Haya mambo ya uchawi yapo kweli au ni tatizo la watu kukosa elimu na kuamini mazingaombwe ? kila nikiomba ushahidi ni stori za vijiweni bila ushahidi

Haya mambo ya uchawi yapo kweli au ni tatizo la watu kukosa elimu na kuamini mazingaombwe ? kila nikiomba ushahidi ni stori za vijiweni bila ushahidi

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,455
Mfano kuna kipindi rafiki yangu alikuwa ananiambia wachawi wanakuja kwake usiku kuna mapaka yanalia, kumbe yeye hakuwa anajua paka wakiwa kipindi cha joto ndio tabia yao

Jirani alikuwa analalamika kuna kitu kinakwangua nyuma ya ukuta usiku, baada ya uchunguzi tukagundua ni paka alikuwa ananoa kucha zake kwajili ya mawindo.

yupo ambae alikuwa anasikia makelele masikioni na kuzunguka kwa waganga wengi wanaomwambia karogwa kumbe ni ugonjwa unaitwa tinnitus husababishwa kwa presha kupanda au kutumia dawa kali.

Wachungaji na wao wamekuwa wakitumia udhaifu wa imani hasa za wanawake kuwaamnisha kila kitu ni pepo na uchawi, imefikia hatua watu wamekuwa kama maroboti wanaamini kila kinachowakwamisha ni pepo bila kuangalia sababu ya kilichochotokea
 
Moja ya biti lao watakuambi HUJAWAHI KUKUTANA NAO
yaani vitisho tisho tuu

Mtu mzima unaanzaje kuamin sijui chuma ulete? Ukiongelea hizo habari nakuona upeo mdogo wakufikiri.

Chuma ulete kwa wazembe wazembe.
Makonda wamagari wanashika hela ngapi, wahudumu wa Mwendo kasi, Wapokea hela wa kFC, Bank pia

Ila chuma ulete ije ifanye kazi kwa wewe kapuku wa biashara ya vitumbua, muuza mkaa, Duka, wakala wa fedha mzembe.
Kuwa na Na nidhamu na hela na umakini kama utaona hiyo chuma ulete
 
Hivi hili tatizo la kuamini hivi vitu litakuja kuisha kweli Afrika?
Huwa nasikitika unakuta kijana mdogo wa miaka 20 ktk karne hii anaamini kwa nguvu zake zote kuwa uchawi upo masikini.
Juzi kati nilikua na mafundi nikawa najaribu sana kuwaelimisha waache hizi imani ila waliishia kunicheka huku wakisema siku kikinikuta nitaogopa hata kutamka neno uchawi.
Inasikitisha sana kuwa sehemu ya hii jamii.
 
Wao wenyewe wamesikia stories tu tafuta hata mzee wa miaka 100 nae atakueleza habari za kusikia tu , hizo hadithi za uchawi zinarithishwa , na ukivumishiwa unavunga tu watu wakuogope mwenyewe mtaani kwetu nasikia wanadai mimi ni mchawi pia🤣
 
Unaweza ukajiona uko smart kuliko wenzako wanaoaminiamini mambo ambayo kwako unaona ni upumbavu bila kujua kumbe wewe ndio mpumbavu.
Hiyo ndio hulka ya binadamu Yani kujiona yeye mbora kuliko wenzako.
Uchawi ulikuwepo tangu kipindi cha manabii. Hujui historia upoupo tu ila kinafsi unajiona wewe ndio mtu smart kuliko wengine.
 
Ni kweli ni porojo za kurithishana ila yapo mazuzu yanaamini yameona kabisa ila ukimhoji hana cha maana atakueleza

NB:Na mm niliwahi vumishiwa uchawi kidogo iniulie husiano na moja ya viofisi vyangu.

Nahisi ukiwa unawaelimisha watu kuacha hizi imani wanahisi ww ndo stering.Mm iliniumiza sana.
 
Shida sio kujiona smart , shida ni huo uchawi upo wapi?

Hata maambukizi ya HIV kila mtu alidai ni uchawi na kulogwa
 
Ni kweli ni porojo za kurithishana ila yapo mazuzu yanaamini yameona kabisa ila ukimhoji hana cha maana atakueleza

NB:Na mm niliwahi vumishiwa uchawi kidogo iniulie husiano na moja ya viofisi vyangu.

Nahisi ukiwa unawaelimisha watu kuacha hizi imani wanahisi ww ndo stering.Mm iliniumiza sana.
Yeah , ni ujnga ujinga tu
 
Nenda sehemu inaitwa KwaMsisi ipo wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Wabishie kuwa hakuna uchawi. Watakachokutenda uje utoe ushahidi humu.
Hao wazee wa Kwa msisi waliwahi kukataa Barbara isijengwe kisa mizimu Yao haitaki hiyo barabara.Serikali ikatumia ubabe kuijenga Kwa maelezo kama yako kuwa haiamini ktk uchawi. Kila wakivunja msitu ili wajenge barabara kesho yake msitu unarudi. Ilibidi serikali iwapoze Kwa kuwapa pesa nadhani kama 4m ili kuruhusu ujenzi uendelee. Wazee wakakubali na ujenzi ukaendelea. Hii habari ililipotiwa na ITV.
 
Nenda sehemu inaitwa KwaMsisi ipo wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Wabishie kuwa hakuna uchawi. Watakachokutenda uje utoe ushahidi humu.
Hao wazee wa Kwa msisi waliwahi kumkataa Barbara isijengwe kisa mizimu Yao haitaki hiyo barabara.Serikali ikatumia ubabe kuijenga Kwa maelezo kama yako kuwa haiamini ktk uchawi. Kila wavunja msitu kesho yake msitu unarudi. Ilibidi serikali iwapoze Kwa kuwapa pesa nadhani kama 4m ili kuruhusu ujenzi uendelee. Wazee wakakubali na ujenzi ukaendelea. Hii habari ililipotiwa na ITV.
Niliwabishia wazigua wakanipiga mkwara mende tu hakuna kitu
 
Back
Top Bottom