Hawa wanafaa kuandaliwa kwa ajili ya Urais 2040, siyo dhambi tuwajenge tufaidike

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,200
27,252
Moja ya sababu kubwa ya nchi nyingi kutoendelea ni kutoandaa viongozi kwa ajili ya vizazi vijavyo na vijavyo.

Leo Mimi countrywide msomi ninatoa maoni yangu kuhusu kuandaa watu Hawa kwa ajili ya uraisi 2040.

Ningeweza kusema 2030 lakini naona ni karibu sana kiasi ambacho itakua sio Tena maandalizi bali mkurupuko.

Hawa wanafaa, tuwajenge tuwaunge mkono;

1) Nickson Simon (Nikki wa Pili)
- Kama wengi wanavyomuita genius, ndivyo ambavyo uhalisia ulivyo. Nikki ana uwezo mkubwa wa akili na anapaswa kuandaliwa kwa ajili ya uraisi 2040. Ni aina ya kijana ambae amezaliwa kioungozi.
Ni msomi, mcha Mungu, muadilifu, mnyenyekevu, msikivu, mkali kwa wazembe. Hakika wakati ni sasa kumuandaa.

2) Innocent Bashungwa
- Jina hili linapaswa kuwemo kwenye orodha ha viongozi wakubwa baadae. Na itakuwa vyema akiandaliwa kuja kuwa raisi wa baadae. Mapungufu yapo Ila anaweza kuandaliwa vizuri na kuyaondoa hayo mapungufu.

3) Juma Aweso
- nashauri akae kwenye nafasi ya uwaziri kwa muda mrefu ili apate zaidi uzoefu baadae atatufaa Sana. Najua ana mapungufu yake Ila system inaweza kumjenga na kuyaondoa.
Ana future nzuri Sana

4) Mashaka mrisho Gambo
- huyu amejipambanua kuwa ni mmoja wa vijana hodari na wenye kaliba ya uongozi.
Ana mapungufu yake Ila yanaweza kurekebishwa na kuja kuwa raisi na hakika tunaweza fika mbali.

5) Anthony Mavunde
- mbunge wa Sasa wa Dodoma ni moja ya watu potential sana miaka ya baadae na akiandaliwa mapema atakuja kuwa kiongozi mzuri sana na mkubwa nchini.
Hao wote Hadi kufika 2040 watakuwa na umri ww miaka 55-60, hivyo utakua wakati muafaka Sana kwao kuwa maraisi. Lakini ninaomba waandaliwe sasa.

 
Chama cha Mapinduzi hakina mtu anayefaa kuwa Rais wa Tanzania, labda rais wa mafisadi, wala rushwa na wahujumu uchumi
 
Eti msomi?
Burundi kuna shule gani za kukufanya uturingie hapa tanzania ambako upo ukimbizini?
 
SISI TUMEKUANDAA WEWE SIO HAWA......SAWA SAWA?
 
Ndipo tunapoangukaga watanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…