Haya Maisha nyie acheni tu, Mzungu mwenyewe hapa alichoka kabisa

Bill Lugano

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
1,186
6,402
Unajua sisi tumekua katika mazingira ambayo kuna vitu huwa tunaona vya kawaida kumbe sivyo. Yaani tunaamini ndio ilivyo kwa watu wote.

Yale maisha mfano watu walikuwa wanalalamika kuwa bei ya sukari kuna kipindi imepanda nikawashauri badala ya kununua sukari wawe wananunua Asali ndo nzuri zaidi. Lita moja tsh 15,000- 20,000 ile mbichi.

Jamaa walinijia juu sana sikuwaelewa why ushauri wangu iwe ugomvi. Home toka tunakua sisi kwetu issue ilikuwa ni uvivu wa kula yaani mnagombana na mama sababu amekaanga mayai na ninyie mnasema mnataka ya kuchemsha.basi kutukomoa akawa anaweka mayai aina yote. Hapo tunamwambia hatutaki ya kuku tunataka ya Mbuni.

Basi ilikuwa shida mwishowe ikawa kila kitu kinawekwa (buffet) basi tunamtuma mdogo wetu aende akakague nini hakipo ndo aseme tunataka sometimes anarudi baada ya masaa mawili anasema amechoka kukagua breakfast. Basi hapo tunataka breakfast in bed. Tunaletewa.

Alikuja mzungu mmoja ni mfugaji mkubwa sana kule USA. ana ng'ombe 3,800 ni tajiri. Mtoto wake akawa anazunguka zunguka ndani. Akapotea. Masaa kama nane hivi anatafutwa. Imepigwa simu polisi wamezunguka eneo zima.sisi tuliwaambia atakuwa tu mle mle ndani wala hakutoka.

Amekuja patikana kumbe alizunguka zunguka akaingia kabatini alikuwa anasimulia. Mpaka wale askari wa kizungu wakashangaa.

Anasema aliingia cold room moja akakuta imejaa mavyakula, vinywaji n.k (aliingia kwenye friji. Ni zile friji kubwa kama sebuleni za watu wengi huku Tanzania.)

Anasema akazunguka zunguka baadaye akatoka kwenda kwenye chumba kingine kikubwa kipo chini huko akakuta kumejaa dry food nyingi sana. Kumbe aliingia kwenye kabati la kutunzia vyakula ambavyo havihitaji ubaridi.

Wale wazungu wakasema wanataka wakaone. Ikabidi tuwaambie walinzi na wafanyakazi pale home wawape tour.hawakuamini aiseee. Walishangaa sana wakati sisi tunaona ni maisha ya kawaida tu.

Nikakumbuka yule JF member ambaye nlimkaribisha home Oysterbay akaingia kwenye friji akawa anashangaa anasema una chumba cha baridi kikubwa kina mavyakula.nikamwambia hilo ni jokofu.alishangaa sana.

Sasa hayo ni maisha ya kawaida sana kwa sisi.but nashangaa kuona watu wengine wanaona kama ni ya anasa. Nimejifunza watu hawatembei kabisa nchi za wengine wakajifunza. Miezi mitatu upo hapa hapa tu...then ukiambiwa haya mambo huamini.

Next week ntarudi TZ nataka nifanye mpango hata wa kuwaalika wana JF kadhaa home. Wakae hata week. La msingi tu watapimwa afya zao then waje wakae home hata week.

Waone mi naishi maisha ya kawaida sana. Na sasa najikuta mpweke ile screen ninayotumia sasa ni ya inch 160 tucheck latest movies duniani na kucheza games.

Ntawaambia wapishi waje watatu.tuwe tunakula na kunywa tu huku wakinipa stories za uswahilini.nami nijifunze maisha yao.maana nmeambiwa kuna watu wana maisha magumu mpaka wanakula mara tatu tu kwa siku.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom