Haya ni mapendekezo ya Tume ya Francis Nyalali (1994)

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,932
987
20190830_183856.jpg
20190830_183607.jpg
20190830_183142.jpg
20190830_233200.jpg
20190830_233120.jpg
Maktaba zina utajiri mwingi ukiamua kufuatilia. Lakini pia unaweza kukutana na swala katika msitu wakati malengo yako yalikuwa kuwinda sungura. Hii nafikiri ndiyo sababu kuna watu hawakosi kwenda pale Maktaba Kuu maarufu kama Tanganyika Library.

Nikirudi katika mada, Tume ya ilikuwa inaratibu maoni ya wananchi kama tuelekee katika Mfumo wa Vyama Vingi au tubaki katika Mfumo wa Chama Kimoja cha Siasa waliandika mapendekezo kadhaa katika Taarifa yao. Tume hii ilijulikana kama Tume ya Jaji Francis Nyalali.

Naomba usome mapendekezo ya Tume halafu utafakari ikiwa ni zaidi ya miaka 20, je tupo kwenye njia sahihi?

Tume hiyo iliundwa na:
1. Jaji Mkuu Francis Nyalali - Mwenyekiti wa Tume
2. Ndg Abdulwahid M. Borafia - Naibu Mwenyekiti wa Tume
3. Julius Sepeku - Katibu wa Tume

Wajumbe toka Tanzania Bara
1. Tito M. Budodi
2. Balozi Dk. Wilbert K. Chagula
3. Hindu B. Lilla
4. Pius Msekwa
5. Juma Mwapachu
6. Balozi Tatu Nuru
7. Isidore L. Shirima
8. L. Nangwanda Sijaona
9. Dk. Kapepwa I. Tambila
10. Crispin Tungaraza

Wajumbe toka Tanzania Zanzibar
1. Wolfango Dourado
2. Ussi K. Haji
3. Pandu Ameir Kificho
4. Aboud Maalim
5. Omari O. Makungu
6. Prof. Haroub Othman
7. Salim Juma Othman
8. Zaina Khamis Rashid
9..Ali Juma Shamuhuna
10. Juma Khiari Simai
 
Attachments

  • Judge_Nyalalis_Report_on_40_Repressive_L (1).pdf
    5.9 MB · Views: 56
Mkuu jaribu kutuma kwa muonekano mzuri ili nasi wa Tecno tuweze soma, yaonekana ilikuwa na mambo mengi mazuri.
 
Tume ilifanya kazi kwa weledi na kwa misingi ya haki. Kilichotakiwa kufanyika ni kiongozi aliyekuwepo wakati huo kusimamia utekelezaji wa mapendekezo hayo.
 
Naikumbuka na baadhi ya wajumbe walitoa ripoti mbadala kwani hawakukubaliana ripoti yote. Miongoni mwa wajumbe waliotoa ripoti hiyo alikuwa ni ndugu Salum Juma Othman kutoka Zanzibar. Hili lilikuja baada ya pendekezo la kuundwa serikali tatu.
 
Tume ilipendekeza mfumo wa Serikali tatu. Hata tume ya Jaji Kisanga ilikuwa imependekeza mfumo wa Serikali tatu, Rais Mkapa akasema hoja hiyo haikuwamo katika Hadidu za rejea.

Naona hapo mahakama kuu ilipewa jukumu la kuhakikisha bunge halitungi sheria inayokiuka katiba sasa unashangaa inatungwa sheria na yanawekwa makosa yasitokua na dhamana wakati katika inatamka mtu yeyote anachukuliwa kama vile hana hatia hadi atakapothibitishwa na mahakama kwamba ana hatia.i.e uhujumu uchumi
 
Ndiyo
Tume ilipendekeza mfumo wa Serikali tatu. Hata tume ya Jaji Kisanga ilikuwa imependekeza mfumo wa Serikali tatu, Rais Mkapa akasema hoja hiyo haikuwamo katika Hadidu za rejea.
Ndiyo. Ni baada ya wale wajumbe kutoa ripoti mbadala.
 
Tume ilifanya kazi kwa weledi na kwa misingi ya haki. Kilichotakiwa kufanyika ni kiongozi aliyekuwepo wakati huo kusimamia utekelezaji wa mapendekezo hayo.
Kwa kuwa ni Mapendekezo ya Tume halali ya Rais, hata sasa twaweza kutekeleza ili Taifa lisonge mbele.
 
Mwingine anaweza kusema, mapendekezo ya Tume hayana maana. Akirejelwa Tume ya Nyalali, Jaji Kipenka na Tume ya Warioba.

Lakini hajaweza kutafakari, mbona Tume nyinhine mapendekezo yao yanazingatiwa?
 
Uongozi wetu na hatma ya Tanzania ; Nyerere aliiponda sana hii tume, alisema ripoti ilikuwa na taarifa za kupika.
 
Uongozi wetu na hatma ya Tanzania ; Nyerere aliiponda sana hii tume, alisema ripoti ilikuwa na taarifa za kupika.
Hayati Jaji Mkuu Francis Nyalali anakumbukwa na wengi kwa sababu ya ile tume yake ambayo ilipendekeza sheria 40 za kikandamizaji zifutwe.Hayo ya kumsingizia Mwalimu kuwa alipenda hizo sheria za kikandamizaji ziendelee ni AIBU kwako.
 
Uongozi wetu na hatma ya Tanzania ; Nyerere aliiponda sana hii tume, alisema ripoti ilikuwa na taarifa za kupika.
Tume ya Jaji Nyalali ilipendekeza mambo mengi, lakini yanayotuhusu hapa ni mawili:
(i) Pendekezo la kugeuza mfumo wa Chama Kimoja cha Siasa, na kuleta mfumo wa Vyama Vingi; na
(ii) Pendekezo la kugeuza mfumo wa Muungano wa Serikali Mbili, na kuleta mfumo wa Shirikisho la Serikali Tatu.

La kwanza lilikubaliwa na Chama na Serikali, na la pili likakatiliwa.

Hili suala la pili liliibuka tena wakati wa bunge la katiba la halikupatiwa ufumbuzi kwa maana ni suala tata.
 
Back
Top Bottom