Hawa wanafaa kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA!

Hoja safi lakini muda siyo mwafaka tafadhali itunze tutaijadili 2014.

mbona za ccm tunazijadili humu humu sasa tena rais wao akiwa bado madarakani kwa hii isubiri mpaka kumekucha,tuanze sasa ili tuwe na muda mzuri wa kuchunguza nyendo zao maana tunataka tupate mr.clean miongoni mwao!
 
ZITTO FOR CHADEMA,ZITTO FOR CHANGE,ZITTO FOR TANZANIA...Vijana tumsupport kijana mwenzetu tuachane na watu wenye damu za TANU na CCM,tutachugue watu ambao hawajawahi kumili kadi yenye nembo ya jembe na nyundo,tuchague watu ambao hawajawahi kukimbiza mwenge wala kushiriki mbio za mwenge,watu hao ni hatari sana hawaoni mbele wanauona mwenge kila wanapotembea,wanapolala,wanapokula...bado wanaamini eti mwenge ukiwekwa kwenye kilele cha mlima kilimanjaro utawamulika maadui,uongo mtupu!

Ni mawazo yako mkuu,lakini kwa ZK is a big NO!nahisi ni rahisi kurubunika huyu mtu,wa kuogopwa kama ukoma
 
Dr. Slaa
Halima Mdee
Zitto Kabwe
John Mnyika

Siyo kwa umuhimu. Sijajua umri wao lakini chochote chaweza kutokea kabla ya 2015 na kuwapa nafasi kiumri.
 
kumekuwa na fikra ama dhana potofu miongoni mwa vyama mbadala tanzania kwamba wagombea urais kupitia vyama hivyo ni lazima wawe wenyeviti ama makatibu wakuu wa vyama hivyo,huu sasa unaonekana kama ni utamaduni uliozoeleka kwenye vyama vya upinzani,kwa kuwa chadema ni chama za kidemokrasia zaidi naona kingejaribu kuonyesha njia kwa kujitofautisha na vyama vya kisultani(tunavijua)kwa kuanzi chadema kwenye uchaguzi ujao kimteue mgombea wake kutoka nje ya utaratibu huo unaobaka demokrasia hapa nchini,wapo watu wenye uwezo ndani ya chadema ambao wakisimamishwa wanaweza kutoa changamoto ya kutosha kabisa hasa ikizingatiwa chadema kama vyama vingine vimesharibu kuwasimamisha mwenyekiti aliyeko madarakani pamoja na katibu wake bila mafanikio,mfano wa watu mahiri ndani ya chadema ambao wanao uwezo mkubwa wa kuipeperusha bendera ya chama ni hawa wafuatao,hebu tujaribu kuwachambua na kupima kuona yupi ni bora zaidi hapa

mh.tundu lissu

mh.zitto kabwe

prof.safari

mh.halima mdee

kichuguu'
 
Kila mtu ana haki ya kukijadili chama chochote na hoja yeyote inayowasilishwa hapa akiona inafaa kufanya hivyo,msizuie watu kuleta wala kujadili hoja hapa ndio pahala pake,the house of great thinker!hatuzimi hoja hapa.

THE ROMANTIC;

Hakuna mtu anayependa kujadili aliyezuiwa kujadili,kwamba kila mtu anapost kwa kutumia simu au kompyuta yake huko alipo then yuko huru kuchangia anapoona inafaa,Kwa maana hiyo then wale wanaoona hii inafaa kujadili uteuzi wa mgombea wa urais sasa ikiwa miaka mitatu kabla ni sawa,then ni ruksa wakiendelea.

Lakini jambo moja la msingi,CHADEMA inajipambanua sana na vyama vingine kama CCM na CUF,Katika kujipambanua huko sisi wana CHADEMA tunaona si busara kujadili mambo ya uteuzi wa urais kwa sasa.Kuna mambo mengine ya msingi na changamoto ambazo zinatukabili kwa sasa,ambazo lazima kuzi adress kwa muda huu.Tunapenda kufanya KILA JAMBO KWA WAKATI WAKE.Pia tunapenda kuweka PRIORITIES.

Kwa hiyo.Kama kuna mtu awaye yote anayedhani anahitaji kuchangia aendelee kuchangia,lakini hatakuwa CHADEMA kwelikweli kwa sababu huo sio utamaduni wetu.Ninyi endeleeni kujadili expected candidates wetu according to nyie.

Asante.Nawasilisha
 
issue si kuleta changamoto kwenye uchaguzi tu bali uwezo wa kuwaondolea wananchi umaskini tulio nao atayeweza kuthubutu kufanya kwa makusudi
 
VOTE FOR CHADEMA

VOTE FOR HALIMA

VOTE FOR CHANGE

157427_100001425908463_4956608_n.jpg

Mh.Halima Mdee

wanachadema wenzangu kama kuna mahali ccm huwa wanatuzidi maarifa ni kwenye kura za kinamama,naseama hivi kwa uzoefu kwa kuwa nimekua mtumisji wa ccm makao makuu dodoma na hapa lumumba for years,mzee slaa tusimtupe,yeye abaki kumarisha chama ikiwa ni pamoja na kumuandaa mgombea wetu halima ambae atatupatia kura nyingi za kina tutakazochanganya na za vijana ambazo ccm hawana,slaa amekaa kiutendaji zaidi anafaa kuwa waziri wetu mkuu baada ya rais wa kwanza mwanamama HALIMA MDEE Kutinga ikulu.

Hii ni mara yangu ya kwanza kuchangia japo nimekua mshiriki wa muda mrefu kama msomaji tu.
 
THE ROMANTIC;

Hakuna mtu anayependa kujadili aliyezuiwa kujadili,kwamba kila mtu anapost kwa kutumia simu au kompyuta yake huko alipo then yuko huru kuchangia anapoona inafaa,Kwa maana hiyo then wale wanaoona hii inafaa kujadili uteuzi wa mgombea wa urais sasa ikiwa miaka mitatu kabla ni sawa,then ni ruksa wakiendelea.

Lakini jambo moja la msingi,CHADEMA inajipambanua sana na vyama vingine kama CCM na CUF,Katika kujipambanua huko sisi wana CHADEMA tunaona si busara kujadili mambo ya uteuzi wa urais kwa sasa.Kuna mambo mengine ya msingi na changamoto ambazo zinatukabili kwa sasa,ambazo lazima kuzi adress kwa muda huu.Tunapenda kufanya KILA JAMBO KWA WAKATI WAKE.Pia tunapenda kuweka PRIORITIES.

Kwa hiyo.Kama kuna mtu awaye yote anayedhani anahitaji kuchangia aendelee kuchangia,lakini hatakuwa CHADEMA kwelikweli kwa sababu huo sio utamaduni wetu.Ninyi endeleeni kujadili expected candidates wetu according to nyie.

Asante.Nawasilisha

Umepata ridhaa wapi ya kuwasemea wanachama wote wa chadema humu ndani?kama dio hicho kikao cha kukuteua wewe utoe statement ya pamoja kiliketi saa ngapi na wapi?acha udikteta mbuzi kijana,zungumza ya kwako usiwasemee wengine!unless wewe ni Nape wa chadema!mbona vijana wa kitz mnapenda sana vyeo?
 
thamani ya shilingi imeshuka,bei za bidhaa ziko juu,katiba mpya haijapatikana,wanafunzi vyuo vikuu bado wananyanyasika.........................ndio rais ajaye huyo.
 
thamani ya shilingi imeshuka,bei za bidhaa ziko juu,katiba mpya haijapatikana,wanafunzi vyuo vikuu bado wananyanyasika.........................ndio rais ajaye huyo.
VIPI KUHUSU LOWASSA,MEMBE NA SITTA nao tusiwajadili tena hapa au?mi nadhani huu ndio muda muafka tuwajue tuanze kuwa pembua mpaka ikifika wakti tutajua pumba ziko wapi na mchele uko wapi,tukisubiri mpaka mwisho tutakuja okota garasa!
 
Acha kujifanya unaipenda sana chadema! Wewe si juzi tu ulikuwa unabishana na mwita maranya! Wewe nenda kawashauri magamba wenzako huko!
 
Mimi hata jamaa zangu wa ccm nawaambia tuachane na wanasiasa waliolelewa na kukuzwa na TANU YOUTH LEAGUE hawatakua na jipya wawe upinzani wawe ccm,hawa watu ndio wametufikisha hapa;vijana kama hawa kina Halima mdee,zitto kabwe,Tundu,lema nampenda kama angejua amesoma ndio wanaoweza kuipeleka hii nchi mbele...watu waliopitia TANU YOUTH LEAGUE wameprove failure kupitia mkapa na Jakaya,tatizo walibanwa sana na nyerere akiwa hai sasa wakipata chance wanakua kama wanakomoa.Mimi katika hao hapo juu namuunga mkono Tundu Lisu,huyu anaweza kabisa kuleta mabadiliko kwanza sio mwanasiasa,hiyo ni sifa ya kipekee kabisa miongoni mwa wengi wanaotajwa,ila tatizo langu kwa chadema ni jinsi ya kuwashawishi waislam wakiamini baada ya ya zile propaganda za ccm katika uchaguzi uliopita kuwa zimewaingia sana,so pengine ni wakati muafaka kufikirir fikiria kuwa na mgombea muislam ili kuwapiga bao ccm ambao inavyoelekea watamsimamisha mkatoliki tena!maana nao wana kaujinga ka kupendelea wakatoliki na waislam tu kutawala nchi hii!
 
Acha kujifanya unaipenda sana chadema! Wewe si juzi tu ulikuwa unabishana na mwita maranya! Wewe nenda kawashauri magamba wenzako huko!

kwani huyo ndio nembo ya chadema humu ndani?suala la urais si suala la chadema peke yao au ccm peke yao ni la wote,tunamzungumzia rais wa nchi mzee sio rais wa chadema,ni kama suala la katiba huwezi kusema ni la kwetu chadema tu hapana ni la kitaifa.Mi nadhani mdee anafaa.

157427_100001425908463_4956608_n.jpg

VOTE
HALIMA MDEE

FOR PRESIDENT

JK mwenyewe chadema damu kwa taarifa yako,we endelea kuamini jk ni ccm,subiri amalize urais,atakuja mbanane huko huko,yeye alichokuwa anataka ni urais na keshaupata...wanaongea mengi sana na wewe hata slaa hamjui ila mtajulishwa wakati muafaka ukifika!hiyo ndio siasa!kuna mtu aliwahii hata kuhisi cuf na ccm zenj watakuja kufanya kazi pamoja?
 
Haya ndio mambo tunayoyataka unaona bwana sio watu wengine ooooh ni mapema sana kujadili mnataka kuficha nini ilhali urais haugombewi chumbani na wala huko sio mahala kwake bali hadharani?ok mkuu sasa unazo sababu zozote za kuwakataa hao na kuwakubali wawili Bi.Halima na mwenzake tundu?

safari na zitto hawa hawana nafasi ni wadini hawa. Mambo yote mbowe
 
Umepata ridhaa wapi ya kuwasemea wanachama wote wa chadema humu ndani?kama dio hicho kikao cha kukuteua wewe utoe statement ya pamoja kiliketi saa ngapi na wapi?acha udikteta mbuzi kijana,zungumza ya kwako usiwasemee wengine!unless wewe ni Nape wa chadema!mbona vijana wa kitz mnapenda sana vyeo?

Mkuu KIM KARDASH;

Heshima kwako kwanza;

Wewe unacheza na propaganda za kujaribu kuleta mijadala ambayo haipo CDM,Lengo unataka kutuaminisha kwamba sisi attention yetu ni kwenye Uraisi kwa sasa.Tumeshakuelewa.Nimekujibu kwa hoja kwamba kama unapenda kuendelea kujadili endelea,kwa sababu kuna freedom of Speech.LAKINI hiyo sio PRIORITY yetu kwa sasa CHADEMA.Ukaishia na ati " Udikteta Mbuzi".Sijatoa maoni ya kukuzuia kujadili,Go on lakini elewa nilichosema,na je katika nilichosema kuna lolote ambalo unaona sio msimamo wetu CDM?

Swala la Authority ya kusema haya usihangaike sana kwa sababu hata wewe sikujui.Lakini huu ndio msimamo wetu.Ninyi hamuwezi kututeteresha.Again endeleeni kujadili Expected Candadates wetu according to Ninyi.

Asante Mh.KIM
 
Kwa mtindo huu ata Vincent Nyerere (Mbunge wa Musoma Mjini) atatajwa kwenye orodha ya wanaofaa kuwa Rais wa Nchi hii 2015.
 
Back
Top Bottom