Hawajanilea lakini wanataka matunzo

Hawajanilea lakini wanataka matunzo

Masulupwete

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2012
Posts
2,366
Reaction score
2,438
Hawa ni ndugu zangu upande wa mama yangu mzazi. Kifupi, nililelewa upande wa baba. Mama alitengana na mzee na kuwa na maisha yake na familia yake na sijawahi kusikia akinitafuta hata siku moja, ndugu zake pia hawajawahi kunitafuta walau kufahamu maendeleo yangu au tu kujua kama bado napumua.

Nilimjua mama nikiwa mkubwa na ni baada ya mimi kumtafuta sana hatimaye nilimuona. Alionekana kufurahi kuniona kwa sababu sote ilikuwa ndo tunaonana kwa mara ya kwanza. Akanizungusha kwa nduguze ambao nao walionekana kunifurahia pia. Baada ya hapo nikasepa zangu.

Ilipita miaka mingi sijamuona yule mama yangu wala nduguze wala kusikia kama wamenitafuta au wamekuja kujua hali ya huku nilikokulia. Kwangu sikuona shida kwa kuwa nilishazoea maisha na haya mazingira niliyokuzwa nayo kifupi nilikuwa na connection kubwa na hawa walionizunguka.

Kwa miaka ya hivi karibuni huyo mama yangu na hasa nduguze wamekuwa wakinitafuta sana na hasa wanapopata matatizo na kuhitaji msaada. Nikiona simu ya huko basi ni lazima kuna shida fulani inayohitaji msaada, na hasa ni msaada wa kifedha (Nadhani wameambiwa saivi nina kakibarua hivyo ninajimudu).

Nimejitahidi kusaidia inapowezekana lakini uzalendo unaelekea kunishinda. Madai hasa kutoka kwa hawa ndugu wanaomzunguka huyo mama yangu yamekuwa mengi na yasiyoisha imekuwa ni kama ni vile nina madeni kwao kiasi hata nimechoka. Nachokiona kwa sasa natengenezewa mazingira ya kuwatunza hao watu ambao wengine hata siwafahamu. Nashindwa kuelewa hawa jamaa wanatoa wapi ujasiri huu wakati hatuko connected kiivyo.
 
Ni ndugu zako saidia kama unauwezo wa kusaidia sababu ya yeye kutokuwepo au kutokuwa connected nae haina umuimu, kuna muda utaitaji msaada pia kwao ivyo kuwa mwema kwao
 
Mkuu. Life lina mengi mazito. Sijui kisa na chanzo chao kutengana, ama nin waliambizana kabla ya mtengano. Au kusema je,ilikuwaje kweli hakuwah kutak ukaribu au since day one ,aliondoka mazima. Je kama alikutafuta,kutaka kukuona alikutana na nini!? Hivo ni vitendawili,kama ilivyo tulivyokuwa tuna hadithiana shule ya msingi.


Ktk maisha shits hutokea kila uchao. Kwa gape la miaka ilitokea kati yenu. Ile bonding kama mama na mtoto imeliwa na wakati na uwepo wa watu wengine. Kilicho baki ni title ya mama na mwana. Ulitegemea makubwa sana, baada ya kukutana naye ,lakin ndio hivyo.

Msaidie yeye ,kama utakuwa na huwezo nalo. Lakini wema usidhidi uwezo, sio kwake tu, kwa ndugunyeyote hata kwa side ya baba yako.

Matatz ya ndugu ,wamekuwa nayo tangu na tangu, hawakuweza kuyatatua, wewe wa juzi huwezi kuyamaliza fanya kwa kiasi, bila kutegemea malipo, shukrani wala fadhia yeyote. Fanya kwa kiasi, na weka clear kwa kauli thabiti zisizo za dhalau wala kejeli,kuwa unafanya sababu akili yako imeona vema na si kwa sababu ni wajibu au haki yao kukudai. Sio deni
 
Mama ndio wa muhimu sababu ni Mungu wa kwanza duniani,haijalishi hajawai kuwa msaada kwako.Hao ndugu waache wapambane na hali kwani waliishije kabla hawajakujua.
 
Hapo ni mama tu....wengine wote unakuwa Mr.sina!
 
Hapo panahitajika hekama ndugu yangu, ila tu kama iko ndani ya uwezo wako wasaidie tu, mana kuna kubaraka nyingi katika kutoa, na wala usihesabu wala usitegemee fadhali, malipo yako Mungu ndo ajuae. Lakini usijiumize fanya kwa kadiri ya uwezo wako ukiwa huna au una mambo yako nayo yanahitaji pesa wambie tu SIIIIIIIIIIIIIIIIINA. Ila mama yako mtunze bila kinyongo wala maswali
 
- Nilichogundua ni kwamba wewe una roho ya uchoyo, na unatafuta sababu ya kujustify uchoyo wako.

- Kama uwezo upo saidia, na kusaidia si ndugu pekee hata ambao huwajui pia.

- Kama uwezo haupo hakuna atakae kushikia kisu.
 
Back
Top Bottom