Haya ndiyo maajabu 7 ya dunia

WilsonKaisary

JF-Expert Member
Apr 4, 2017
392
946
Mara nyingi watu husikia mara kwa mara kuhusu maajabu 7 ya Dunia, ila wengi wao hawajui ni yapi. Basi tuwe pamoja katika kuyaelezea tupate kuyafahamu vizuri.. Maajabu hayo ni kama yafuatayo:

1: Piramidi za Giza (Misri ya Kale)
2: Mabustani ya Semiramis (Babeli)
3: Hekalu ya Artemis mjini Efeso (Asia Ndogo)
4: Sanamu ya Zeus mjini Olympia (Ugiriki ya Kale)
5: Kaburi la Mausolo mjini Halicarnasso (Uajemi)
6: Sanamu ya Kolossos kisiwani Rhodos (Ugiriki ya Kale)
7: Mnara wa Pharos ya Aleksandria (Misri)

AJABU LA 1: Piramidi za Giza (Misri ya Kale)

Piramidi za Giza ni kati ya majengo yanayojulikana zaidi duniani. Pamoja na mava mengine ni sehemu ya makaburi ya Giza yaliyokuwa mahali pa kuzika wafalme wa Misri na wakubwa wa milki yao kwa muda wa miaka 2500.
Ziko kando ya bonde la mto Nile, karibu na mji wa Giza takriban kilometa 15 kutoka Kairo, mji mkuu wa Misri.
Na Boaz Marco

AJABU LA 2: Mabustani ya Semiramis (Babeli)

AJABU LA 3: Hekalu ya Artemis mjini Efeso (Asia Ndogo)

Hekalu hilo lilihesabiwa kati ya maajabu saba za dunia. Lilijengwa mjini Efeso kwa muda wa miaka 120 kuanzia mwaka 560 KK. Mfalme Kroisos wa Lidia ndiye aliyeanzisha ujenzi huu. Hekalu lilikuwa na urefu wa mita 115 na upana wa mita 55. Nguzo zake zilisimama mita 18. Liliharibika mara kadhaa na kujengwa upya. Mwaka 262 BK liliharibiwa kabisa wakati wa uvamizi wa Wagodoni. Leo hii kuna nguzo moja tu inayoonekana.

AJABU LA 4: Sanamu ya Zeus mjini Olympia (Ugiriki ya Kale)

Sanamu ya Zeus mjini Olympia ilimwonyesha mungu mkuu wa dini ya Ugiriki ya Kale. Zeus aliaminiwa kuwa baba wa miungu wa Ugiriki. Sanamu yenye kimo cha mita 12 ilimwonyesha mungu huyu akikalia kitini kama mzee mwenye hekima. Ilikaa kwenye hekalu kubwa ya Zeus ya Olympia kando la uwanja wa michezo ya Olimpiki. Ilitengenezwa na mchongaji mashuhuru Phidias aliyejenga kiini cha ubao na chuma pamoja na jasi na kuifunika kwa ubao, dhahabu na pembe. Phidias aliifanyia kazi kwa miaka 8 kuanzia mwaka 438 KK. Baada ya kuimaliza Phidias alishtakiwa kuwa ameiba kiasi cha dhahabu iliyokusudiwa kwa sanamu akauawa.

Watu wa Kale walihesabu sanamu hii kati ya maajabu saba za dunia. Mwaka 40 BK Kaisari wa Roma Caligula alishindwa kupeleka sanamu kwenda mjini Roma. Lakini wakati wa karne ya 4 ilipelekwa Konstantinopoli ikasimamishwa pale hadi mwaka 475 ilipoharibiwa katika moto kubwa.

AJABU LA 5: Kaburi la Mausolo mjini Halicarnasso (Uajemi)

AJABU LA 6: Sanamu ya Kolossos kisiwani Rhodos (Ugiriki ya Kale)

Sanamu ya Kolossos kwenye kisiwa cha Rhodos ilikuwa kati ya maajabu saba ya dunia ya kale. Kolossos ilikuwa mnara wa taa mwenye umbo la sanamu ya mtu aliyesimama kwenye mlango wa bandari na kushika moto kama mwenge. Kazi ya sanamu ilikuwa kuelekeza meli bandarini wakati wa usiku. Sanamu ilimwonyesha mungu wa jua Helios.

Ilijengwa kwa muda wa miaka 12 ikakamilishwa mnamo 300 KK na kuwa na kimo cha zaidi ya mita 30. Ilikuwa sanamu kubwa kabisa ya dunia ya kale. Kumbukumbu zimehifadhiwa kuwa matumizi ya vifaa yalikuwa pamoja na tani 13 za bronzi na tani 8 za chuma zilizofunika nguzo za matofari na mawe zilizokuwa majenzi ya ndani.

Sanamu ilisimama miaka 60-70 tu ikaanguka wakati wa tetemeko la ardhi mnamo 226 KK. Ikakatika kwenye magoti. Mabaki yalikaa palepale kwa sababu watu wa Rhodos waliogopa hasira ya mungu Helios wakisimamisha kitu kilichoangushwa na miungu.

Kwa miaka karibu 900 watalii wa dunia ya kale walishangaa mabaki makubwa. Mwaka 654 Rhodos ilivamiwa na Waarabu Waislamu na Muawiya (wakati ule bado gavana wa Shamu bado khalifa) aliuza metali kwa mfanyabiashara. Inasemekana ya kwamba ngamia 900 walihitajika kubeba mzigo.

AJABU LA 7: Mnara wa Pharos ya Aleksandria (Misri)

Pharos ya Aleksandria ilikuwa mnara wa taa mjini Aleksandria ya Misri ikahesabiwa kati ya maajabu saba ya dunia. Kimo chake hakikujulikana kikamilifu lakini kilikuwa kati ya mita 110 na 150. Mnara huu ulijengwa kwenye kisiwa kidogo kilichoitwa "Pharos" kiliochokuwa mita chache mbele ya mwambao wa Aleksandria. Baadaye mnara uliitwa kwa jina la kisiwa.

Ujenzi ulitokea mnamo mwaka 282 KK. Kwa karne nyingi Pharos ilikuwa kati ya majengo marefu ya dunia. Iliporomoka baada ya matetemeko ya ardhi yaliyotokea Aleksandria 1303 na 1323.. 'Kumbuka hilo Jina alitoa Alexander the great wa ugiriki'

"la zianda ugiriki ni baba wa mataifa Duniani"

FB_IMG_1590905179525.jpg
 
Ushawahi kusikia the treasure Pit of the Oak Island? Yani ile construction ya ile pit n beyond human's understanding na haijulikani ni nani aliijenga
 
Hayo maajabu yalikuwa maajabu kwenye ulimwengu wa kale kwa ulimwengu wa sasa ulivyopiga hatua tunayaona kama ya kawaida.Katika maajabu yote hayo limebaki moja tu hilo la Pyramid mengine yameshindwa kusurvive kutokana na majanga ya asili
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom