Mkuu analysis yako ya kutumia ununuaji wa vocha wala si sahihi. voda bado customers kibao. kwanza kuna postpaid wanalipa kwa bill, makampuni kibao yapo kwenye mkataba. kuna vodajaza hawa wanalipiwa na makampuni yao kutokana na wadhifa wa mtu. mfano meneja anawekewa credit ya laki moja kwa mwezi, labda wafanyakazi wa ngazi nyingine kwa mwezi wanawekewa alfu 80 kwa mwezi na kampuni inailipa voda. kuna bundles mtu ananunua minutes labda minutes 300. mkuu dark city technolojia ya sasa si analogue, ishapitwa na wakati, vilevile kukwangua ma voucher nako kunapitwa na wakati, kwa mtindo huo kuna vodafasta mkuu, lengo la kampuni ni kuondokana na physical recharge na kubase zaidi na electronic recharge ndo maana ya vodafasta.kaka kuna mpesa. katika menu ya mpesa unaweza kununua credit kuingiza kwenye akaunti yako, ukamtumia mtu pesa, ukalipia dawasco na tanesco. atm recharge za nmb, nbc zote hizi unaingiza credit kwenye simu. sasa means zote hizi baba why bother scratching voucher? hawa hawa wenye vibanda ndo walikuwa wanaongeza bei za voucher? ya buku 5 utauziwa buku 5 na mia tano. kitu kingine jamani mfahamu voda hawategemei kupiga simu tu, kuna data pale subscribers kibao, kuna wimax pale sijui km mnaifahamu wadau kuna yale mabenki sijui yana atm zao zinaitwa umoja, connection yote pale ni wimax, very speed na bandwith yake ni ya kufa mtu, nbc, barclays km sijakosea na makampuni mengi tu yatakuja, yote hiyo ni wimax. just a tip mkataba wa bank moja kwa mwezi thamani yake yafikia milioni 500. haya kaeni chonjo soon mtaanza kulipwa mishahara yenu kupitia mpesa hiyo yaja, ni suala la marketing tu, wala msiogope technolojia hiyo mwajiri wako akikubali utakuwa kwenye karne mpya. subscriber base inaongezeka daily sababu ya mpesa, pita vodashops angalia ile misululu ya watu wanaochukua na kuweka mpesa, kuna jamaa alilalamika sana humu eti kachajiwa elfu saba kutoa pesa, hiyo ni option mazee, km unapanda ndege kwenda mwanza kwa laki 2 wakati kuna basi la elfu 50 sijui, ni uchaguzi wako tu. jaribuni kuangalia product and services kampuni inazo offer kuliko kuangalia voice peke yake. na hiyo tigo ni dar tu huko mikoani utalia na kusaga meno.