GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,417
- 120,728
Katika safiri safiri zangu zote hasa kwa kutumia njia ya barabara kwa kupanda Mabasi kwenda Mikoani kwa muda mrefu sasa nimekuja kugundua kitu kuwa kumbe Watanzania ' ujanja ' wetu upo mdomoni tu lakini hakuna Watu ' waoga ' duniani kama Watanzania.
Ukipanda basi lolote la kwenda Mikoa ya Kaskazini au ile ya Magharibi mwa nchi kama Tanga, Kilimanjaro na Arusha kwa upande wa Kaskazini na ile ya Iringa, Mbeya, Rukwa, Ruvuma ni lazima tu mtapita haya maeneo mawili NYETI na MUHIMU ya Mto Wami na Milima ya Kitonga.
Kinachokuwa kinanishangaza siku zote ukisafiri tu na Mabasi haya utakuwa humo ndani ya Basi abiria wote tunapiga stori, kufurahi na kujiachia kwa aina zote za ' mikogo ' ila ikifika tu tunakaribia ama Wami au Kitonga utaanza kuona Sura zote za Abiria zinabadilika ghafla, hofu na uwoga ukianza kuwatawala usoni huku wale wenzangu na mie wakianza ' kutubu ' mapema dhambi zao na wengine kila mara tu kufanya ishara ya msalaba utadhani Pope Francis XVI kaingia kusalisha.
Na tukishavuka tu hayo maeneo tajwa mawili ya Wami na Kitonga utaona abiria wote wanaanza tena kuonyesha jeuri na viburi vyao ambavyo wakati mkiwa hayo maeneo walikuwa hawavionyeshi na hata wengine wakitaka kulia kwa uwoga.
Je ni kwanini karibia 99.9% ya Abiria wa Mabasi ya Mikoani wanaopita ama Wami au Kitonga huwa wanatia huruma na kuwa wapole sana wakiwa hayo maeneo? Je hii ina maana kuwa Watanzania ni waoga wa Kufa au tuna Ugonjwa fulani uliotuharibu Saikolojia zetu kutokana labda na historia ya hayo maeneo mawili tajwa?
Naomba kuwasilisha na karibuni katika ' utiririkaji ' Wakuu.