Haya jeshi la Polisi Tanzania

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,151
1,427
Kumbe hata wakuu wa nchi wanatambuwa kuwa Jeshi letu la Polisi Tanzania ni la walarushwa

kwani haingii akilini hata mala moja pale ambapo Waziri mkuu anaona ni bora kutumia Jeshi la wananchi kuliko hawa polisi wenye kazi ya kubambikiza watu kesi na kutumika katika mambo ya kisiasa

lakini pia iliwahi kusemwa na Mkuu wa Nchi kuwa ni vyema Jeshi la wananchi likatumika katika kupambana na majangili huko mbugani
kauli hizi za wakuu wa nchi zinaonyesha ni jinsi gani walivyokuwa hawana imani na hili jeshi letu la Polisi


Jamani Jeshi la Polisi Mjilekebishe-watu wanajuwa maouvu yenu
 

JamboJema

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,143
208
kwa nini hao wakuu walalamike badala ya kuchukua hatua? Si wao ndo 'wanalimiliki'? Wanatuthibitishia ni wavivu tu wa kufikiri.
 

Mabagala

JF-Expert Member
Nov 27, 2009
1,481
324
Sasa si walifute tu jeshi la wananchi lifanye kazi zote? kwnza wanajeshi hawana kazi kwasababu hamna vita, wapewe tu majukumu yote ya polisi
 

Mr. Bigman

JF-Expert Member
May 7, 2011
2,560
1,295
Polisi waliopo sasa nchini tz wote wapelekwe likizo ya miezi sita. Wakati huo Jwtz watake charge ya majukumu yote ya polisi wa sasa na Jeshi jipya la Polisi liundwe. Halafu timua ngunguri wote wa sasa baada ya hiyo likizo ya miezi 6 kwani wamezoea kuonea raia wa ngazi za chini kwa kuwapiga, kuwabambikia kesi,kuchukua rushwa. Timua wote
 

H1N1

JF-Expert Member
May 29, 2009
4,217
1,575
POLISI Wapo lakini hawana makamanda wa kuwaongoza...wanajiongoza wenyewe mnataka wafanye nini ? eti kutii sheria bila kushurutiswa ndo falsafa mpaya ya geshi letu la polisi,wananchi hawajawahi kshurutishwa kutii sheria leo unataka watii bila kushurutishwa wapi na wapi ? kama Jeshi la polisi lingekuwa na makamanda wanao waongoza mapolisi kikazi,hakika kusingekuwa na maeneo ambayo vibaka wamejitangazia jamhuri,kama vile Jangwani,mkwajuni na mwenge stend,au madereva wa madaladala wasingejitangazia jamhuri yao yenye sheria za kuziba lane za barabara na kusababisha foleni kama vile, Manzese,daladala hufunga lane moja ya barabara kwa kushusha na kupakia abiria wakiwa kwenye eneo la barabara bila kufuata chaki na kusababisha msongamano mkubwa wa magari ambao kimsingi usingekuwepo,Ubungo mataa,madaladala kusimama pembeni ya barabara kusubiri abiria na kuziba njia moja ya barabara na kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wengine wa barabara,ubungo mataa moro.rd.daladala kupakia nje ya kituo na kusababisha njia moja tu kutumika na kusababisha msongamano mkubwa wa magari kwenye mataa,Kimara mwisho,kushusha na kupakia wakifunga upande mmoja wa barabara wakiacha kituo cha madaladala,Kimara polisi post ipo mita 100 toka mahala ambapo daladala zimejitangazia jamhuri yao. hayo ni maeneo machache kati ya mengi ambayo mabosi wa barabara wanajiamulia wanachotaka kufanya.
Hii yote ni ukosefu wa makamanda.
 

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,151
1,427
Kaka jarıbu kutofautisha R na L.

baada ya marekebisho hayo vipi maoni yako juu ya Mh waziri mkuu kutaka JWTZ ndio wakabidhiwe kazi ya kudhibiti magendo ya sukuari kupelekwa nje ya nchi wakati polisi wakionekana ni kama wala rushwa tu na ndio wanaowakumbatia majambazi?

we si unaona hata wale vijana wa mahenge kifo kiliwakuta kwa kuwa walikuwa na mamilioni ya pesa walivuna kutoka katika madini lakini polisi wakazingizia ni majambazi ili wapige pesa

mimi nadhani jeshi la polisi limeshindwa kazi liwekwe pembeni na JWTZ wachukue nafasi
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,938
Polisi wanachojua kufanya kwa ufanisi mkubwa ni kuua raia wasio na hatia. Lakini wakiambiwa kupambana na wahalifu hawathubutu kutia mguu.

Mtu anakutwa anatembea hata jiwe hajashikilia lakini polisi anamtwanga risasi kichwani na kutoa ripoti ya uongo kwamba alikuwa anajihami baada ya kushambuliwa. Kila siku tunasikia polisi wanazidi kuua raia kwakuwa wakuu wa serikali wamebariki madudu yanayofanywa nao.

Kwa mfano kuna mwananchi aliuawa geita kwenye maandamano ya wananachi waliokuwa wakipinga diwani wao ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa halmashauri ya geita kuvuliwa uongozi. Polisi wakampiga mtu risasi kichwani na kumuua. Jana RPC wa mwanza Liberatus Barlow anasema hata kama ikithibitika kwamba askari polisi ndiye alimuua yule mwananchi, atashitakiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia, haya ndo maajabu ya tanganyika.
 

Power G

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,891
1,190
Kama mkuu wa kaya anachukua rushwa ya suti na kuuza nchi, unategemea askari ambaye mshahara wake haufiki hata laki 2 afanyeje?? Wanawaonea bure tu hawa askari masikini.
 

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,343
23,803
Hii thread nimeisoma leo na imenisikitisha leo jinsi gani tulio wengi hatujui majukumu, mipaka na kazi za Jeshi la polisi na Jeshi la wananchi..so sad indeed!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom