Hawa watoto ndio maana wanafail aisee | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hawa watoto ndio maana wanafail aisee

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Sangarara, Feb 9, 2012.

 1. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Kuna Binti mmoja kutokana na uzuri wake ililazimika abaki kwenye kumbu kumbu zangu
  tangu mara ya kwanza tukutane Dukani Jirani na Maskani yangu. Baada ya nazani nilifanikiwa
  kumuona mara ya pili akiwa amevaa school uniform ndo nikajua kwamba ni Mwanafunzi.

  Sasa Jana Jioni, baada ya kufika home nikalazimika kwenda Bar Jirani na nyumbani ili nipate
  serengeti zangu ndogo za baridi, nilipofika Bar nikakutana na Kijana mmoja mjanja mjanja
  sana, na kafunga ndoa hivi karibuni, alikuwa akiingia Bar kama mimi, na sababu hatujaonana
  muda mrefu tulipokariaba tukaanza kupeana salamu, hagi nyingi, vicheko, gonga sana mikono.
  Haya yote tulifanya tukiwa jirani kabisa na meza ambayo kuna mabinti watatu walikuwa wamekaa
  na sikuwa nimewali sababu niliishawapa mgongo pia by the time,

  Sasa Jamaa akaniuliza, vipi wife kaishajifungua, sikumjibu bali nilimtolea simu na kuanza kumuonyesha
  picha za uzao wangu, twe twins. a baby boy and a baby girl, nikamtajia na majina yao, sasa
  huku jamaa akiwaanawashangaa matwins wangu kwenye simu, nikamsikia binti mmoja katika wale watatu
  anayarudia majina ya watoto wangu, nikageuka kumuangalia, na yeye akawa ananiangalia, ikabidi nimpe
  tano (nikagonga nae) huku namuambia uko juu hayo masikio sio ya kawaida - Na alikuwa ni yule
  binti mzuri mwanafunzi. ndo apo nikagundua kumbe anapiga mvinyo pia, maswali mengi sana
  yakapita kichwani mwangu muda huo huo, lakini nika let it go.

  Then Jamaa huyu akaniambia vipi, karibu tukae mi niko na dada zangu hapa, nikakwepa, nikamueleza kuna
  mtu namsubiri tunamaongezi hivyo ngoja nikakae palee, nikamplease kidogo na yeye akanielewa.

  Cha Hajabu
  Wakati naanza Serengeti ya Pili, Yule Jamaa akaja, akaniuliza, una mfahamu yule binti, nikamuuliza yupi,
  akaniambia yule kanyoa nywele (binti mzuri), nikamueleza navyo mjua, na kwamba hata Jina wala anaishi
  wapi au kusoma wapi sijui.

  Jamaa Akafunguka
  Hoo Binti anakaa na dada yake mtaa wetu huo huo (huyu kijana anaishi mbali ha hapa kidogo), akanielekeza
  nyumba, na akaanza kunieleza anaishi na nani, ikabidi nimuwahi, kwani vipi? Hoo unajua huyu binti pale
  kaja na rafiki zake, ili mimi kaniagiza kwako. "nikasema kimoyo moyo kazi imeanza". Oooh anakufahamu
  sana, na amefurahi sana pale mlipogongesha mikono, "nikajua hili gemu kali". Oooh, na ameishaambiwa
  mke wako mkorofi sana hivyo anaomba tuhame hapa twende sehemu ingine ana maongezi na wewe.
  Nikamuuliza Jamaa, wewe unafanya nini na wale mabinti, mnaongea nao nini? Jamaa akaniambia tutaongea
  mbele, akaniuliza tunaenda wapi. nikamuambia akamuuliza huyo binti anataka twende wapi, Ile Jamaa
  anasimama tu kuelekea kwenye meza ya wale mabinti. Nikampigia simu wife aje Bar haraka sana, na fasta
  nikawaagizia ile meza vinywaji na nikalipa. Wife alipikuja nikamuambia nikamuambia nilijisau kuja na pesa
  Bar kwa hiyo kama kaja nayo anilipie bia mbili tuondoke, akakubali akalipa na tukaondoka. nikawa
  nimemkwepa Ibilisi.

  Tatizo ni kwamba, Nimeamua kutoa mchapo huu, sababu mchana huu, Nimepokea message iliyotoka kwa
  huyo binti inasema
  "Babbie, Pole na Kazi, Jana Mke wako aliharibu mipango yetu, mi nshatoka shule, naomba unieleze nikufuate
  wapi ukishatoka Job, Loving you. Jina"

  Hapa nimechanganyikiwa, namtafuta huyu rafiki yangu kwenye simu kumuuliza kwa nini kampe yule binti
  number yangu, simu haipatikani. Na ninajiuliza huyu mtoto nikimkimbia zaidi na ndio kaanza kutuma mimessage
  hili swala litajulikana kwa mama wawili sasa hivi.

  Naomba ushauli wenu, ninachokifikiria nimuelekeze sehemu tukutane alafu nimcouncil kujihepusha na haya
  mambo. Au ndio ntakuwa natenda wema kupita uwezo???
   
 2. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hee, Baba wawili, hii thread inahamia nyumbani! I am waiting for you
   
 3. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Sasa hapo cha kuchanganyikiwa ni nini?Kama utaki kufanya ushetani huyo binti mdogo sana wa kukushinda wewe.Wewe una uwezo wa kukataa au kukubali.Mwambie wewe hutaki kufuatwa fuatwa na atakusikia lakn ukiaanza na sauti za kike ...ohh mie sitaki bwana!!!!.....utaharibu ndoa yako hivihivi...
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,521
  Trophy Points: 280
  kimenukaaa
   
 5. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Dah wewe shujaa wa mwezi JF,kuna watu sasa hivi wanakulaumu kweli,we subiri!
   
 6. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Ndefu mno, ntasoma jioni.
   
 7. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #7
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  duuu! haya mpe ushauri km member wa jf then mkagombane nyumbani km wanandoa!
   
 8. sister

  sister JF-Expert Member

  #8
  Feb 9, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,027
  Likes Received: 3,933
  Trophy Points: 280
  na wewe mwambie hivi, we katoto sikia sitaki unifwate fwate wala unitumie hizo massage zako, au nenda kwenye mtandao wa simu anayoitumia ukaifungie namba yake asikutafute.
   
 9. client3

  client3 JF-Expert Member

  #9
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 6, 2007
  Messages: 742
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  yaani siamini kabisa kwamba mtu mzima kama wewe ushindwe kuhandle ka-issue kadoooogo ka kibint hako eti mpaka uombe ushauri,sasa ukikutana na mijimama iliyokubuhu ya mjini hapa si utajikuta umempeleka kwako akawe 2nd wife,sema na wewe unamtamani tu huna lolote.
   
 10. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #10
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Huyu ni Juma,
  Juma ana Dada
  Dada yake Juma ni Roza...
   
 11. mtekula

  mtekula Member

  #11
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 19, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mpe cheupe tu ukimpa nafasi tu umekwisha wangu chezea wanawake wewe utajuta kufanya nae meeting isiyo rasmi shauri yako.
   
 12. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #12
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Ninachokifikiria ni kwamba, baada ya meeting ya, kakiendelea kunisumbua naliwasilisha nyumbani mwenyewe
  wife anisaidie.
   
 13. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #13
  Feb 9, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Ha...ha..ha dah!! Nimekuelewa saaaana!!
   
 14. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #14
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Client3
  Katika mambo ambayo namshukuru mwenyezi Mungu kwamba wakati wote huwa nayahandle kwa kufikiria badala ya feelings ni
  namna ya kuzihandle issues kama hizi, sababu ni very common kwenye maisha ya kila kitu. Mi nimeshare na wadau hii issue sababu
  nimeumizwa na matokeo ya form four yalivyo mabaya. I will give you a very positive feedback, hofu yangu ni kama atabadirika tabia
  moja kwa moja.
   
 15. M

  Mundu JF-Expert Member

  #15
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Juma anasema
  Tia chai Roza
  Tia maziwa
  Tia Sukari...
   
 16. Vaislay

  Vaislay JF-Expert Member

  #16
  Feb 9, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 4,512
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  mwambie akukome baba twins
   
 17. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #17
  Feb 9, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Hii ni confrontation: Binti ananipigia simu kuniuliza kama nimepata message yake, nimemuambia nimetapa. kakata simu,
  the kanitumia message nimjibu. Wazazi tunakazi.
   
 18. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #18
  Feb 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  I wiil be back soon!
   
 19. J

  Jrafiki Member

  #19
  Feb 9, 2012
  Joined: Dec 23, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ujana unakusumbua wewe.
   
 20. S

  Shansila Senior Member

  #20
  Feb 9, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 189
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada,ni PM namba ya huyo dogo ili nimcounsel,humtendei haki huyo dogo.
   
Loading...