Hawa wanawake siyo wema

Hawa wanawake siyo wema

Innocent Kirumbuyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
4,642
Reaction score
4,476
Mwaka 2013 nakumbuka ilikuwa ni mwezi wa 6 nilipofika Tabora nikitokea Tanga ambako nilikaa kwa miaka miwili, nilipofika Tabora nikatokea kumpenda sana msichana mmoja aitwae Suzy wa Tabora.

Japo nae alionyesha kuwa ananipenda ila hakuwahi kunikubalia kuwa pamoja nae, kila nilipomtaka aje kunitembelea alinidanganya kwa maneno mazuri. Lakini kila alipokuwa na shida ya pesa mimi nilimtimizia ili ajue kuwa nampenda kweli.Siku moja Suzy aliniita kwao nikaenda mimi na rafiki yangu Jaffary mtu wa Geita.

Tulipofika tukapewa viti, kwa bahati nzuri kwao alikuwepo yeye mwenyewe na rafiki yake aitwae Neema. Tulipofika akaniambia kuwa ameniita ili kunitamburisha kwa rafiki yake Neema, sasa cha ajabu alikuwa hajui kama mimi ni msukuma wa Kasamwa, ila yeye nilivyokutana nae nikitokea Tanga alijua mimi ni Mtanga. Akaanza kuongea kwa kinyamwezi na kinyamwezi na kisukuma ni yale yale. Akawa anamwambia yule rafiki yake Neema kwa kinyamwezi kuwa "unamuona huyo mvulana mwenye shati jeupe?

Neema akajibu ndio, Suzy akaanza kuelezea sasa kwa kinyamwezi; Huyu ndio yule mtanga huwa nakwambia kuwa ananisumbua kunitongoza ila mimi huwa simtaki, lakini ni king'ang'anizi sana"rafiki yake Neema akamuuliza;kwani uliwahi kumwambia kuwa humtaki?

Akajibu kuwa sijamwambia ila angekuwa ni kijana mwenye akili timamu angejiongeza mapema maana huwa kila akinitaka mi namchenga ila nikiwa nina shida ya pesa nikiomba tu ananipa) yule rafiki yake akanitazama kwa huruma kabisa, kisha mimi ili kujifanya kuwa hatuelewi wanachoongea nikauliza kuwa mnatusema eti? My Suzy akanijibu kwa sauti ya upole kuwa hapana baby ninamtamburisha rafiki yangu sema tu kwa kuwa nyie hamjui kinyamwezi ndio maana mnadhani tunawasema.

Kisha Suzy akaendelea kumwambia Neema kuwa "yaani amenitongoza siku nyingi sana ila namzungusha ili ajielewe lakini ni kupe huyu" Neema akauliza "kwanini unamfanyia hivyo? Si bora ungemwambia ukweli kuliko kumpotezea muda na pesa zake bure" Suzy akajibu "sio nampotezea muda na pesa zake bure, bali anajipotezea yeye mwenyewe na hata sasa hivi alikua anataka niende nae kwake alipopanga ila nimekataa na nitamuomba pesa hapa hapa mbele yako uone kama ataninyima"

Sasa muda wote huo mimi na rafiki yangu Jaffary tulikuwa tunasikia na kuelewa kila kitu na Jaffary alipotaka kucheka nilimgusa ili asicheke.Suzy akamaliza kunitambulisha akaniomba elfu 5 kuwa ana shida nayo.

Nikaingiza mkono mfukoni nikatoa elfu 5 na kumpa na siku hiyo nilikuwa na hiyo hiyo elfu 5 tu. Rafiki yangu Jaffary aliniangalia kwa jicho la hasira ila mimi sikujali maana nilijua nikifanyacho.

Suzy akapokea kisha akaniambia "bai baby wangu"na mimi nikajibu, bai my dear kisha tukaondoka, hatimae leo imetimia miaka mitano tangu nipate aibu ambayo sitawahi ipata tena toka kwa wanawake.
 
Ilitakiwa aongeze na ‘mpumbavu’ juu ya hiyo kupe. Yani anatoa mfano kabisa kuwa atakuomba hela na wewe utatoa na bado unatoa?
Hata hivyo pole mkuu kwa kupenda ambapo hukupendwa.
Ilipaswa umpe huyo rafiki yake hiyo 5000 na umtongoze hapo hapo maana inaelekea alikuwa anakuonea hurumu kulinganisha na huyo ‘My Suzy’ wako.
 
Mhhhhhhhh mapenzi tena basi
 
Hujamalizia vizuri mkuu, mliachanaje?
 
Mwaka 2013 nakumbuka ilikuwa ni mwezi wa 6 nilipofika Tabora nikitokea Tanga ambako nilikaa kwa miaka miwili, nilipofika Tabora nikatokea kumpenda sana msichana mmoja aitwae Suzy wa Tabora.

Japo nae alionyesha kuwa ananipenda ila hakuwahi kunikubalia kuwa pamoja nae, kila nilipomtaka aje kunitembelea alinidanganya kwa maneno mazuri. Lakini kila alipokuwa na shida ya pesa mimi nilimtimizia ili ajue kuwa nampenda kweli.Siku moja Suzy aliniita kwao nikaenda mimi na rafiki yangu Jaffary mtu wa Geita.

Tulipofika tukapewa viti, kwa bahati nzuri kwao alikuwepo yeye mwenyewe na rafiki yake aitwae Neema. Tulipofika akaniambia kuwa ameniita ili kunitamburisha kwa rafiki yake Neema, sasa cha ajabu alikuwa hajui kama mimi ni msukuma wa Kasamwa, ila yeye nilivyokutana nae nikitokea Tanga alijua mimi ni Mtanga. Akaanza kuongea kwa kinyamwezi na kinyamwezi na kisukuma ni yale yale. Akawa anamwambia yule rafiki yake Neema kwa kinyamwezi kuwa "unamuona huyo mvulana mwenye shati jeupe?

Neema akajibu ndio, Suzy akaanza kuelezea sasa kwa kinyamwezi; Huyu ndio yule mtanga huwa nakwambia kuwa ananisumbua kunitongoza ila mimi huwa simtaki, lakini ni king'ang'anizi sana"rafiki yake Neema akamuuliza;kwani uliwahi kumwambia kuwa humtaki?

Akajibu kuwa sijamwambia ila angekuwa ni kijana mwenye akili timamu angejiongeza mapema maana huwa kila akinitaka mi namchenga ila nikiwa nina shida ya pesa nikiomba tu ananipa) yule rafiki yake akanitazama kwa huruma kabisa, kisha mimi ili kujifanya kuwa hatuelewi wanachoongea nikauliza kuwa mnatusema eti? My Suzy akanijibu kwa sauti ya upole kuwa hapana baby ninamtamburisha rafiki yangu sema tu kwa kuwa nyie hamjui kinyamwezi ndio maana mnadhani tunawasema.

Kisha Suzy akaendelea kumwambia Neema kuwa "yaani amenitongoza siku nyingi sana ila namzungusha ili ajielewe lakini ni kupe huyu" Neema akauliza "kwanini unamfanyia hivyo? Si bora ungemwambia ukweli kuliko kumpotezea muda na pesa zake bure" Suzy akajibu "sio nampotezea muda na pesa zake bure, bali anajipotezea yeye mwenyewe na hata sasa hivi alikua anataka niende nae kwake alipopanga ila nimekataa na nitamuomba pesa hapa hapa mbele yako uone kama ataninyima"

Sasa muda wote huo mimi na rafiki yangu Jaffary tulikuwa tunasikia na kuelewa kila kitu na Jaffary alipotaka kucheka nilimgusa ili asicheke.Suzy akamaliza kunitambulisha akaniomba elfu 5 kuwa ana shida nayo.

Nikaingiza mkono mfukoni nikatoa elfu 5 na kumpa na siku hiyo nilikuwa na hiyo hiyo elfu 5 tu. Rafiki yangu Jaffary aliniangalia kwa jicho la hasira ila mimi sikujali maana nilijua nikifanyacho.

Suzy akapokea kisha akaniambia "bai baby wangu"na mimi nikajibu, bai my dear kisha tukaondoka, hatimae leo imetimia miaka mitano tangu nipate aibu ambayo sitawahi ipata tena toka kwa wanawake.
Ungekuwa na uwezo wa muendelezo wa part 2 hii ungeuza kwa Mtitu kufidia nusu hasara.

Kama sterling ningekuwa mimi huyo rafiki angeliwa faster kuliko hata upesi.

Kuna watu mnatutia aibu wanaume, hii si aibu yako bali aibu yetu, yani kamchezo ka kazungurukee hukajui?

Mwanamke mshenzi kama huyo unamla yeye, dada zake, rafiki zake na ikibidi mama mtu.
 
dada alifanya magic na wewe kweli ukatoa elfu 5,duh!
 
Wenzako Huwa Wanakula Marafiki Wa Mademu Zao
Sasa Wew Umeshindwa Nini Hapo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom