Haya Maisha Haya.....

RRONDO

Platinum Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
60,043
Reaction score
137,796
Huku uswazi ninapoishi kuna wale vijana wanaokota chupa za plastic nafikiri wengi mnawafahamu. Wanakuwa very rough hivi. Juzi juzi wakati natoka geto uswazi nikakutana na mmoja na zigo lake la chupa, tukapishana paap.

Kwenda mbele akili ikarudi hii sura mbona naijua? Nilivyogeuka nikagongana nae kageuka ananiangalia akanipotezea akaondoka, njia nzima nikawa najiuliza huyu nimemuona wapi? Baada ya muda akili ikakumbuka ni fulani, tumekuwa nae mtaani enzi hizo!

Kujiridhisha nikampigia simu ndugu yangu mmoja, nikamwambia nimekutana na mtu kama fulani anaokota yale machupa, ndugu yangu huyu akanithibitishia ndio yeye anajua kuwa anafanya kazi hio. Nikakumbuka utotoni, kwao huyu jamaa ilikuwa ni familia mfano wa kuigwa, kila kitu kiko mstari. Baba very strict watoto wanasoma. Kilichotokea hadi huyu jamaa kuwa hivi sijui ni nini. Yote maisha!

Kisa hiki kimenikumbusha siku moja bi mkubwa kanipigia simu. RR jana nimekutana na James supermarket kanipa $500! Anakutafuta! Huyu James wakati nasoma yeye alikuwa level moja na kaka yangu. Mimi form 1 wao form 4. James kwao hali ilikuwa mbaya sana mara nyingi alikuwa anakuja na bro nyumbani weekend analala na kupata mahitaji mengine ya shule. Ni stori ndefu sana, kifupi nilienda kuonana na James tukaongea sana na kukumbushana mengi na sasa hivi ana kampuni kubwa sana ya IT na yuko vizuri sana kiuchumi.

Kuna mengi ya kujifunza hapa.
 
Maisha yana kupanda na kushuka......hatuijui kesho yetu
 
kwenye kuokota machupa nadhani kuna kitu kimekuwa kimemtokea huyo mtu, kuna watu wanafanya kazi za ajabu sana ila hawaokoti machupa, wengi wa waokota machupa kwa kiasi fulani kichwani zimepungua
 
'KEEP YOUR CITY CLEAN'

kutunza mazingira ni jambo la msingi sana hasa kwa hizi 'recycled materials'
 
kuna visa kuvisema hapa naingiwa na hofu na mfadhaiko ila kuna watu mambo yalikuwa safi ila sasa yameenda kombo ila yote maisha cha msingi ni pumzi ya uhai, duniani tunapita tu yule unayeweza kumuinua fanya ivyo MUNGU atakubariki
 
Maisha ndivyo yalivyo,
Hata le mutuz pale alipo si kuwa anafurahia basi tu ili mradi maisha yaende na kujifariji na wabebezi!
ha ha ha ha mkuu umenichekesha sana ujue le mutuz ni age mate na wakina jk sema wenzake wametusua yeye alikimbilia ulaya saizi kaludi maisha yamempiga so kaamua kuishi kijanja janja ha ha ha jamaa anamiaka zaidi ya 60 alafu utamuona kwenye after school bash na watoto wa sekondari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…