POLISI Wapo lakini hawana makamanda wa kuwaongoza...wanajiongoza wenyewe mnataka wafanye nini ? eti kutii sheria bila kushurutiswa ndo falsafa mpaya ya geshi letu la polisi,wananchi hawajawahi kshurutishwa kutii sheria leo unataka watii bila kushurutishwa wapi na wapi ? kama Jeshi la polisi lingekuwa na makamanda wanao waongoza mapolisi kikazi,hakika kusingekuwa na maeneo ambayo vibaka wamejitangazia jamhuri,kama vile Jangwani,mkwajuni na mwenge stend,au madereva wa madaladala wasingejitangazia jamhuri yao yenye sheria za kuziba lane za barabara na kusababisha foleni kama vile, Manzese,daladala hufunga lane moja ya barabara kwa kushusha na kupakia abiria wakiwa kwenye eneo la barabara bila kufuata chaki na kusababisha msongamano mkubwa wa magari ambao kimsingi usingekuwepo,Ubungo mataa,madaladala kusimama pembeni ya barabara kusubiri abiria na kuziba njia moja ya barabara na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wengine wa barabara,ubungo mataa moro.rd.daladala kupakia nje ya kituo na kusababisha njia moja tu kutumika na kusababisha msongamano mkubwa wa magari kwenye mataa,Kimara mwisho,kushusha na kupakia wakifunga upande mmoja wa barabara wakiacha kituo cha madaladala,Kimara polisi post ipo mita 100 toka mahala ambapo daladala zimejitangazia jamhuri yao. hayo ni maeneo machache kati ya mengi ambayo mabosi wa barabara wanajiamulia wanachotaka kufanya.
Hii yote ni ukosefu wa makamanda.