Hawa watoto ndio maana wanafail aisee

Kaka Sangarara asante sana kwa kushare experience na sisi. Nami naomba namba yake ili nikuepushie matatizo kwenye ndoa yako. mbona mimi ambae sijaoa havinisumbui sana zaidi ya salamu tu asbh nikienda kazini? au niko serious mno? usisahau kunipa nmba, kama yeye alivyopata namba yako, basi na mimi naomba namba yake

akikupa namba ukamshindwa nirushie mie ndo mtaalamu bwana!
 
sijaona sababu ya wewe kumuita mkeo hapo kukwepa ibilisi, suppose imetokea nje ya mkoa ukiwa safarini......?
 
Sangarara na hadithi yako ndeeefu. kisa na mkasa wa kutoa namba yako ya simu kwa binti huyu wa mwanaume mwenzio ni nini kama hukuwa umenuia!! Mabadiliko ya vijana wetu huanza kwa wazazi kama ninyi. Ubarikiwe sana mzazi mwenzangu
 
kwa nilivyokusoma inaonekana unakamind hako kadent mzee,wat a coincedence,mnakutana bar,dukani!t seems ur interested na huyo mrembo whether ukimuona unamuangalia kupita maelezo,thts y mtoto kaona afunguke mwenyewe
 
pole sana.
Heri ukamsimulia mkeo issue nzima mapeeeeeeeema ataimaliza yeye.

Watoto wa siku hizi maadili hakuna, wazazi hawana muda na watoto, na jamii inaona mtoti wa mtu mwingine ni mkubwa mwenzie, tofauti na enzi zetu ambapo kila mmoja kwenye jamii ana wajibu wa kumwadabisha mtoto.
 
pole sana.
Heri ukamsimulia mkeo issue nzima mapeeeeeeeema ataimaliza yeye.

Watoto wa siku hizi maadili hakuna, wazazi hawana muda na watoto, na jamii inaona mtoti wa mtu mwingine ni mkubwa mwenzie, tofauti na enzi zetu ambapo kila mmoja kwenye jamii ana wajibu wa kumwadabisha mtoto.

Kuna mwingine alikuwa anaishi na wazazi huku amejioza kwa mwanaume. Anatoroka kwao kwa kisingizio anaenda kusalimia ndugu kumbe anaishi na mume wa mtu (mkewe kaenda kijifungua mkoani). Sasa matokeo yametoka ana Div 4 ya 32. Sijui hali yake ikoje!
 
Kutana naye umwambie huhitaji hicho anachofikiria, na
umwambie wazi huhitaji mawasilino naye. Ukicheza na mbwa ....
Ni lazima akutane nae? Kumbuka jamaa ameshakolea na uzuri wa bint. Kwa nini asimkomeshe kwenye simu?
 
Wanajamii, Naomba niwape feedback.
Jana nimekutana na huyu Binti mida ya saa na moja nusu jioni, tumeachana nae around saa tano kamili, lakini kuanzia saa kumi jioni ndio nilipata picha wanawake huwa wanakuwa kwenye wakati mgumu namna gani wakati wanatongozwa, kilichonisaidia ni kwamba nilikuwa naifurahia sana hii experince ya huyu binti, mchaka mchaka alionepeleka nao ndani ya masaa kama nane kuanzia saa tisa mchana sijawahi kuupitia huko nyuma. Nitawaeleza kila kitu.

Naomba niende straight kwenye point, sababu members wengine nimeona wanalalamika nimeweka maelezo mengi sana, japo najua maamuzi yatawanyima information nyingi sana juu ya kilichojiri Jana.

Kwa kifupi ni kwamba.
1. Yule binti ana umri wa miaka 21, na juzi jumanne ndo amemaliza mitihani ya form six alikuwa anareseat.
2. Si kweli kwamba Yule binti alikuwa akinifahamu, sababu alinieleza Juzi ndio ilikuwa mara ya kwanza kuniona pale Bar Japo
alikuwa anamfahamu Mke wangu- Uzuri na Binti anamkubali wife kwa uzuri, urembo n.k kumbe wanawake
wanaogopana uzuri pia, nimejua Jana. Na hata nilipomueleza kwamba mimi nimekuwa nikimuona several times (chumvi) alikiri
kwamba hajawahi kuninotice even once, yaani hata siku tumekutana Dukani She did not notice my presense. Binti ananyodo kwa
kweli. Infact tulipokutana tu hapo hotelini hakupoteza muda alinirushia lawama nyingi sana kwa kutokuwa responsive kwenye
simu.
3. Baada ya kuwa nimemmaliza nguvu zote za mategemeo ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mimi Binti alifunguka kwamba,
Yule Jamaa yangu ndio alimueleza kwamba mimi ndio namtaka yeye, na kwamba niliishamueleza Jamaa siku nyingi sana juu ya hilo
ndio maana nilitaka kama ingewezekana juzi hiyo hiyo tutoke kwenda kuongea sehemu. Kwamba Jamaa alimueleza binti ,
niko tayari kumpa binti nyumba akae bure na wife wangu ntamueleza kwamba binti kapanga (pumbavu kweli jamaa).
4. Baada ya kumbana binti, alinieleza kwamba yule Jamaa amemuharibia maisha sababu amekuwa anamletea wanamme kwamba
wanamtaka kumbe yeye ndo anamuexpose kwao, then jamaa wakiisha tembea na binti wanasepa kwani baada ya kutembea nae
tu huwa anamgeuka na kuwaeleza yeye ni malaya wa kutupa.
5. Nikamuuliza binti, kwa nini amekubali kujihusisha na mapenzi wakati bado mwanafunzi, hili swali nilipomuuliza mwanzoni kabisa mwa
mzungumzo yetu alinijibu kwamba, kama mimi najua yeye ni mwanafunzi kwa nini nimemtongoza, kumbuka mwanzoni nilikua
najua binti ananitaka, baada ya muda swali hilo hilo akatoa majibu linalomaanisha kwamba amekuwa manipulated na Jamaa, na kwamba toka amefika Dar mwaka Jana wanaume aliotembea nao wote kaletewa na Jamaa. Nikamuuliza amefahamiana vipi na Jamaa, akasema Jamaa ni rafiki mkubwa sana wa dada yake lakini dada yake hafahamu lolote linaloendelea kati yao.
6. Nilipomuuliza kama yuko tayari Dada yake afahamu hili swala, binti akakataa, nilipomuuliza ni kwa nini kama anajua jamaa anamuharibia maisha kwa nini havunji mahusiano nae, akasema Jamaa anafahamu siri zake nyingi sana na huwa anamueleza kwamba akimkatalia Jambo lolote lile, anazimwaga siri zote, nikamuuliza kama jamaa ameishawahi kumtaka kimapenzi, akasema alimtaka kimapenzi mwanzoni kabisa akamtolea nje, lakini baada ya hapo hajarudia kumtaka tena badala yake anamletea midume,

Ilikuwa Simple sana
Tulipofika tu, tukaanza kupiga story za toka jana na nini, binti akaanza kumsifia wife, then akaanza kulalamika kwa nini nachelewa kupokea simu au nilikuwa na mwanamke mwingine, story nyingi sana huku anamsifia jamaa yangu alivyo msiri na yeye akijihapiza kwamba hawezi kufanya mambo ya kitoto yatakayopelekea wife ajue mahusiano yetu, Alinistahji kwa kuvaa kistaharabu lakini ile sehemu tuliyokaa tuliwaharia majirani mapozi kabisa, sababu binti ni mzuri sana na amejaa smiles na vicheko.

Lakini nachoshukuru upepo ulibadirika mapema tu, wakati ndo tuko kwenye bia ya tatu tatu, binti alinishukuru kwa pesa niliyomtumia, nilipoonyesha kushtuka kwamba nimemtumia pesa gani, akaniambia si umempa (akamtaja jamaa) shilingi laki moja mchana ukamuambia aninunulie na voucher ya elfu kumi na ndo ukamuuambia nikutafute kabla ya saa kumi tupange kuonana wapI? Hapo ndo nilijua kwamba Jamaa anahusika, nilipokataa na binti akashtuka vibaya sana, Kimsingi for the fisr time Jana na yeye
ndo aliweza kupata nguvu ya kujua nini kilikuwa kinaendelea kwenye maisha yake, alinieleza kila kitu kama nilivyoweka hapo juu.
na alilia sana yule binti jana. na asubuhi hii kaniambia amemueleza dada yake kila kitu, na dada yake amekesha analia, leo wanamtafuta Mshenzi mkubwa yule.
 
Em kuwa serious huyo binti hawezi kukuharibia nyumba yako.Muone huyu dada yake na umueleze tabia ya mdogo wake.Because unaweza kukmwita pempembeni akasema eti we ndo ulikuwa unamtaka.Na kama ukiwa unaongea naye hakikisha uko n rafiki yako unamuonya na sehemu ambayo ni ya wazi na mchana kweupe.ok brother
 
Mkuu yamaanisha hauna maamuzi yako binafsi hadi mkeo akusaidie????
Kuwa mwanaume mwenye maamuzi ya busara badala ya kujiharibia ndoa yako kisa kibinti km hicho.
Angalia usije mletea ngoma mama wawili, akashindwa kuja walea watoto wenu bureee. :A S-coffee:

Jamaa kamdondokea denti ....hakuna cha kuogopa wala nini!

Anapima upepo wa wana JF!!

Mtu mzima na mke na watoto, utashindwaje kudeal na mtoto wa shule, tena kwa kumkaripia??

Babu DC!!
 
Kiongozi, Yaani mpaka sasa hofu niliyokuwa nayo juu yake kunichanganyia mambo yangu haipo hata kidogo, kwanza Binti ananiona mimi kama mkombozi wake.

Japo alikataa kumueleza dada yake, yeye mwenyewe ameishamueleza na leo wanamtafuta Jamaa. hawa wadada inavyoonekana leo patakuwa hapatoshi na Jamaa na hii issue ni lazima iwe kubwa mtaani, mimi mwenyewe nimeishavaa safety Jacket nimemueleza Wife full story Jana Usiku kwa hiyo hata yakimfikia haitokuwa news.

Na Binti anaonekana Kichwani ni safi ila haya mambo ndo yamekuwa yanamchanganya, anadai yeye alifail kwa bahati mbaya sana on her first form six seating ndo maana alikuwa na courage ya kureseat, form form aliscore division one ya pont kumi na tano.

Wanaume wote wa JF naomba tuwe mfano, tuwaache hawa watoto wasome shule Jamani tunawaharibia maisha yao.
 
Pole sana,mueleze mkeo kisa chote atakuelewa.Ila uache kujirahisi kama kugonga tano na vimalaya hivyo,yatakukukuta makubwa zaidi.
Kuna Binti mmoja kutokana na uzuri wake ililazimika abaki kwenye kumbu kumbu zangu
tangu mara ya kwanza tukutane Dukani Jirani na Maskani yangu. Baada ya nazani nilifanikiwa
kumuona mara ya pili akiwa amevaa school uniform ndo nikajua kwamba ni Mwanafunzi.

Sasa Jana Jioni, baada ya kufika home nikalazimika kwenda Bar Jirani na nyumbani ili nipate
serengeti zangu ndogo za baridi, nilipofika Bar nikakutana na Kijana mmoja mjanja mjanja
sana, na kafunga ndoa hivi karibuni, alikuwa akiingia Bar kama mimi, na sababu hatujaonana
muda mrefu tulipokariaba tukaanza kupeana salamu, hagi nyingi, vicheko, gonga sana mikono.
Haya yote tulifanya tukiwa jirani kabisa na meza ambayo kuna mabinti watatu walikuwa wamekaa
na sikuwa nimewali sababu niliishawapa mgongo pia by the time,

Sasa Jamaa akaniuliza, vipi wife kaishajifungua, sikumjibu bali nilimtolea simu na kuanza kumuonyesha
picha za uzao wangu, twe twins. a baby boy and a baby girl, nikamtajia na majina yao, sasa
huku jamaa akiwaanawashangaa matwins wangu kwenye simu, nikamsikia binti mmoja katika wale watatu
anayarudia majina ya watoto wangu, nikageuka kumuangalia, na yeye akawa ananiangalia, ikabidi nimpe
tano (nikagonga nae) huku namuambia uko juu hayo masikio sio ya kawaida - Na alikuwa ni yule
binti mzuri mwanafunzi. ndo apo nikagundua kumbe anapiga mvinyo pia, maswali mengi sana
yakapita kichwani mwangu muda huo huo, lakini nika let it go.

Then Jamaa huyu akaniambia vipi, karibu tukae mi niko na dada zangu hapa, nikakwepa, nikamueleza kuna
mtu namsubiri tunamaongezi hivyo ngoja nikakae palee, nikamplease kidogo na yeye akanielewa.

Cha Hajabu
Wakati naanza Serengeti ya Pili, Yule Jamaa akaja, akaniuliza, una mfahamu yule binti, nikamuuliza yupi,
akaniambia yule kanyoa nywele (binti mzuri), nikamueleza navyo mjua, na kwamba hata Jina wala anaishi
wapi au kusoma wapi sijui.

Jamaa Akafunguka
Hoo Binti anakaa na dada yake mtaa wetu huo huo (huyu kijana anaishi mbali ha hapa kidogo), akanielekeza
nyumba, na akaanza kunieleza anaishi na nani, ikabidi nimuwahi, kwani vipi? Hoo unajua huyu binti pale
kaja na rafiki zake, ili mimi kaniagiza kwako. "nikasema kimoyo moyo kazi imeanza". Oooh anakufahamu
sana, na amefurahi sana pale mlipogongesha mikono, "nikajua hili gemu kali". Oooh, na ameishaambiwa
mke wako mkorofi sana hivyo anaomba tuhame hapa twende sehemu ingine ana maongezi na wewe.
Nikamuuliza Jamaa, wewe unafanya nini na wale mabinti, mnaongea nao nini? Jamaa akaniambia tutaongea
mbele, akaniuliza tunaenda wapi. nikamuambia akamuuliza huyo binti anataka twende wapi, Ile Jamaa
anasimama tu kuelekea kwenye meza ya wale mabinti. Nikampigia simu wife aje Bar haraka sana, na fasta
nikawaagizia ile meza vinywaji na nikalipa. Wife alipikuja nikamuambia nikamuambia nilijisau kuja na pesa
Bar kwa hiyo kama kaja nayo anilipie bia mbili tuondoke, akakubali akalipa na tukaondoka. nikawa
nimemkwepa Ibilisi.

Tatizo ni kwamba, Nimeamua kutoa mchapo huu, sababu mchana huu, Nimepokea message iliyotoka kwa
huyo binti inasema
"Babbie, Pole na Kazi, Jana Mke wako aliharibu mipango yetu, mi nshatoka shule, naomba unieleze nikufuate
wapi ukishatoka Job, Loving you. Jina"

Hapa nimechanganyikiwa, namtafuta huyu rafiki yangu kwenye simu kumuuliza kwa nini kampe yule binti
number yangu, simu haipatikani. Na ninajiuliza huyu mtoto nikimkimbia zaidi na ndio kaanza kutuma mimessage
hili swala litajulikana kwa mama wawili sasa hivi.

Naomba ushauli wenu, ninachokifikiria nimuelekeze sehemu tukutane alafu nimcouncil kujihepusha na haya
mambo. Au ndio ntakuwa natenda wema kupita uwezo???
 
We jamaa ni muongo,form six ndo wameanza mitihan..how come useme wamemaliza mitihan
 
Mwambie mtoto mzuri unataka nini kama kamchezo subiri mpaka mama watoto apate ujauzito ehh ndo unaweza ukawa sub
 
kuwa mwanaume ni pamoja na kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi pale yanapotakiwa kufanyika... sipati picha kwa nini issue ndogo tu ya mtoto wa shule ikichukulie energy na muda wote huo ku-deal nayo
 
Back
Top Bottom