bila ajira na kuwadanganya ajira zipo kumbe anaaajiri waliokwisha ajiliwa eti ni ajira mpya. Refer kwa zile alira elfu 13 zq ualimu ambazo kiuhalisia waliajiliwa walikuwa elfu moja halafu magazeti yote yakasema epfu 13 kwa lazima.

2. Mauaji kila kona mpaka maiti zinaokotwa kwenye viroba coco beach

3. Uchumi kuendeshwa kiujanja ujanaja mpaka akafikia hatua ya kidanganya ulimwengu kuwa uchumi unakua kwa asilimia 7 wakati ni asilimia 4 mpaka repory ya imf ikafichwa.

4. Udictator ukatamalaki sana mpaka siasa za upinzani zikazimwa kibabe eti hawastahili kuishi bali kuuuawa refer kwa tundu lisu
Ilikuwakuwaje wewe hukuuliwa ili hali kila kona kulitapakaa mauwaji yake??

Hao wanafunzi wa vyou kwa sasa wameondokana na khali hiyo?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom