Haya mambo yameishia wapi?? any updates please | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Haya mambo yameishia wapi?? any updates please

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kaburunye, Jul 20, 2010.

 1. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Watanzania tuna ugonjwa mbaya wa kutokufuatilia mambo mpaka yafikie hatima yake. Nadhani vyombo vyetu vya habari ni muhimu visaidie katika hili. Sijui wadau wengine mnasemaje. Kwa mfano sijui mambo haya hapa chini yaliyokamata vichwa vya habari huko nyuma yameishia wapi?

  1. Sakata la Dr Slaa kudai kawekewa vinasa sauti kwenye chumba chake - polisi walidai wanafanya uchunguzi. je huu uchunguzi haukamiliki

  2. Ripoti ya sababu ya mlipuko wa mabomu ya mbagala - Dr hussein Mwinyi alisema ameunda tume na atatoa ripoti hadhari na kwamba atawajibika kama ikionekana kuna uzembe. Hii ripoti imeshatoka?

  3. Kesi za EPA - mwanzoni hizi kesi zilionekana kufuatiliwa sana na tulikuwa tunapata updates za mara kwa mara. Hizi kesi bado zipo au ndo zimekufa natural death??

  4. Kesi ya Zombe - tuliambiwa serikali imekata rufaa? hili jambo linaendeleaje?

  5. Kifo cha utata cha aliyekuwa naibu waziri - Salome Mbatia - tuliambiwa dereva wa lile lori lililosababisha ajali alikuwa anatafutwa? Jamaa kakimbilia mwezini au yuko sayari gani ambako vyombo vya dola haviwezi kufika? je mwenye lori hakutoa msaada wowote ili jamaa akamatwe. Inasemekana mama aliuwawa kwa sababu za kisiasa - maana ndiye alikuwa mweka hazina wa CCM wakati wa uchaguzi na alijua siri nyingi ikiwemo ya EPA

  6. Kesi ya Mramba, Yona na Mgonja - hii kesi ilifunguliwa kwa kumaanisha kweli au ni danganya toto? kipi kinaendelea, naona inaenda kwa mwendo wa kinyonga - au upelelezi bado unaendelea kama kawaida ya jeshi letu la polisi

  7. Kiwira - serikali ilisema inafanya tathmini ya kuuchukua mgodi huu - sijui hili nalo limefikia wapi. Nani anaumiliki mgodi kwa sasa

  Wadau mi ninayoyakumbuka kwa haraka haraka ni hayo. Kama yako mengine hebu tukumbushane. Nadhani itabidi tuwe na register ya kurekodi hizi skendo zote na kuzifuatilia kwa karibu maana tunasahau kwa wepesi sana na kuanza kushabikia skendo mpya mpya na baada ya muda tunazisahau pia. TUTAFIKA kwa staili hiiii???
   
 2. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Utafuatilia wapi?
  Mi nlienda kwenye banda la JWTZ pale sabasaba,
  nikaulizia ripoti ya mabomu, nikaambiwa hayo ni mambo ya wakubwa, hata wao hawajui kitu.
  Siasa na miochezo michafu zinaangamiza taifa letu.
   
 3. m

  mob JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2010
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,028
  Likes Received: 511
  Trophy Points: 280
  samahani je zile kura za wezi na wauza madawa ziko wapi who is the winner
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Jul 20, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,427
  Likes Received: 22,349
  Trophy Points: 280
  Kikwete
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Jul 20, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli watanzania tuna utamaduni wa kusahau mambo ya muhimu kama uliyotaja hapo juu.
   
 6. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #6
  Jul 20, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,356
  Likes Received: 388
  Trophy Points: 180
  Wenzetu ulaya wanafuatilia mpaka kieleweke aisee!!! Sijui Tanzania hatuweki kumbukumbu kwenye diary zetu??
   
 7. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #7
  Jul 20, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Huko ulaya magazeti hayana njaa, hayaandiki ili kupendwa na wenye mamlaka, bali yanaandika ili yakubalike na jamii. Hapa kwetu waandishi wa magazeti wanajitahidi kuandika mambo ambayo yatamfurahisha mkubwa wake au mkubwa wa serikli. kwa hiyo issue kama hizo ambazo zitaipa serikali tension haziandikwi kabisa. Vilevile huko kwa wenzetu kuna wabunge. Sisi hapa kwetu tuna vikongwe vinavyopiga tu usingizi pale mjengoni! sasa ni nani atakayefuatilia hayo mambo?
   
 8. kaburunye

  kaburunye JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo kipi kifanyike?
   
 9. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wezi na wauza madawa
   
 10. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mimi swali langu limebez kwenye spoti.
  Tuliambiwa kuwa Moja ya faida ambayo Tanzania itanufaika na kombe la Dunia kufanyika South Africa, ni baadhi ya timu shiriki kuja kufanya mazoezi katika graundi la Taifa. Hivyo watalipia fees na TFF na Taifa litakuwa limejipatia fadha nyingi na exposure ya kutosha.
  Mpaka kombe la dunia linaisha sijaona hata timu moja zaidi ya Brazil tena kuja kucheza mechi ya kirafiki mechi ambayo imeleta hasara(kimapato) kwa TFF.
   
Loading...