Hapa ninapokaa nipo jirani kabisa na kanisa fulani ambalo kwa mida hii sasa ndo limezama kwenye maombi mazito ya kiroho. Hawa waumini wake wamejizatiti sawa sawa kuziangamiza nguvu za muovu shetani. Lakini sasa hali ni tofauti sana kwangu. Yaani hapa nilipo nawaza vitu vya ajabu ajabu tu visivyo na tija yoyote kabisa. Mbaya zaidi na masaa menyewe haya usiku unaelekea kutulizana sijuwi mwisho wake itakuwaje na masaa ya kuikimbilia siku mpya ya kesho yamebaki machache. Asubuhi yangu ya kesho inaweza isiwe nzuri