Kwanini Maisha Wenzangu wamefanikiwa kasoro mimi tu

Utawala2025

JF-Expert Member
Oct 20, 2023
330
1,060
Hii imekaaje.

Watu uliopambana nao kutafuta kazi leo wana kazi nzuri Maisha mazuri wewe unajitafuta bado.

Uliowaacha sekondari au shule ya msingi wakiwa vilaza leo wana maisha mazuri wamepiga hatua ya kujenga na kuendesha magari Makali wewe bado unajitafuta.

Mwanamke aliyekuacha wakati hauna Maisha na akikuambia hauna hela ana Maisha mazuri wala hauna lolote la kumlinganishia tena.

Karibia kila kijana mwenzako unayemuona kuanzia social media na maisha ya kawaida ametoboa sana na ana kila kitu.

Kasoro mimi tu ?

Unajiuliza na kwama wapi?

Na kama tukisema wakati wa Mungu je kwangu mimi utafika lini.

Kusali nasali na mshirika active kabisa.

Biashara umejaribu zimefeli.

Sijui Kazi hakuna barua mahali haujapeleka ,huko utumisbi dodoma mpaka umepazoea.

Wakuu naombeni nipate utajiri kwa Bali yeyote ile kama ni Ufreemason au hata uchawi na mimi mnipe?
 
Nenda Posta Freemason hall direct.

Usisimamishwe na wale matapeli wanaorandaranda karibu na hall. Wale wenyewe wanaogopa kuingia ndani hata kusogelea mlangoni.

Hawa wanaoitangaza masonic mtandaoni nao achana nao maana nao ni wajinga na waoga.

Nenda utapewa vimaswali vitatu hivi takuambia jinsi ya kuyajibu
 
Kwa nini unajilinganisha kwa mambo ya maendeleo tu?

Nina uhakika katika wote uliosoma nao ama kuishi nao, sio wote wamefanikiwa.
Kwa nini usijilinganishe na wanaoumwa na kulazwa vitandani? Kwa nini usijilinganishe na wanaosumbuliwa na matatizo mengi? Ukijilinganisha basi utapata sababu ya kushukuru.

Kila mtu ana zamu yake. Kama ni muumini wa Mungu, basi yeye kwa wakati wake atakufanikishia.

Kama huamini Mungu, basi dunia kwa kutumia nyenzo zake itafanya kwa wakati wake.

Nina uhakika, una sababu moja au mbili za kushukuru.

Jawa na moyo wa shukrani kisha dunia itakupa sababu nyingi zaidi za kuendelea kushukuru. Be Grateful Mkuu.
 
una survivorship bias, unaangalia tu wale waliofanikiwa, japo ndio inaweza ikawa wote ulliosoma nao, watu waliokuwepo kwenye maisha yako zamani, wamekuzidi mafanikio, ila sio kwote.... unakuza mambo.

tafuta namna uache kujilinganisha na watu

ushauri ninaoweza kukupa ni uache kutumia sana mitandao ya jamii, huko ndo unaona watu wanapost maisha mazuri wewe unajiskia vibaya
 
Sina ushauri wowote zaidi ya kutafuta connection basi. We jitupie tu sehemu yoyote kufanya kazi , alafu kuwa mdadisi, mwaminifu na mnyenyekevu, alafu jitahidi kujifunza kila kitu, ukiwa humble na una cheti chako, Mungu anaweza kukusaidia kupata mtu wa kukuvusha . Yaani ujishushe Ili u-gain, unaweza jifunza vitu vingi kwa waqjiri, ila usifanye kazi kwa wahindi, hutagain chochote.
 
Mkuu ikiwa una sali usiache kusali hata kama huoni ishara yeyote.Mimi nilikuwa naombea kuhusu kazi,hapo nimemaliza chuo bado cheti sijachukua,sio mtu wa kutoka,cv sijaitengeneza vizuri kilikuwa kipindi kigumu sana.Kuna muda nilikata tamaa nikasema ee Mungu naomba nionyeshe ishara hii kazi itakapotekea.Hazikupita siku nyingi mama aliota nipo ofisini nafanya kazi na boss wangu ni mhaya.Basi haikuchukua muda kuna link ilitumwa nikatuma tu maombi kama utani nikaitwa.Nikafanya interview nikapita,na baada ya muda nikaja kujua boss wa pale ni mhaya kama mama alivyoota.Hakuna linaloshindikana kwa Mwenyezi Mungu, Mungu ni mkubwa kuliko mawazo yako muamini yeye katika kila hali
 
Hii imekaaje.

Watu uliopambana nao kutafuta kazi leo wana kazi nzuri Maisha mazuri wewe unajitafuta bado.

Uliowaacha sekondari au shule ya msingi wakiwa vilaza leo wana maisha mazuri wamepiga hatua ya kujenga na kuendesha magari Makali wewe bado unajitafuta.

Mwanamke aliyekuacha wakati hauna Maisha na akikuambia hauna hela ana Maisha mazuri wala hauna lolote la kumlinganishia tena.

Karibia kila kijana mwenzako unayemuona kuanzia social media na maisha ya kawaida ametoboa sana na ana kila kitu.

Kasoro mimi tu ?

Unajiuliza na kwama wapi?

Na kama tukisema wakati wa Mungu je kwangu mimi utafika lini.

Kusali nasali na mshirika active kabisa.

Biashara umejaribu zimefeli.

Sijui Kazi hakuna barua mahali haujapeleka ,huko utumisbi dodoma mpaka umepazoea.

Wakuu naombeni nipate utajiri kwa Bali yeyote ile kama ni Ufreemason au hata uchawi na mimi mnipe?
Yaah sometimes inatokea but unabidi kuongeza juhudi na kuchagia jambo moj la kulifanya kwa juhudi zote,

Na iunachokisema sometime unaweza kuhisi umerogwa but no, time bado wakat bado upo
 
Back
Top Bottom