Haya nakusanyo ya kuvuka lengo TRA wanaumiza importers

R Mbuna

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
2,283
5,361
Habari za wakati huu wakuu.

Hili swala la TRA kulazimisha kulipishana kodi sasa imekuwa kero kwa kweli. Mimi nina fanya shughuli za clearing & forwarding sasa kuna mteja wangu huwa anaagiza hizi safety equipment i.e viatu, life jacket nk.

Safari hii ameleta mzigo kama kawaida sasa imekuja issue ya kukagua maana tulishalipa ushuru kwa mara ya kwanza baada ya ukaguzi wa mzigo yaani physical inspection wanalazimisha ule mzigo kwenye declaration tumeweka wrong HS code .

HS code ambayo inakubalika world wide ni 6307:20:00 ambayo ina 0% kwenye import duty na description yake inaeleza exact with nature ya mzigo wa mteja. Lakini wao wanataka tutumie HS code 6307:90:00 which has 25% kwenye import duty ambayo kwenye description wameandika other.

Tunawaomba hawa ndugu zetu wakusanya kodi waangalie uhalisia wa bidhaa na hizo HS code ambazo wao wenyewe walizipendekeza. Sio kwa vile mkuu anapenda kodi basi mlazimishe tu kodi hata sehemu haihitajiki.

HS code huwa zinakubalika katika nchi nyingi tu kimataifa kwa mfano huu mzigo umefanyiwa preverification na SGS tangu port of loading na wakaweka hiyo HS code na ndio ambayo imetumika kwa mizigo yao yote tangu waanze biashara. Iweje leo without prior notice wanataka tubadilishe HS code?

Kodi ni wajibu wetu kulipa ila sio kuwekeana viwango ambavyo havipo kwa mujibi wa sheria stahiki.

R Mbuna
 
Back
Top Bottom