Empty maisha
Senior Member
- Oct 10, 2020
- 124
- 186
Wakuu habari za usiku na poleni kwa majukumu.Naomba niende kwenye mada. Iko hivi siku za hivi karibuni umeibuka utapeli na wizi wa kutisha na ni hatari sana. Wahanga wakubwa wa tukio hili NI watumishi wa umma hasa walimu waliostaafu.
Katika tukio la hivi karibuni (sitataja mhusika na mahali lilipotokea kwa kuwa vyombo vya dola vinalifuatilia) mama mmoja mstaafu ametapeliwa 14,000,000/=. Uchunguzi wa awali unaonesha mtandao huo wa kihalifu ni mkubwa na unahusisha baadhi ya watumishi wasio waaminifu wanaoratibu Malipo ya wastaafu. Naandika hivi nikiwa na mfano wa huyu mama ambaye nimefanya naya kazi kituo kimoja Hadi anastaafu. Mama baada ya kustaafu alikaa miezi 6 bila kupewa pension ya kila mwezi hivyo alikuwa na madai ya miezi hiyo 6.
Kuna siku wezi Hawa walimpigia simu mama wakajitambulisha kuwa wao NI wafanyakazi wa hazina wanaoshughulikia Malipo ya wastaafu na wakaeleza habari za mama kwa usahihi bila kukosea hata kidogo. Walimweleza kuhusu taarifa zake zote, kituo chake Cha kazi, tarehe aliyostaafu, tarehe ya barua ya kuomba kibali Cha kustaafu na tarehe aliyojibiwa.
Baada ya hapo walimweleza kuwa ana miezi 6 hajalipwa pension ya kila mwezi na wakamwahidi kuwa wanashughulikia Malipo hayo haraka iwezekanavyo na ifikapo tarehe fulani watakuwa wameshamlipa malimbikizo ya pension yake. Siku chache kabla ya tarehe hiyo walimpigia Tena wakimwambia tayari wameshamlipa na alipoenda benk alikuta kweli hela IPO na hawakumtafuta tena.
Siku moja tu baada ya kulipwa mafao yake walimpigia Tena wakamuuliza umeshalipwa mafao yako? Mama akawajibu hapana, wakamwambia tumeshakulipa nenda benk ukaangalie na alipifika benk kweli mzigo upo.Wakamwambia ila umepunjwa 28,000,000/=
Wezi hao wakamuuliza mama umejiunga na NMB mobile mama akawaambia hapana,wakasema ili uweze kupata hiyo uliyopunjwa jiunge NMB mobile na mama akafanya hivyo na tatizo likaanzia hapo.
Baada ya kujiunga wakamwambia bonyeza hivi na vile kumbe mama ndo anahamisha pension yake.
MY TAKE:
1. Hawa watu wanapata wapi taarifa za mtu binafsi za kiutumishi, namba za simu na kibenki?
2. Wanapata wapi mchakato wa Malipo mbalimbali ya wastaafu na kujua Malipo yamefikia hatua fulani na ni taarifa za kweli kabisa?
3. Baada ya tukio hili la mama kutapeliwa,nimeongea na wastaafu mbalimba wengi wao wamekiri kupigiwa simu na mtandao huu ukieleza taarifa za kweli kabisa kuhusu mstaafu husika
4. Kwa nini tusiamini kuwa wanaoratibu Malipo ya wastaafu ndiyo wanaohusika? Kwa nini wasiwekewe mtego?
5. Wastaafu wengi wao hasa walimu analipwa 80 ml au 90 ml baada ya miezi 2 unashangaa hela imeisha kumbe wanapigwa kwa mtindo huu.
6. Wito wangu hawa tuwasadie kimawazo hasa wanapo karibia kustaafu tuwaeleze kuwa taarifa yoyote inayohusu utumishi wako utapata kwa mwajiri wako kupitia kwa aliyekuwa msimamizi wa kazi.
7. Jf NI kubwa hata vyombo vya ulinzi na usalama wanapita hapa wawachunguze Hawa wanaoratibu Malipo ya wastaafu Kama NI hazina,tamisemi wakurugenzi na watu wa TSC hawa wanaweza kuwa ndo chanzo Cha matatizo.