dev senior
JF-Expert Member
- Aug 12, 2012
- 458
- 557
Habari zenu wakuu..
Siku ya leo asubuhi ilinikuta kasumba iliyonikasirisha kupita maelezo, ikiwa ni mara ya pili ndani ya wiki hii moja nimepigwa faini ya jumla ya pesa taslimu laki moja na themanini elfu (180,000) na hawa watu wanaokamata magari maeneo ya mjini maarufu kwa jina la YONO (tambaza auction mart & general broker).
Nakiri kwamba, mara ile ya kwanza nilikuwa nimefanya kosa. kwa sababu nilipaki sehemu sio, nikimsubiri mtu pembezoni ya barabara maeneo ya gerezani...japo sehemu ile niliyopaki kulikua hakuna kiashiria chochote ninachokataza kupaki eneo lile... baada ya dakika takribani 4 kundi la watu kama watano walinivamia na kujitambulisha kama mawakala wa YONO ( tambaza auction mart), na kuniambia kwamba nimefanya kosa ivyo natakiwa niende yard yao iliyopo keko nikalipe faini hiyo 50,000.
Ndipo nilipoenda na wale jamaa mpaka kwenye jengo ilo la serikali, na nikaacha gari hapo nakwenda kulipa pesa hiyo benki ya crdb, na kisha kupeleka pay-in-slip halmashauri... lakini cha ajabu nilipofika pale na kuwaonyesha stakabadhi za halmashauri, walinikabidhi gate-pass yakutolea gari pale yard, na kwakuwa nilikuwa na haraka sikubishana nao, lakini nikawauliza hii ndo risiti ya kuonyesha kwamba nimelipa hii faini.
Yule mdada ambaye ni muhudumu hakuwa na jipu zaidi ya kuniambia "onyesha hii gate-pass pale mlangoni watakuruhusu"...siku ile gate-pass niliwaachia.
Sasa leo hii ilikuwa hivi, nilipita mtaa fulani maeneo ya kariakoo, na nilipofika kwa mbele kuumaliza huo mtaa nikakutana na noah ambayo ilinisimamisha na vijana kama wanne wa YONO wakatoka kwenye ile noah... wakaniambia mzee umefanya kosa, nikauliza kosa gani, wakasema umepita kinyume na one way-drive...
Nikauliza kibao kinachoonyesha one way-drive kiko wapi? twendeni mkanionyeshe na nitalipa faini bila hivyo silipi hii faini, ndipo mabishano yaliendelea na wao kugoma katukatu kunielekeza wapi kilipo hicho kibao kilipo... mabishano yalipozidi ndipo wakaita break-down na kuichukua gari yangu mpaka yard yao keko....
Nilipofika keko wakaniambia nikalipe laki moja na thelathini 130,000, nikauliza je, ni lazima niende benki kulipa? Wakaniambia lipa hapo kwa cashier..
Kwa kweli nilikuwa na hasira, leo nilikasirika, hela yenyewe kuipata ilivyokuwa shida namna hii hawa jamaa wananifanyia SIFA namna hii yani wananikomoa.... Kwa kweli nilitamani kulia.... lakini kama ilivyokuwa mara ya kwanza, baada ya kujichanga na kukopa kwa marafiki zangu nilienda kulipa pesa hiyo... lakini cha ajabu sikupewa risiti, na niliuliza kama mara ya kwanza..risiti iko wapi, je kama nimelipa nitajuaje kwamba hii hela imeenda serikalini au halmashauri... yule mdada cashier anayetoa gate-pass akakosa jibu... nikasema hili swala lazima niliulizie maswali...
Hawa YONO nani kawapa mamlaka ya kukamata magari maeneo ya mjini, je ni jeshi la polisi na usalama barabarani au ni halmashauri ya jiji? Kwanini wanatoza faini pasipo kutoa risiti?
Je, hawa watu ni matapeli? Na kwanini hawa watu wanatumia majengo ya serikali, kuendesha shughuli zao?
Je, wizara ya mambo ya ndani imeshindwa kutumia jeshi la polisi kuendesha operation kama hizi?
Gate-pass yenyewe hii hapa..
Kwa kweli leo nimejiuliza maswali mengi wakuu.. Kwa dhati naomba kufahamishwa kuhusu hawa wanyang'anyi..