Hawakumaanisha walichokisema

Hawakumaanisha walichokisema

Tumekusamehe KOIKA nishirika la misaada la korea kusini kama lilivyo JAICA la Japan labda ndilo ulitaka kumaanisha ukajikuta umeandika KOIKA na linaitwa KOICA na si KOIKA.
Asante
 
@mshanajr mbona umesahau Mbowe na yeye alileta mbwembwe akarudisha gari la kifahari la serikali huku media zikiona baadae alirudia kimya kimya pia?
Nimezungumzia kwa muktadha wa serikali sio kwa watu tena kwa majina
 
Nakumbuka hata ktk kampeni za uraisi Magufuli aliweka wazi kuwa akiingia madarakani haya magari atauza na hakuna kununua tena haya magari! hadi leo naona kimya au 'anayavutia pumzi'?
Tena ndio yameingizwa mengi zaidi haya new model
 
View attachment 413574
Kuna mahali zamani sana nyumbani kwa ndugu yangu niliona picha ya simba yenye maneno haya NO POLITIC yaani kwa kinyasa hakuna siasa.

Kuna kipindi katika maisha yangu nilivutiwa na siasa wakati ule wa chipukizi na skauti ilikuwa mwaka 1983! Nilikolezwa nikakolea, nikawa na ndoto nyingi...hasa kuwa mwanasiasa mahiri!!!

Sisi kama nchi hatukuwa na uwezo wa kutengeneza gari zetu wenyewe hivyo kama nchi tukaingia mkataba na waingereza kutuuzia magari yao serikalini!

Huu ulikuwa ni mkataba rasmi na ndio maana kipindi chote cha mwalimu Nyerere tulitumia magari ya muingereza Landrover Range rover nk.

Mzee Mwinyi aliposhika hatamu mwaka 1985 akaamua kuvunja mkataba na waingereza na kuingia mkataba mpya rasmi na wajapani wakati huo waziri mkuu akiwa Mzee John Samwel Malecela na naibu wake akiwa ndugu Edward Ngoyai Lowassa.

Mkataba huu ulimaliza kipindi cha magari ya uingereza kutamba nchini na nchi ikaanza rasmi kutumia magari ya kijapani maarufu kama land cruiser, huu ni mradi mmoja mkubwa sana wa mabilioni ya dola!

Wajapani kwa Shukrani yao kwenye hili wakaanza kutuletea magari makuukuu kwa bei poa wakati ule kama jaba na vile vile kutufumba mdomo na kutuziba macho kwa misaada mbalimbali kama KAJIMA KOIKA ya sasa nk nk

Ni takriban miaka zaidi ya 30 sasa tunatumia magari ya kijapani, mapya na chakavu, tafsiri yake ni kwamba mpaka vipuri nk ni vya kwao, ukija kuangalia kwa jicho angavu wajapani wamefaidika na sisi zaidi kuliko sisi tulivyofaidika nao..hawawezi kirahisi tu kukubali watupoteze!

Kwenye duru za siasa serikali ikaanza kupigiwa kelele kuhusu kutumia magari ya gharama kubwa bila sababu! Hii ikawa ni kama mtaji wa kisiasa, na joto lilipozidi watu ili wapate kura wakaanza kutoa ahadi za kutonunua hayo magari tena.

Sensa zikafanyika na baadhi yakaanza kurudishwa serikali kuu ikiwa ni maandalizi ya kuacha kuyatumia! Ilikuwa ni hatua moja mbele muhimu sana kisiasa kuna waziri mmoja wa ujenzi akajizolea umaarufu kwenye hili....!

Alichosahau ni kimoja kwamba hivi vitu vina mikataba rasmi kuwa ili upate msaada fulani inabidi kila mwaka wa fedha uagize toka kwao si chini ya magari kadhaa.

Leo hii pamoja na kelele zote zile ndio kwanza ma land cruiser ya ukweli na new model yanabanana serikalini na wizara na vitengo vyake.

Ukitaka kufanikiwa kwenye lolote maanisha unachokinena na nena unachomaanisha.

Si kila kitu ni matamko ya kisiasa majukwaani, kuna mikataba rasmi kama yale magorofa ya mabepari zikipokuwa ofisi za umoja wa vijana.
View attachment 413586

ALAMSIKI.....!!!!
Dah!ktk vitu ambavyo mpaka leo vinaniuma ni kuona serikali yetu bado inanunua magari ya kifahari hasa haya ma Landcruza V8 wakati hospitali chanjo hakuna,shule shida,madawa kwa ujumla!!au haya magari wanapewa na wahisani labda mi cjui?!ila kama wananunua,hii sio kabisa!
 
Ukiwaangalia kwa mbali kama wazarendo, ukiwasogelea wezi wa kutupwa na tena hawataki kusimangwa wakituibia afadhar na zaman tunaibiwa tunaona na tunawasema
 
Kweli kabisa Wakuu. Kama kuna mahali sijamsoma JPM ni kwenye hii anasa ya magari serikalini. Nilifikiri alikuwa mtu sahihi kabisa kukomesha anasa hii. Lakini sijawahi hata kumskia akiongelea issue hii. Kuna rekodi kibao zilishatolewa kuhusu namna serikali inavyopoteza fedha kwa kuhudumia haya madude. Kwenye mambo ya anasa, sisi watanzania si maskini kabisa. Ni heri watu 500,000 wakakosa umeme lakini kiongozi mmoja akapata landcriser v8 mpya! hizi ndizo akili zetu..
 
RC Dar V8 la nini?
Hili ni swali fupi sana lakini hutapata jibu! Hata mimi naweza kuuliza tena! Hivi RC wa Dar ana umuhimu wowote kutumia gari la aina hii? Kuna magari ya bei nafuu na matumizi nafuu mengi sana amabyo angeweza kuyatumia!
 
Nimezungumzia kwa muktadha wa serikali sio kwa watu tena kwa majina
Acha unafiki bado kijana wewe, kwa hiyo Mbowe kutumia gari la serikali la kifahari ni sawa, anaahidi kurudisha lakini ni mbwembwe tu alifanya mwingine ndio unakuwa uongo.
KATAA KUWA NYUMB.U
 
Back
Top Bottom