Haya ni mapenzi au huruma?

Hodi humu ndani
mie sio mwenyeji sana, ni mgeni kiasi
Nimekuja na shida yangu tafadhali naomba msaada wenu
Mie ni dada wa makamo, niko nje ya nchi kwa masomo.Tangu nifike hapa nimekuwa mtu wa kujiepusha sana na mambo ya mapenzi na kujitahidi kujikita zaidi kwenye masomo nisije nikakosa degree yangu na kurudi bongo kwa aibu au nikaamua kubaki huku kwa kukwepa aibu ya kushindwa.Namshukuru Mungu nimeweza kuruka viunzi vingi vya mapenzi.Well, tatizo limekuja siku za karibuni kukutana na kaka mmoja anayetokea moja ya nchi zilizo kusini mwa Afrika.mwanzoni alipoanza kunifuatilia kimapenzi nilisikia kichekesho kwa sababu kaka huyu macho kumchuzi,(makengeza) kwa hiyo nilikuwa nasikia kucheka kila mara anaposisitizia azma yake ya kuwa na mie.Cha ajabu jinsi siku zinavyokwenda naanza kumwonea huruma(sina hakika kama ni huruma au ni mapenzi)natamani kumwona mara kwa mara. asiponitakia goodnite najisikia vibaya.Akikaa siku nzima bila kunipigia nasononeka. In short mie nisipoona yale macho basi hujisikia vibaya mwenzenu na kila nikimuona kamoyom kangu kananidunda lakini najipa moyo kwamba ninachojihisi ni huruma sio mapenzi.sasa wadau ninawezaje kujua hasa nini kilicho moyoni mwangu.Weekend hii kaniofa twende movie lakini nasita mana sina uhakika na feelings zangu mwenyewe.ushauri tafadhali kabla sijachemka dada yenu.
nionee huruma mimi mtz mwenzako nami nipo nje ya nchi kwani wewe upo nchi gani?
 
nionee huruma mimi mtz mwenzako nami npo nje ya nchi kwaani wewe upo bara gani kama ni ulaya mimi ntakufata tuu wewe nipe full informations
 
usikubali kupoteza dhamira yako. Soma acha ujinga. Tatizo mitoto ya kike ndo maana walikuwa hawaisomeshi hapo awali. Mtoto kike chuoni anatakiwa aondoke na degree mbili; moja academic na mb.o.o

jamani, hayo kweli mambo.o!
 
Kula kitu roha inapenda, waswahili husema ukipenda chongo huita kengeza, na ukipenda kengeza (macho kumchuzi) valisha mawani.lol!
 
nami nipo nje nipe mm mtz mwenzako aniambie tuu yupo nchi gani kama ni hapa ulaya mm ntafunga safari
 
tutafutane hata mimi npo nje tuoniane huruma sisi wa tz niambia tu upo nchi gani kama ni hapa ulaya
 
Biblia imesema msinyimane, M/mke ampe m/mme haki yake na m/mme hvo hvo.., mmepewa bure toeni bure!!! so usimnyime kaka wa watu, endelea tu kumhurumia mwaya alafu mwisho wa siku uje tena hapa ukilia ukiomba ushauri
 
Biblia imesema msinyimane, M/mke ampe m/mme haki yake na m/mme hvo hvo.., mmepewa bure toeni bure!!! so usimnyime kaka wa watu, endelea tu kumhurumia mwaya alafu mwisho wa siku uje tena hapa ukilia ukiomba ushauri

Unajua for sure siwaelewi nyie watu nisimnyime nini ambacho nilikieleza kwenye shida yangu hapo mwanzo?
 
Asante mpendwa, na kadegree kenyewe sio ka kwanza ni ka pili na mkaka anapiga ka tatu

acheni uzinzi..kaa usome..umri huo unajiita dada wa makomo ndo maana huolewi kwa ajili ya kutest twat mara wa makengeza mara kiguru mara mwenye upara.aaagh...mitoto ya kike bana
 
Dada wewe ushapenda hapo hamna huruma wala nini! Usikilize moyo wako dia. Pia kuwa makini na masomo usijefeli jaribu kubalance mapenzi na masomo
 
Biblia imesema msinyimane, M/mke ampe m/mme haki yake na m/mme hvo hvo.., mmepewa bure toeni bure!!! so usimnyime kaka wa watu, endelea tu kumhurumia mwaya alafu mwisho wa siku uje tena hapa ukilia ukiomba ushauri

wacha kutumia maandiko vibaya. Imesema ...mpe MUME, sasa kwani huyo ni mme wake? Hata uchumba bado. Kidunia dunia, mwambie aende step2... BED INTERVIEW.
 
Usikubali kupoteza dhamira yako. Soma acha ujinga. Tatizo mitoto ya kike ndo maana walikuwa hawaisomeshi hapo awali. Mtoto kike chuoni anatakiwa aondoke na degree mbili; moja acad
emic na mb.o.o

acha ubaguzi wako wa kijinsia, wewe umeshatongoza wanawake wangapi lakini unajiona una haki kabisa kisa wewe ni mtoto wa kiume
 
job true true toa hiyo kitu halafu uone nduki zake na miafrika mingi ina familia kama unataka kua small house sawa endelea na huruma sawa mama..
 
Back
Top Bottom