Huku uswazi ninapoishi kuna wale vijana wanaokota chupa za plastic nafikiri wengi mnawafahamu. Wanakuwa very rough hivi. Juzi juzi wakati natoka geto uswazi nikakutana na mmoja na zigo lake la chupa, tukapishana paap.
Kwenda mbele akili ikarudi hii sura mbona naijua? Nilivyogeuka nikagongana nae kageuka ananiangalia akanipotezea akaondoka, njia nzima nikawa najiuliza huyu nimemuona wapi? Baada ya muda akili ikakumbuka ni fulani, tumekuwa nae mtaani enzi hizo!
Kujiridhisha nikampigia simu ndugu yangu mmoja, nikamwambia nimekutana na mtu kama fulani anaokota yale machupa, ndugu yangu huyu akanithibitishia ndio yeye anajua kuwa anafanya kazi hio. Nikakumbuka utotoni, kwao huyu jamaa ilikuwa ni familia mfano wa kuigwa, kila kitu kiko mstari. Baba very strict watoto wanasoma. Kilichotokea hadi huyu jamaa kuwa hivi sijui ni nini. Yote maisha!
Kisa hiki kimenikumbusha siku moja bi mkubwa kanipigia simu. RR jana nimekutana na James supermarket kanipa $500! Anakutafuta! Huyu James wakati nasoma yeye alikuwa level moja na kaka yangu. Mimi form 1 wao form 4. James kwao hali ilikuwa mbaya sana mara nyingi alikuwa anakuja na bro nyumbani weekend analala na kupata mahitaji mengine ya shule. Ni stori ndefu sana, kifupi nilienda kuonana na James tukaongea sana na kukumbushana mengi na sasa hivi ana kampuni kubwa sana ya IT na yuko vizuri sana kiuchumi.
Kuna mengi ya kujifunza hapa.