Haya ya mwaluko B ni kiboko

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
nimeangalia kwenye taarifa ya habari ya tbc1 nimeona shule moja ya msingi ya mwaluko b mkoani shinyanga wanatumia darasa moja wanafunzi wa madarasa mawili mfano darasa la 6 na 7 wanachangia darasa moja kwa wakati mmoja yaani mwalimu wa darasa la 7 upande mmoja na mwalimu wa darasa la 6, huku wanafunzi wote wamekalia mawe na wakaonyesha choo inayotumiwa inasikitisha.. Kweli kikwete unaona tuendelee na mchakato wa kuwalipa dowans? Mbona huna huruma kwa wananchi wako, kweli mimi nayasubilia hayo maandamano ya tarehe 24 - 02 - 2011, cha kushangaza baada ya taarifa hiyo akaonyeshwa msekwa akijisifia eti mafanikio ya ccm.

Naomba tulijadili
 
Inatia machungu sana kwa kweli watanzania tuamke jamni mbona wenzetu Misri wameweza!!
 
mwenye shibe hamtambui mwenye njaa, wakati wao wanalipana mamilioni kwa kuuza sura hapo biafra wenzao wanateseka kwa kukaa juu ya mawe.
 
of course yote haya yanatokana na negligence na kupuuza mambo ,lack of self disciplines na kupata uongozi pasipo kutoka jasho ,so wot to do ni kutafuta means to show them that we are fed up and nw enough is enough.
 
hebu pata picha, umekalia jiwe daftari mapajani, hujala chochote tangu asubuhi mpaka saa 8 kwa halafu mwisho wa siku unalinganishwa na mwanafunzi anaesoma pale Tanganyika
 
This country bwana is very poor,,,


Umeona eeh?
Sasa hiyo Shule ni afadhali hata waandishi wameweza kufika huko, zingine zipo mahali hakufikiki.
Tanzania vijijini kunatisha kishenzi. Sasa viongozi wetu wakikaa Dar basi wanaona tumeendelea kweli, hasa kwa vile hata wakisafiri ama wanatumia ndege, au mabasi yanayopita kwenye lami, halafu wanaishia mijini, wakiona vijana wanawashangilia na wamebeba bendera basi wanaridhika, wanafikiria nchi iko poa. Wakiangalia magari yalivyo mengi mijini (ukweli sio mengi, ila barabara ndio chache) basi wanaona fresh tu, eti tumeendelea. Inasikitisha.

Jamani, Tanzania tunahitaji mikakati mipya kabisa ili kuondoa umasikini huko vijijini.
 
Kwa kweli hiyo ni moja kati ya maelfu ya shule za namna hiyo zilizojaa vijijini!!
 
hebu pata picha, umekalia jiwe daftari mapajani, hujala chochote tangu asubuhi mpaka saa 8 kwa halafu mwisho wa siku unalinganishwa na mwanafunzi anaesoma pale Tanganyika
 
Back
Top Bottom