Hawa wanafaa kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA!

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
Kumekuwa na fikra ama dhana potofu miongoni mwa vyama mbadala tanzania kwamba wagombea urais kupitia vyama hivyo ni lazima wawe wenyeviti ama makatibu wakuu wa vyama hivyo,huu sasa unaonekana kama ni utamaduni uliozoeleka kwenye vyama vya upinzani,kwa kuwa chadema ni chama za kidemokrasia zaidi naona kingejaribu kuonyesha njia kwa kujitofautisha na vyama vya kisultani(tunavijua)kwa kuanzi chadema kwenye uchaguzi ujao kimteue mgombea wake kutoka nje ya utaratibu huo unaobaka demokrasia hapa nchini.

Wapo watu wenye uwezo ndani ya chadema ambao wakisimamishwa wanaweza kutoa changamoto ya kutosha kabisa hasa ikizingatiwa chadema kama vyama vingine vimesharibu kuwasimamisha mwenyekiti aliyeko madarakani pamoja na katibu wake bila mafanikio,mfano wa watu mahiri ndani ya chadema ambao wanao uwezo mkubwa wa kuipeperusha bendera ya chama ni hawa wafuatao,hebu tujaribu kuwachambua na kupima kuona yupi ni bora zaidi hapa
9.jpg

Mh.Tundu Lissu

269398_218120438224649_116393691730658_547970_3290987_n.jpg

Mh.Zitto Kabwe

safari_236.jpg

Prof.Safari

157427_100001425908463_4956608_n.jpg

Mh.Halima Mdee
 
Usitupotoshe.Muda haujafika wa kuzungumzia hayo.Tujadili agenda za kitaifa zinazowasumbua wananchi.Matatizo ya kiuchumi hayajatatuliwa.CDM ina utaratibu wa kumtafuta mtu anayefaa kusimamishwa.
 
Nimehamua kuwatenga na kuwapeleka mahakani wana siasa wote watakao anza kujadili mambo ya urais kabla ya wakati haujafika manake ni kinyume cha sheria ya maadili ya uongozi kujadili mambo hayo.
 
Wewe ccm unahangaika nini na chadema?
mi chama changu cha walipa kodi tanzania CCWT na pia ni mwanachama wa chama cha wapiga kura Tanzania ndio tunahangaikia usajili bado hivyo kwa sasa lazima tushiriki kuhakikisha kila chama kinasimamisha wagomea wenye mashiko,uchaguzi mkuu ni suala la kitaifa zaidi kuliko kichama ndio maana hutoniona hata siku moja natoe maoni nani wanafaa kugombea uenyekiti wa chama,urais ni wa wote hauna chama,amkeni vijana.
 
Dada peleka unafiki wako hukohuko CCM sisi huku CDM hatunaga taratibu kama zenu za Kimagamba na huu sio muda wa kujadili haya mambo wakati kuna mambo ya msingi ya kujadili mfano Ukosefu wa Ajira,namna gani Mafisadi tunaweza yatokomeza,kupanda kwa gharama za maisha n.k sasa ww unaleta upuuzi wako hapa? Endeleeni na harakati zenu na akina Sitta,Membe na Manywele
 
Ndugu yangu acha jazba,rais wa nchi yetu kwa hali ya kukomaa kwa demokrasia ilivyo anaweza kutokea chama chochote kati ya hivi viwili ccm na cuf,hivyo ni lazima wanaotajwa tajwa pande zote mbili wapitie hapa ili angalau tujiridhishe ya kwamba tumepanda wagombea bora kutoka vyama hivi viwili ili tuwe pia na uhakika na kumfahamu sawasawa mtu tunaetegemea kumkabidhi maisha yetu.Kwanini lakini inakuwa rahisi sana humu ndani kujadili mambo na ya ccm ya chadema watu wanajaribu kufanya jitihada za makusudi kuyazima,chadema ni chama chetu watanzania kama ilivyo ccm na kina lengo la kushika dola siku moja lazima tukijadili na kuwachambua wanaokizunguka kama tunavyofanya kwa ccm,kwanini hamtaki hii,mnajaribu kuficha kitu gani?
 
Kua muelewa Kim,huu sio muda wake wa kujadili haya haijalishi yupo au hayupo umdhaniae rejea maelezo yangu hapo juu la utakua na tatizo la kuelewa mabandiko ya wengine
 
Kila mtu ana haki ya kukijadili chama chochote na hoja yeyote inayowasilishwa hapa akiona inafaa kufanya hivyo,msizuie watu kuleta wala kujadili hoja hapa ndio pahala pake,the house of great thinker!hatuzimi hoja hapa.
 
Kua muelewa Kim,huu sio muda wake wa kujadili haya haijalishi yupo au hayupo umdhaniae rejea maelezo yangu hapo juu la utakua na tatizo la kuelewa mabandiko ya wengine

ila kwa wanaotajwa tajwa ccm kuwajadili ruksa sio?kwanini chadema unapenda iwe exceptional case labda?zipo sababu zozote za msingi unazo za kufanya hivyo labda?zitaje.
 
Wote hapana; Chadema ijipange zaidi kwenye majimbo 2015 huku ikimuandaa Mr. Mnyika for Urais 2020 kwani atakuwa amefikia umri wa miaka 40;
 
ZITTO FOR CHADEMA,ZITTO FOR CHANGE,ZITTO FOR TANZANIA...Vijana tumsupport kijana mwenzetu tuachane na watu wenye damu za TANU na CCM,tutachugue watu ambao hawajawahi kumili kadi yenye nembo ya jembe na nyundo,tuchague watu ambao hawajawahi kukimbiza mwenge wala kushiriki mbio za mwenge,watu hao ni hatari sana hawaoni mbele wanauona mwenge kila wanapotembea,wanapolala,wanapokula...bado wanaamini eti mwenge ukiwekwa kwenye kilele cha mlima kilimanjaro utawamulika maadui,uongo mtupu!
 
Wote hapana; Chadema ijipange zaidi kwenye majimbo 2015 huku ikimuandaa Mr. Mnyika for Urais 2020 kwani atakuwa amefikia umri wa miaka 40;

Huyo pia mimi nilimfikiria lakini nilipo jaribu kudurusu kiwango chake cha elimu nilisikitika sana.....labda kama atajiendeleza hata open university maana umri unamruhusu!
 
Huyo pia mimi nilimfikiria lakini nilipo jaribu kudurusu kiwango chake cha elimu nilisikitika sana.....labda kama atajiendeleza hata open university maana umri unamruhusu!

Huyu mtu alikuwa ni straight 'A' student P.C.M sekondari, na akaenda mlimani na division I, lakini kutokana na hulka yake ya uana harakati, wakam disco kwa makusudi; Ni kweli akijiendeleza litakuwa jambo la busara sana;
 
mwambieni afanye maarifa arudi shule tunataka kuwapa nchi vijana machachari kama yeye lakini shule kwanza!
 
Kati ya ulowataja, futilia mbali Prof. Safari na Zitto. Hawafai

Haya ndio mambo tunayoyataka unaona bwana sio watu wengine ooooh ni mapema sana kujadili mnataka kuficha nini ilhali urais haugombewi chumbani na wala huko sio mahala kwake bali hadharani?ok mkuu sasa unazo sababu zozote za kuwakataa hao na kuwakubali wawili Bi.Halima na mwenzake tundu?
 
Back
Top Bottom