genious wa kijiji
Senior Member
- May 1, 2014
- 173
- 250
Mwaka juzi nilichaguliwa Chuo cha Mwenge kule Moshi lkn sikufanikiwa kwenda kutokana na hali ngumu ya kiuchumi. Sikuwa na hela hata kidogo na wakati huo ndo nilikua nimetoka form six. Home wazazi ni hohehahe wa kutupwa hawana mbele Wala nyuma.
Sikupata mkopo hata ASILIMIA sifuri hivyo nikaamua kuahirisha masomo nipambane mtaani.
Nikaanza kufanya vibarua kwenye mashamba ya mpunga kule ifakara. Nikapambana nikapata hela kidogo nikaenda maeneo ya kibaigwa nikakodi shamba ekari tatu za mahindi.
Huku kibaigwa Kuna mjomba angu mmoja ndo nikawa nakaa kwake. Nimelima kwa kujibana Sana Nikapata gunia kumi za mahindi. Nilivyouza nikapata laki sita nikaenda kukodi ekari tano huko huko zikawa Saba.
Nikalimia vizuri mwaka Jana kuanzia Novemba. Mahindi yalistawi Sana nikajipa imani kuwa mwaka huu lazima nikaanze chuo maana Kama ningevuna vizuri nisingekosa gunia 50 za mahindi na ningeyauza nisingekosa chini ya million mbili na nusu.
Hii ingetosha kabisa kulipia ada na michango mingine ya chuo.
Wakati napanga hayo mvua kubwa ikaendelea kunyesha. Mashamba yangu yalikua mbugani hivo yaliharibiwa Sana na mvua. Wakulima wa mbugani wanajua jinsi mvua ya mwaka huu ilivyotuletea hasara.
Hivyo sikufanikiwa kuvuna hata debe Moja na hivo sikurudisha hata Mia.
Baada ya kupata hasara hiyo kidogo nichanganyikiwe ndo nikaenda Dodoma kwa ndugu yangu mmoja akawa ananipa bodaboda nafanya deiwaka.
Nimefanya kwa muda wa miezi kadhaa, akapata matatizo akaiuza boda yake hivo hata riziki kidogo nikaacha kupata.
Nilikua nimekusanya Kama laki mbili hivi nikaenda veta kusoma driving. Sasa Nina cheti Cha udereva ila bado Sina leseni. Nikaanza kupambana Tena mtaani.
Nikawa nasaidia mafundi kujenga ila malipo ni ya kutosheleza Kula tu siwez kusevu kwa ajili ya kulipia Ada endapo nitaamua kwenda chuo mwezi wa 11.
Nipo hapa nimechanganyikiwa kabisa Sina Hili Wala lile. Nataman Sana nikasome ila sijion nikitimiza lengo Hilo.
Nikawaza nije humu jukwaan mnisaidie Moja kati ya haya yafuatayo.
(1) kazi
Kama mtu Ana kazi yoyote halali yenye malipo mazuri (kutosheleza Kula na kusevu kidogo kwa ajili ya Ada) anipe connection.
Nipo vizuri kwenye kompyuta, sales management n.k
Mapishi pia nayaweza Sana. Kuuza duka, stationary, na hata kuwa houseboy wa mtu ni sawa kwangu. Napendekeza kazi iwe Dodoma ila hata mikoani Niko Tayari Kama itakua na maslahi.
2. Mtu mwenye bodaboda aniajiri kwa hesabu ya siku au kwa mkataba. Nitafanya kazi kwa uaminifu mkubwa Sana Hadi tajiri utafurahi.
3. Mtu anayeweza kuniajiri kwenye gari. Ingawa bado Sina leseni ila akitokea mtu akanipa gari nauza hii simu chapu ( thaman yake ni 90 elfu) naenda kukata leseni daraja D ambayo ni elfu sabini.
Nikipata gari dogo Kama kirikuu itakua vema. Au Kama Kuna kampuni inahitaji dereva naomba connection.
Ikiwa dodoma itapendeza zaidi.
Naombeni msaada ndugu zangu nipo Dodoma