Mkuu umenena vyema... Haya tuanzie pale tulipoishia kwenye Mabomu ya Arusha!!!
TAMKO HILI LINAMHUSU PIA MWIGULU NCHEMBA
YAH. Kinachozaniwa ni bomu kutupwa kwanye mkutano wa CHADEMA kiwanja cha Soweto tarehe 15 June saa 11.30 jioni.
Sisi watanzania tunaoishi Israel tumekaa na kutafakali kwa kina tumefikia uamuzi wa kukionyeshea kidole C hama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kuwa ndivyo vimehusika kwa namna moja au ingine katika tukio la kutupa kinachozaniwa kuwa ni bomu katika mkutano wa mahisimu wao CHADEMA uliofanyika katika viwanja vya Soweto mjini Arusha mnamo tarehe 15 June 2013 saa 11.30 jioni.
Tunakituhumu Chama cha Mapinduzi na serikali yake hasa
POLICE kuwa kimehusika kwa sababu zifuatazo:-
1.Kwa akili za kawaida tu mtu hawazi kujitupia bunda la nyuki mwilini mwake ili zimuume, ila atataka amtupie hasimu wake nyuki hizo zimuume ili amcheke, hivyo basi CHADEMA hawawezi kufanya njama za kutupa bomu katika mkutano wao wenyewe ni lazima njama hizo zimefanywa na adui wao Mwingine ambae sisi tunadhani ni CCM ikisaidiwa na serikali yake kwa maana jeshi la polisi
2. Si mala ya kwanza CCM kufanya njama zinazofanana na hizi ambazo baadae zinapelekea uchaguzi kuahirishwa, tumerejea uchaguzi mkuu mwaka 1995 ambapo baada ya CCM kukabwa sana na NCCR katika mkoa wa Dar-es-salaam uchaguzi uliahirishwa sehemu ile tu. Ilikuwa hivi upepo ulivyokuwa unaenda wakati wa kampeni ulionyesha kuwa CCM itapoteza kwa upinzani majimbo yote 5 ya mkoa wa Dar-es-sallam hivyo CCM na tume yake ya uchaguzi viliamua kuahirisha uchaguzi mkoani humo kwa kisingizio eti sehemu nyingi karatasi za uchaguzi hazikufika, fikiria siku hiyo kulikuwa na karatasi za kupigia kura kijijini Nyamgali wilaya ya Kasulu mkoa wa Kigoma umbali wa km 900 eti karatasi zishindwe kufika manzese km 3 toka makao makuu ya tume pale garden avenue, zile zilikuwa ni njama ambazo zilisaidia kuokoa majimbo ya Dar, maana baada ya uchaguzi na matokeo kutangazwa sehemu nyingine wakazi wa Dar walikata tamaa basi uchaguzi wa marudio wapinzani wakapata jimbo la Ubungo peke yake.
3. Tumeshangazwa sana na kitu kinachoitwa complete impunity anacho enjoy huyu mtu anaeitwa Mwigulu Mchemba kada wa CCM na tumeambiwa ni naibu katibu mkuu ccm Tanzania bara. He is operating with complete impunity, where does that aura of impunity coming from? ma wise men tumejiuliza, amekuwa kama astrologer, akisema mambo kweli yanatokea alisema CHADEMA imepanga kuuwa watu akaonyesha ile kanda ya Lwakatare, juzi wakati wanahitimisha kampeni Arusha alisema wanainchi msihudhulie mikutano ya CHADEMA mtakufa na kweli watu wamekufa, halafu wala hakamatwi wala kuhojiwa . Hii inatutia mashaka sana ndio maana tuionyeshea kidole CCM.
4. Jeshi la polisi ni kama vile halipo au limelala usingizi au saa ingine linasaidia mission kufanikiwa. Jeshi hilo ni la Serikali iliyoundwa na chama tawala cha CCM, fikiria lile tukio la bomu hapo Arusha kwenye ufunguzi wa kanisa, jeshi la polisi lilikamata watu feki feki tu, juzi wakati watu wanamkimbiza Yule aliyedhaniwa katupa bomu polisi wakaharibu mission kwa kutupa mabomu ya machozi na risasi za moto ili watu watahaluki na kupoteza lengo, na mpaka sasa tunaambiwa hamna mtu aliyekamatwa zaidi ya kuahirisha uchaguzi ili watu wakate tamaa wasije kupiga kura ile tarehe iliyopangwa wapige kura CCM peke yao maana hii mission ni ya kwao.
5. Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Magesa Mlongo ni kiongozi wa serikali hapaswi kuwa na upande katika uchaguzi huu lakini yupo mstari wa mbele kuwapasia mapande CCM ili waweze shinda hata kata moja anatumia sana polisi yuko radhi hata kuwaweka ndani wabunge wote wa CHADEMA walioko Arusha, kwa hiyo hata angejua njama za kutupa bomu asingeweza zuia .
6. Grunate lenyewe gololi zake zimeonekana kama bomu lilitengenezwa China na silaha yenye kuwa na gololi kama hizo humilikiwa na serikali sasa kwa hali hii kwa nini tusiionyeshee kidole CCM na serikali yake?
HITIMISHO.
CCM inapaswa wajue kwamba mwisho wao umefika na hawawezi kutawala watu kwa nguvu, wawaachie wanainchi wachague viongozi wanaowataka, hakuna hali ya kudumu kila kitu kinamwisho wake, no situation is permanent, mwisho wa CCM umefika kama Roman empire ilivyofika mwisho, waswahili walisema mlimbua inchi ni mwanainchi mwenyewe, atakaeanzisha machafuko inchi hiyo ya Tanzania ni CCM wenyewe kwa upuuzi huo wanaoufanya, tunaomba wakubali hali.
Leo hii 17 June 2013 mjini Tel.Aviv ni Sisi:-
Ebaeban –mwenyekiti
Samson Wanzogo-Katibu
Abdalah Chinjocha –Mjumbe
Juma Bidiga-mjumbe
CC, Ikulu, jeshi la polisi, Mwigulu Nmchemba, Mbowe na wenzie Zitto Kabwe, Tundu Lissu etc, TISS.