Haya mazoea ya kuanza kuanika vifo mitandaoni siyo kabisa

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,037
Imekuwa kawaida kabisa mtu akisikia fulani kafariki kuanza kumweka kwenye status mitandaoni na maneno kama RIP!!

Lakini tunafahamu kabisa yawezekana kabisa wanafamilia wameona mwanafamilia fulani asipewe taarifa mapema mpaka yafanyike maandalizi fulani kutokana na changamoto zinazomkabili.

Kwa mfano mtoto yupo kwenye mitihani yake ya mwisho, au ni mgonjwa wa presha n.k.

Kwa mazingira ya sasa imekuwa haiwezekani kumficha mwanafamilia fulani kwa manufaa mapana ya familia. Naomba sana usitangaze kifo cha yeyote bila kibali cha mkuu wa familia hiyo.

Kuna familia zimesababishiwa vifo kwa mtu kuona status ya mtu inaonesha kifo cha mtu wake wa karibu kutokana na presha!!

Naomba sana.
 
Kwà mfano kuna askofu mstaafu wa kanisa fulani amefariki uxiku wa kuamkia tarehe 25/12/2021, watu wakaanza kurusha taarifa hizi facebook wakati hata tovuti rasmi ya kanisa haijatoa taarifa hizo rasmi. Hii ni mbaya sana!!
 
Imekuwa kawaida kabisa mtu akisikia fulani kafariki kuanza kumweka kwenye status mitandaoni na maneno kama RiP!! Lakini tunafahamu kabisa yawezekana kabisa wanafamilia wameona mwanafamilia fulani asipewe taarifa mapema mpaka yafanyike maandalizi fulani kutokana na changamoto zinazomkabili. Kwa mfano mtoto yupo kwenye mitihani yake ya mwisho, au ni mgonjwa wa presha nk. Kwa mazingira ya sasa imekuwa haiwezekani kumficha mwanafamilia fulani kwa manufaa mapana ya familia. Naomba sana usitangaze kifo cha yeyote bila kibali cha mkuu wa familia hiyo. Kuna familia zimesababishiwa vifo kwa mtu kuona status ya mtu inaonesha kifo cha mtu wake wa karibu kutokana na presha!! Naomba sana.
Hao wa mitandaoni wanajuaje kama siyo hao ndugu wa marehemu ndiyo wanatoa taarifa, ninavyojua mfano mtu akifia hospital baada ya Daktari kuthibitisha mwili huwekwa mochwari huku ndugu wanao uguza wakitaarifiwa Sasa hao ndugu wakiamua kukaa kimyaa nani atajua?
 
Imekuwa kawaida kabisa mtu akisikia fulani kafariki kuanza kumweka kwenye status mitandaoni na maneno kama RiP!! Lakini tunafahamu kabisa yawezekana kabisa wanafamilia wameona mwanafamilia fulani asipewe taarifa mapema mpaka yafanyike maandalizi fulani kutokana na changamoto zinazomkabili. Kwa mfano mtoto yupo kwenye mitihani yake ya mwisho, au ni mgonjwa wa presha nk. Kwa mazingira ya sasa imekuwa haiwezekani kumficha mwanafamilia fulani kwa manufaa mapana ya familia. Naomba sana usitangaze kifo cha yeyote bila kibali cha mkuu wa familia hiyo. Kuna familia zimesababishiwa vifo kwa mtu kuona status ya mtu inaonesha kifo cha mtu wake wa karibu kutokana na presha!! Naomba sana.
Msiba ukiwa kwako hutapata hata nguvu ya kupost....wanaweza kwakuwa ni wa jirani. Ila sio vizuri kuweka status za msiba ovyo ovyo
 
Huna neno lolote la kuwaambia wasiojulikana ambao wameleta vilio na machungu makubwa mno yasiyokuwa na maelezo kuliko hawa wanaoandika humu? Angalia bila hawa, leo tungejua je kuwa Askofu Desmond Tutu katutoka?
 
Msiba ukiwa kwako hutapata hata nguvu ya kupost....wanaweza kwakuwa ni wa jirani. Ila sio vizuri kuweka status za msiba ovyo ovyo

Unaeleweka mkuu. Nikupe pole tena kwa msiba uliokupata. Hali unayoipitia wengi tumeipitia, haizoeleki na hadi tutakapoitwa wenyewe tutaendelea kuipitia.

Mola akutie nguvu. Mola atutie nguvu.

Wengi wetu tumepita na tunapita katika machungu haya ya misiba. Ni kweli kuwa msiba unaokuhusu maumivu yake hayaelezeki.

Manesi, madaraktari na mortuary attendants hushughulika na maiti za watu wengine katika hali ya kawaida kama kazi. Wakiongea yao na kucheka kama Kwamba kila kitu ni shwari kabisa.

Hao hao wakute kwenye misiba inayowahusu. Hapo si ndipo utapoyastaajabu ya Mussa:

"Ni wakushikilia hata kusimama wenyewe hawawezi."

Ndiyo maana wanasema "aibu ya maiti aijuaye mwosha."

Maisha ndiyo yalivyo.

Kifo hakizoeleki.
 
Kuna vitu huwezi ku control. Halafu kuna vitu sio siri. Sasa msiba nao ni siri?
Jamaa anazungumzia suala la kusambaa taarifa....

Kama ndugu zako kwenu ni wazima wa afya hakuna mtu mwenye matatizo ya moyo mshukuru Mungu.

Ila kuna watu wameshapoteza maisha kwa kukutana na taarifa za ghafla kama hivyo kwenye status.
 
Siwalaumu wapasha habari. Misiba mingi tumeijulia mitandaoni mingine hata ikiwa inakanushwa vikali:

IMG_20211221_134205_429.jpg

Vifo vya akina Mandela, Mkapa, Magufuli, Tutu nk vimesikika mwanzo mitandaoni.

Kujaribu kupambana na teknolojia ni kupigana vita vya kushindwa.

Tupigane dhidi ya wasiojulikana wanaotufikisha huku:

IMG_20211225_085219_327.jpg

Kwa bahati mbaya sana mleta mada ni sympathizer wao.
 
Si walaumu wapasha habari. Misiba mingi tumeijulia mitandaoni mingine hata ikiwa inakanushwa vikali:

View attachment 2058062

Vifo vya akina Mandela, Mkapa, Magufuli, Tutu nk vimesikika mwanzo mitandaoni.

Kujaribu kupambana na teknolojia ni kupigana vita vya kushindwa.

Tupo game dhidi ya wasiojulikana wanaotufikisha huku:

View attachment 2058065

Hiyo misiba unayosema uliisikia mitandaoni haimaanishi taarifa zilianzia mitandaoni.

Huenda taarifa zimeanzia huko kwa ndugu ndio baadae ikatangazwa mitandaoni.
 
Unaharibu uzi wa mwenzio kisa unachuki binafsi na JPM! Angalia hutapata maendeleo kisa ni chuki kwa mtu aliyekwisha fariki! Lini utapevuka wewe Mrundi?
 
Hiyo misiba unayosema uliisikia mitandaoni haimaanishi taarifa zilianzia mitandaoni.

Huenda taarifa zimeanzia huko kwa ndugu ndio baadae ikatangazwa mitandaoni.

Sikukatalii kwa unayoyasema.

Ni kweli kuwa misiba mingi hata hii unayoiona humu huanza na ndugu lakini si yote.

Bila shaka huu haukuanza na ndugu:

IMG_20211221_134205_429.jpg

Kupambana kuzuia taarifa kusambaa ni kupigana vita vilivyoshindwa.

Tupambane kuzuia vifo ikiwamo kuwakemea vikali wasiojulikana wanaotugawia vifo kama njugu.
 
Muanze kwanza kushughulikiana humo humo ndani mwenu usilaumu watu wa nje! Wa nje atajuaje kama hayajatoka ndani!? Ndani mwenu mmeshindwa kuihifadhi hiyo siri, mimi mpita njia yanihusu nini kuihifadhi?
 
Issue sio kuhifadhi siri ndani....msiba unaweza kutokea lakini wana familia wakawa sio wote wenye taarifa.

So kitendo cha kuweka taarifa za msiba status hovyo hovyo zinaweza kusababisha matatizo kwa ndugu wengine watakapopata hizo taarifa kupitia mitandao ya kijamii!
 
Taarifa ya msiba ni lazima itoke rasmi kwa wanaohusika kwanza na ndugu zao wote wameshapeana taarifa. Tunachokataa ni mtu baki kuwa wa kwanza kutoa taarifa mtandaoni hadi ndugh wengine wanashigjliwa kwa kupigiwa simu za pole kumbe hata taarifa bado hawajazipata. Nina mfano hai: Kuna mwanafunzi wa UDSM alikuwa amebakiza mtihani mmoja wa mwisho na tena alikuwa mwaka wa mwisho!! Baba yake mzazi akafariki, ndugu zake wakaamua wasimtaarifu maana kesho yake alikuwa anafanya mtihani wake wa mwisho. Kuna mtu akawa ameweka kwenye status yake ya whatsaap picha ya marehemu na maneno RIP!! mwanafunzi mfiwa akaona ile status maana alikuwa naye kwenye group moja!! Mambo yakaharibika kabisa!! yule mtu aliyeharibu akaishia kusema nilidhani taarifa anayo!! Kuna watu wanachukulia mambo kirahisi sana sijui ni kukosa upeo au ni kuamua tu kujitoa ufahamu!!
 
Siku nikiondoka wekeni uzi hapa hata kama watoto wangu wengine hawajajua.

Wengine walikuwa wanatuma tangazo redioni.

Nyie bandikeni popote hata picha wekeni.
 
Kwà mfano kuna askofu mstaafu wa kanisa fulani amefariki uxiku wa kuamkia tarehe 25/12/2021, watu wakaanza kurusha taarifa hizi facebook wakati hata tovuti rasmi ya kanisa haijatoa taarifa hizo rasmi. Hii ni mbaya sana!!
Mnatakiwa kujifunza,zama hizi karibu kila mtu amekuwa mwandishi wa habari,ile mfumo wa zamani wa kusubiri mpaka chombo fulani maalumu ndicho kitoe taarifa ulishapitwa na wakati.ukitaka kuzuia ni sawa na kuzuia mafuriko.
 
Unaeleweka mkuu. Nikupe pole tena kwa msiba uliokupata. Hali unayoipitia wengi tumeipitia, haizoeleki na hadi tutakapoitwa wenyewe tutaendelea kuipitia.

Mola akutie nguvu. Mola atutie nguvu.

Wengi wetu tumepita na tunapita katika machungu haya ya misiba. Ni kweli kuwa msiba unaokuhusu maumivu yake hayaelezeki.

Manesi, madaraktari na mortuary attendants hushughulika na maiti za watu wengine katika hali ya kawaida kama kazi. Wakiongea yao na kucheka kama Kwamba kila kitu ni shwari kabisa.

Hao hao wakute kwenye misiba inayowahusu. Hapo si ndipo utapoyastaajabu ya Mussa:

"Ni wakushikilia hata kusimama wenyewe hawawezi."

Ndiyo maana wanasema "aibu ya maiti aijuaye mwosha."

Maisha ndiyo yalivyo.

Kifo hakizoeleki.
Asante mkuu
 
Back
Top Bottom