Haya wakubwa huu ndo uaminifu!

Haya wakubwa huu ndo uaminifu!

popiexo

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Posts
742
Reaction score
184
KUAMINIANA!

95r1vh3vlg9m



Mke wa Frank anajivunia mume mtulivu, hashindi baa na hatongozi videmu.

Akitoka kazini huenda kucheza basketball na hurudi nyakati za dinner. Siku moja mkewe akamhurumia. Anachoka na kazi. Mtu gani asiyependa starehe japo kidogo?

Mke akamlazimisha outing, Frank akabisha lakini taxi ikafika. Gonga Club & Lodge.

Walipofika mlangoni tu, mlinzi akaita, “Mambo Frank!” “Poa”


“Nilidhani huwa huji club, inakuwaje mlinzi anakufahamu?”

mke akauliza
“Yule mgambo, mchana analinda ofisini kwetu, usiku anapiga part time hapa” akajibu Frank

Wakachagua meza. Kukaa tu tayari mhudumu ameshaleta castle lager.


Akamuuliza mama anakunywa nini. Mhudumu alipoondoka mama akauliza,
“amejuaje unakunywa castle kama hakufahamu?”

Wakati Frank anajikanyaga aanze vipi kujitetea, mhudumu wa vyumba akawa amefika na kuuliza.


“Mkuu kama kawaida nimekuandalia namba tano, nendeni tu vinywaji nitawaletea huko huko”

Kufikia hapo mama akawa hana simile tena, akanyanyuka akitukana kama chizi. Akatoka nje mbio na kuingia katika taxi iliyokuwepo pale.


Wakati anapatana bei na dereva, Frank naye akaingia. Mama
yakamporomoka matusi kibao na kilio juu. Alipovuta kamasi na kupiga kwikwi akamsikia dereve anasema.

“Duh, eee bwana Frank huyu malaya uliyeokota leo balaaaaaaaaaaaaaaa kuliko wa jana!!!!!!”

 
kila mara nimekuwa nikiwashangaa watu kuwaficha kwa wenzi wao katika baadhi ya mambo mfano kama mwanzo ulikuwa mnywaji basi sio kama ukishaoa unajifanya kutokunywa, watakiwa kuendelea kunywa hata kama wakwezo wapo wajue kama mkwe wao kumbe yuko hivi na si kujificha na mwisho wake ndiyo madhara kama yale kwa frank yaliyomkuta,kajificha weee mwisho kaumbuka.
 
Back
Top Bottom