zitto junior, Sina uhakika kama ni Zitto ninaemsikiaga,ila kama kweli ni wewe au alietumia jina na picha yake,hakika unastahili kukaa kwanza na kufikilia upya ulichokiandika.
Historia ya Rwanda ni ya pekee,historia ya Tanzania ni ya pekee,hivyo,sina budhi kukwambia kwamba kamwe siasa za nchi hizi lazima ziwe sawa.
Kamwe hutoelewa historia ya Rwanda kama mnyarwanda,kamwe hutofeel maumivu waliyoyapata wanyarwanda,wawe walioua,waliokuwa wakiwindwa,na kila mwenye moyo wa kibinadamu.Hivi nikuulize Zitto,uliwahi angalau kuja Rwanda ukapate taarifa huko huko site kuliko hizi unazosoma magazetini na kuhadithiwa! Kama ni Zitto naekusikiaga,kaka yangu,kwenye siasa haya yapo sikatai,lakini,kama umeweza kuona thamani ya damu ya Lissu,kwa kujeruhiwa,ukafumbua mdomo wako na kutaka haki itendeke,kwa nini unaona Kagame ndo dictator? Hii ingekupa picha kamili ya maisha ya watusi unaowataja kuwa wababe leo,kuanzia miaka ya 1958. Kama unaijua thamani ya uhai wa binadamu;
-Unaweza kunieleza faida au ushujaa wa kuchinja mtu kwa kisu,panga,mkuki au siraha nyingine!
-Unayajua maumivu ya mzazi kutwangiwa kichanga kwenye kinu,na mwanamke aliyezaa!
-Unawaza nini kuhusu kifo cha wanawake watusi unaowasema,wakioshindiliwa milingoti sehemu zao za siri mpaka wanakata roho?!
-Unajisikiaje mwanamke,sawa na dada yako au mama yako,wanaume wanapishana juu ya kifua chake,kwa kulazimishwa,kisa wasikie utamu wa kabila tofauti?
-Ni kama wapi uliwahi sikia mtu analipa pesa ili auwae kwa risasi lisitumike panga?
-Umewahi angalau kuwatembelea walionusulika,wenye makovu ya wazi wakupe angalau historia yao?
Ni mengi tu lakini hayo ni badhi.Sasa basi, kama mtu huna msaada wa kumpa,usimpotoshe,kwa sababu hata kilichotokea ni uchochezi wa kuwaonyesha badhi ya watu kuwa wao ndo bora.
Watusi hao,walikimbilia nchi za watu kama watutsi, wakarudi wakiwa inkotanyi,wakapigania haki yao,walivyokomboa nchi wakawa wanyarwanda tu,si vingine,la hasha.
Kuna majina uliyoyataja,ila tu nikwambie kwamba yapo mengi,na nwingine atakayejisikia kuwekwa kwenye orodha hiyo atawekwa tu.
Rwanda ni nchi ya wanyarwanda,si shamba la bibi ambapo wajukuu wanatakiwa wajitawale.
Kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake,lakini endapo hayahatarishi maisha ya wenzake au kuwatishia amani.Je,uliwahi kuuliza wahusika chanzo cha hao kuwa huko waliko? Kama haki mnayopigania kwenu huko,hata wanyarwanda wana haki sawa. Wenye itikadi kama za hao,ndo chanzo cha maovu yaliyoikumba nchi. Ni kweli alipigana vita ya kukomboa nchi,je hiki kinafaa kuwa kigezo cha yeye kutaka kutawala anavojisikia yeye? Hiyo vita alipigana yeye peke yake?Waliopoteza maisha na waliolemaa wasiojiweza,unadhani wanahitaji kuona hali ile inajitokeza tena?
Hamna mnyarwanda aliye juu ya sheria,labda aliyepo nje ya Rwanda,na huyo ayawasumbua anaokaa nao siyo wnayarwanda nchini kwao.
Kiongozi mhutu unayemsema,vita atakayoianzisha ni huko aliko,Rwanda ya sasa inavamia haivamiwi.Kama yupo anayeijamini,msaidieni aje atapokelewa