Miwatamu
JF-Expert Member
- Oct 2, 2012
- 1,450
- 490
Inanikera na leo imenikera zaidi hadi nasikia kukereketwa kooni! Jamani hapa ninapoishi kuna jirani ambaye ni baba mwenye familia ya mke na watoto wanne. Kati ya watoto hao mmoja wa kufikia ni wa kike ambaye amehitimu elimu ya msingi, na wa kiume yupo darasa la sita wakati hawa wengine wawili ni wadogo.
Huyu bwana akiwa nyumbani anafanya kazi zote kama mke/mdada wa kazi ikiwa ni pamoja na kupiga deki, kuosha vyombo, kupika, na kufua nguo zote hadi nguo za ndani za mke wake na matambala anayotumia akiwa katika siku zake (hii ni kweli kabisa) na mbaya zaidi kazi hizi huzifanyia nje kweupe kabisa na akina mama majirani wakiwa wanamwangalia ikiwa ni pamoja na hao watoto wake wote !! Sasa kitu ambacho kimeniudhi leo ni kuona anafua suruali na nguo zingine za huyo binti yake wakati yeye anacheza lede barabarani, binafsi najiuliza haya ndio mapenzi tunayostahili kuwaonesha/kuwafanyia watoto na wake zetu? Na Je, nitumie njia gani kumfikishia ujumbe kuwa anayofanya ni kujidhalilisha? Kwani imefika sasa watoto wanamuona kama mhudumu tu hapo nyumbani. Naombeni ushauri wemu kwani mwanakwetu anatutia aibu.