Haya ya Vicky, Catherine na Jacqueline, kuna ya kujifunza ila tunapotezea

Eli Cohen

JF-Expert Member
Jun 19, 2023
1,311
4,019
Kitu kimoja ambacho mimi huamini ni kuwa mara nyingi mwanamke yoyote anaekubali kuwa mke wa pili au kuwa mke mpya baada ya ndoa ya kwanza kuvunjika, huwa ni MOTIVE ndio inayomshawishi kuingia kwa mwanaume huyo.

Hakika ndugu zangu, MOTIVE hio mara nyingi unakuta mali nyingi au pension ya uzeeni.

Ndio maana hawa wanaume wakishafariki unakuta hawa wanawake kitu kinachozunguka kichwani mwao huwa ni mali, mali, mali.

Tusidanganyane eti huwa wanafata upendo wa kweli baada ya penzi la kwanza kuvunjika, no, hakuna mwanamke atakubali kuwa mke wa pili au kuwa mke mpya wako kama unapanda dala dala kila siku.

Catherine magige, Vicky Kamata na Jacqueline ni miongoni ya vithibitisho ni jinsi gani unavyoweza kuharibu mstakabali wa familia yako unapoleta mwanamke mwingine maishani mwako for the sake of sijui umemchoka mkeo, sijui mkeo anazingua, etc.

Kumbukeni hawa wanawake wanaokuja baada ya mke wa kwanza mara nyingi wanakuwa michepuko ya hawa wanaume, sasa kama imetokea kuvunjika kwa ndoa kubwa ndio utaona sasa baba anajifanya kumleta mwanamke huyo. So mwanamke anaekubali kuwa mchepuko wako asili yake ni uhuni. So tambua kuwa kinachofata ni mwanamke kufanya uhuni huko mbeleni.

KUWEKENI MAKINI WANAUME.


View: https://youtu.be/qFZayn7AXi4?si=hfD3-CKqZoo9PbJD


View: https://youtu.be/4q9vG_62a7Q?si=geDriZtEN07vQWk-


View: https://youtu.be/JfOtj22lDrQ?si=_d97-3S81u_ocTPy
 
Uko sawa kabisa mkuu.
Sema on a serious note, tutafute ukwasi wa kutosha. Mwanaume ukiwa loaded unakula pisi kali from ujanani mpka uzeeni e.g kina Mengi et. al.
Ukishadanja haujui kinachoendelea, we umepumzika kwa amani.
Sema tusisahau kuwawekea msingi watoto wetu ili at least wasiteseke wakabaki wanalaumu
 
Uko sawa kabisa mkuu.
Sema on a serious note, tutafute ukwasi wa kutosha. Mwanaume ukiwa loaded unakula pisi kali from ujanani mpka uzeeni e.g kina Mengi et. al.
Ukishadanja haujui kinachoendelea, we umepumzika kwa amani.
Sema tusisahau kuwawekea msingi watoto wetu ili at least wasiteseke wakabaki wanalaumu
Kabisa.

Mi nadhani ni bora uwe una gonga huko nje tu unatuliza munkali kuliko kuleta mwanamke mwingine maishani mwako kisa tu sijui mmefanyanaje na mke, sasa ukadhani utapumzikia hapo kumbe waleta bomb.
 
Kabisa.

Mi nadhani ni bora uwe una gonga huko nje tu unatuliza munkali kuliko kuleta mwanamke mwingine maishani mwako kisa tu sijui mmefanyanaje na mke, sasa ukadhani utapumzikia hapo kumbe waleta bomb.
Nadhani shida pia kwa watanzania wengi ni
1. Sheria zetu ziko kizamani haziendani na dunia ya sasa.
2. Asilimia kubwa hatujui sheria zinasemaje kuhusu masuala mbalimbali ndoa included.
Sidhani kama n kosa mtu kuamua kuoa tena baada ya kushindwana na mwenzake, shida ni pale ambapo wanashindwa kufuata sheria kukamilisha hilo. Mathalani kama kuwa na talaka halali, kuwa na wanasheria ambao utaonyesha kwao mgao wa mali zako pindi utakapokufa n.k.
Wenzetu wametuacha mbali kwa sababu pindi wanapokufa, mwanasheria wao hua anakuja na kusoma mgawanyo wote wa mali na kila mtu anapewa haki yake n.k

Ni wakato muafaka watu waliosomea sheria wajitahidi kuelekeza zaidi kuhusu sheria mbali mbali rather than kugombania elf 5 za kugonga muhuri
 
Badilisheni mentality. Hata mke wa kwanza asilimia kubwa huwa wanafuata ukwasi. KIMSINGI BORA UNGESISITIZA WANAUME TUTAFUTE PESA MUDA WOTE WA MAISHA YETU. Kitu kimoja usichojua ni kuwa hata mkeo wa kwanza sijui wa ujanani heshima na mapenzi huongezeka ukiwa na pesa

Turudi kwa uzi wako.

Kama Kuna cha kujifunza nadhani jamii ijifunze kuheshimu mawazo na maamuzi ya wanaume. Hii ya kujazana akili kuwa wake wa pili wanafata mali muanze kuyafuta. Kwann mtu akifa jamii inaingilia kati maamuzi yake, kama ni mabaya kwann msiyaingilie akiwa mzima? Nyie mnaongea hamjui wanaume wanapitia nini kwenye ndoa zao!!!

Kama binadamu wanume huwa wanahitaji Sana faraja na Amani ndani ya ndoa. Wanawake nao Kama binadamu huwa wanakengeuka wanaanza kuchukia waume zao, wanawapa wakati mgumu Sana! Sasa mwanaume anajitoa anapata mwanamke mwingine anampa faraja anampenda jamaa anajiweka mazima bahati mbaya akifa jamii mnarudi kumnyanyasa huyu mwanamke, ni makosa haya.

Hela zangu natafuta mwenyewe kwa jasho na damu nina haki kuamua nikifa achukue Nani fulstop

Watoto wengi huwa wanakuwa brainwashed na mama zao wanajenga bifu na baba zao wanamnyanyasa wanamtenga mzee anatafuta mwanamke mwingine anapewa Amani na upendo anapumzika siku akifa yanaibuka yote yanakimbilia mahakamani, ujinga kabisa

Mkiamua kuondoka na mama yenu mkamuacha mzee anahangaika wakati aliwapenda akawasomesha mkaingia ujinga wa ugomvi wa mama yenu basi jueni maisha yameisha hapo. Mwacheni mzee apambane na afe kivyake
 
Wanawake wengine wanaonewa tu

Pande zote mbili wote wana'Tamaa ya Pesa. Kila mtu atajitahidi kuvutia kwake.
#dont judge hamjui story nzima
 
Back
Top Bottom