Hawa watoto wanaofanya gwaride ni wanaccm?

carefree

JF-Expert Member
Dec 19, 2010
266
47
Havi hawa watoto wanaofanya gwaride la maadhimisho ya miaka 34 ya ccm ni wanaccm au wanafunzi wametolewa shule wkt huu ni msimu huu ni wa masomo?
 
hao watoto ni njaa yao ya wali na kupenda t shirt na track suit za bure ndo kumewafikisha hapo si ulimsikia makamba akiwahamasisha kwamba kesho watakula pilau na kumwagiza katibu aaandae pilau kesho. Ikiwa wazazi wao walihongwa t shirt, kofia na kanga wakawachugua sembuse watoto wao no wonder dodoma iko nyuma kielimu wanaendekeza vya bure wakati vya bure gharama
 
Si serikali iliwahi kutoa waraka wa kuzuia wanafunzi kutolewa madarasani kushiriki siasa?
 
Si serikali iliwahi kutoa waraka wa kuzuia wanafunzi kutolewa madarasani kushiriki siasa?
Serikali ya ccm kusema na kutekeleza kwao ni tatizo kubwa sana..tena nakumbuka kauli hiyo aliitoa pale udom....l
 
Wameahidiwa wali, ukipita karibu wape hi, watauinua ile ishara ya vidole viwili ndo utajua they are for who!
 
Watoto hawa hawana itikadi yoyote ile, ila tu ni suala la wazazi kuwashinikiza ili waweze kushiriki ktk siasa hizi. Tatizo sugu ni pale tutaposema A na kutimiza Y, safari bado ni ndefu ktk nchi yetu
 
Si wana CCM na pengine wangeelewa CCM inapaswa kujibu kwa maisha magumu waliyonayo wangewatoboa macho hao viongozi wanaoshirikiana nao kuandaa gwaride.....its funny watoto wa shule za private wako darasani wanasoma,St Kayumba zetu ndo wanapiga gwaride kwa kuahidiwa pilau....:coffee:
 
Wanawapotezea masomo na muda bure watoto. Hao wakikua watakuwa CHADEMA kama kaka zao!
Na Sisiemu itakuwa ishakufa na kuzikwa!
 
CCm tutawashitaki kwa kukiuka mkataba wa kimataifa wa haki za mtoto uliokubaliwa mnamo mwaka 1989 na kusainiwa na kuridhiwa na Tanzania mnamo mwaka 1990 katika kipengele cha 1,33,34,36,39 vinaleza kwa uwazi umuhimu wa kumlinda mtoto kutokana na ukatili uonevu na unyanyasaji,kipengele cha 1 kinaeleza kabisa heshima ya mtoto leo hii watoto wanatundikwa kwenye mazoezi karibu wiki mbili zimepita wanashinda juani hakuna choo wapewi chakula wamekoseshwa masoma hawapumzishwi na pia hawana itikadi kwani hawajafikia umri wa miaka kumi na nane,mkataba unakatazwa kuwatumia watoto kwenye matangazo wanachofanya CCM na serikali yake wanachofanya ni kuwatumia watoto kutangaza CCM kinyume cha hata sheria y a mtoto ya Tanzania ya mwaka 2009.
Wazazi na walimu pi wanatakiwa kuchukuliwa hatua kwa kuridhia CCM kuwatumia watoto kwenye matangazo ya CCM kuwadhalilisha kwa kuwavika kofia kubwa kuliko vichwa vyao kwa maana hivyo kuwatesa sana na mifulana ambayo iko kama magauni
Makamba na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma lazima wafungwa kwa kuwahonga watoto kesho pilau na maji kama walikuwa wanawajali kwa nini walikuwa ha wawapi pilau watoto wakati wa mazoezi
hata kwenye ripoti ya watoto inayopelekwa na wanarakati itabidi iorodheshe kiwango cha ukatili kwa watoto na uvunjifu wa haki za watoto kwa kiwango cha juu na serikali ya Tanzania kupitia chama chake
kwa kifupi CCM hawajifunzi kabisa
 
Watoto hawa siyo wa Ccm ni minors. Vipi wanaharakati wa haki za watoto mko wapi? Tusaidieni. Hivi wanapatikanaje? Huko shuleni na chama kingine kikienda watapewa?
 
Back
Top Bottom