Haya ndio maisha bora kwa kila Mtanzania!

johnmashilatu

JF-Expert Member
Sep 16, 2010
718
703
Miaka mitano iliyopita, wakati kama huu, wakazi wa kijiji cha Kigaga wilayani Kibondo mkoani Kigoma, kama wengine Tanznaia, waliahidiwa maisha bora kwa kila mdanganyika

leo miaka mitano baadaye, zahanati ya kijiji chao imefungwa kwa wiki mbili baada ya mhudumu pekee aliyepo, kuifunga kwa kuwa anakwenda kuhudhuria semina mjini Kigoma

Matokeo yake, wakazi wa kijiji hicho wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita tano kwenda vijiji jirani kufauta matibabu

badaye ya kutafutwa, mhudumu huyo Bi Merina January amesema anarejea wakati wowote kuanzia sasa kuendelea kutoa huduma

huduma zenyewe mtaalamu huyo pekee katika zahanati hiyo, anazitoa kwa kufuata ratiba. anassema "Jumatatu na Jumanne anatoa huduma za tiba kwa wagonjwa wa Jumla, Jumtano anatoa huduma kw aajili ya akina mama wajawazito wanaofika kwa mara ya kwanza, alhamisi chanjo kwa watoto, ijumaa kwa wajawazito, ...."

mhudumu huyo ambaye anafanya kazi zote kuanzia usafi hadi kazi nyingine yoyote ya kitabibu unayoweza kufikiria anaiomba halmashauri ya wilaya ya Kibondo kumwongezea ANGALAU mhudumu mwingine kwani nanye ANACHOKA

Nenda kapige kura na tafakari
 
Kupiga kura ni muhimu kwa mtu yeyote mwenye akili timamu mahala popote alipo hapa Tanzania ameishuhudia miaka mitano ya maisha bora kwa kila mtanzania. Hatusubiri mtume ili macho yafunguke tupate kuona! Kwa kuwa mafisadi macho yao yanaona lakini wanayanyima uhuru wa kuona wakati wako macho mchana kweupe, ipo siku watalazimishwa kutoona wakati wanataka kuona!

Wewe, mimi, yule na wale hakikisha unapiga kura ya ndiyo kwa viongozi makini na waadilifu wenye kujali utu wa watu kama Dr.Slaa.

Tukishirikiana tutaijenga tanzania katika misingi ya utu,
 
Matatizo ya namna hii hayapo Kibondo tu karibu Tanzania nzima matatizo yanafanana.
 
'm afraid. 'm shivering. I can't imagine another 5 horrible years with JK. Lord have mercy. The guy has to go!
 
Back
Top Bottom